Fursa kwa wana IT: Wateja wanahitaji Kariakoo ya mtandaoni inayofanana na Alibaba.Com, kama una uwezo chukua hatua bila kusita

Mbona zipo kaka,

Nida Danish
www.nidadanish.com

www.shoponline.co.tz

Kupatana.com

Jiji.co.tz

Na zingine zingi
Hizi bado mkuu,I mean something like alibaba.com ambapo itakuwa specific eneo moja ambalo ni kariakoo.Kama ni muuzaji kutoka sehemu nyingine tofauti na kariakoo hutaweza kujisajili.

To be specific,
Muuzaji atajisajili then atatuma zile document za TRA kuthibitisha yupo location ya kariakoo,atatakiwa kusema ni muuzaji wa reja reja au jumla,atatakiwa kusema duka lake lipo mtaa gani na atatakiwa kulipiga picha.Pia platform itakuwa na escrow ili wauzaji na wanunuaji walindane.Mwisho kutakuwa na algorithim ya kushindanisha bei ili wale wapigaji wasionekane.
 
Wauzaji wa online Tz Wengi Wana tamaa....wanaweka cha juu kiasi kikubwa Sana mwisho mtu unaamua kwenda kkoo mwenyewe...bado udanganyifu wa quality...unaweza uziwa used ukiamini mpya...
Platform itakuwa na algorithim ya kuwafanya wauzaji wacompete bei.Wale wa cha juu kikubwa kwenye bidhaa ambayo anauza bei ndogo atapata shida sana kuonekana kwenye platform.
 
Anhaa, hii ni wajasiriamali wanaotengeneza bidhaa zao na kuuza.

Na wateja sasa wa kununua hizo bidhaa.

Kwa hizo za wachina na viwandani vya nje ya Tanzania tayari kuna mitandao mingine. Hata features zake zinawafaa zaidi walio katika location za ndani
 
Wazo zuri tatizo ni utekelezaji katika mazingira ya kibongo. Changamoto kuu ikiwa ni nidhamu mbovu kwa wote, wanunuzi, wauzaji na wasafirishaji.
 
Wazo zuri tatizo ni utekelezaji katika mazingira ya kibongo. Changamoto kuu ikiwa ni nidhamu mbovu kwa wote, wanunuzi, wauzaji na wasafirishaji.
Kama kuna uwezekano wa kuwapa foreigners walitekeleze nayo kheli.


Ila tutakuwa wajinga sana.
 
Boss endelea kuwa winga. Hata hiyo alibaba imecover eneo dogo sana la china. Updates wafanyabiashara wachache sana wanafanya. Sema Amazon labda of which bado. Hata group za whatsapp wafanyabiashara wachache sana hupost product zao. Endelea kupiga hela kwenye uwinga, kuwa smart, mtiifu, mwaminifu na mvumilivu. Itatosha ww kuwa alibaba kkoo yetu.
Acha mawinga wapige pesa mzee
 
Mawazo ya kizamani haya.

Innovation ni kitu muhimu sana.
 
Jamaa ana wazo zuri ila halitekelezeki kwa nchi yetu. Wale wafanyabiashara wanaotakiwa kupost ndo huwa hawapost kabisa na mtamtafuta wenyewe. Na wao ndo chanzo cha neno CHIMBO. Na ni kweli huko China kuna ambao hawako kabisa Alibaba lakini wanapiga biashara.
 
Bado hujanishawishi kwamba wazo halitekelezeki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…