Wauzaji: uaminifu, kwa kuwa haupo pale kuchagua, anaweza kukuleta kitu kisicho na ubora, kisa anajua unaweza ona usumbufu kurudisha... pia wanatabia ya kuweka cha juu ambacho akiharisiki wakiamini kama wewe sio wa kwenda sokoni kuchagua basi kuna uwezekano mkubwa hujui bei halisi na una hela. Japo sio wote ila hizo ni baadhi ya kero za kawaida sana unaponunu kitu mtandaoni. Watatafuta tu namna ya kukuchakachua.
Wanunuzi: Kuna watu either hawajui wanachokitaka au sijui ni nini, unampelekea bidhaa bila kujua muda na gharama zako, anaweza kughairi wakati bidhaa ndo ishamfikia. Au anasema hicho alichokiagiza, Na vile issue ya physical address bongo bado changamoto, unapeleka bidhaa unafika karibu na eneo husika simu haipatikani, hupokelewi etc. bado kuna changamoto za kulipana kama ulitegemea kupokea cash bidhaa ikifika kwa mhusika, unafika unapigwa kiswahili, unapewa pungufu na mengineyo.
Wasafirishaji: mmewasiliana uletewe bidhaa muda fulani ni kawaida sana kukuletea visingizio lukuki kabla bidhaa kukufikia, unaweza kujikuta umepoteza siku nzima kububiri mtu wa derivery..
Japo japo sila mununuzi, muuzajia au mfanyabishara wa bongo yuko hivyo, ila wabongo kuheshimu muda watu, biashara ya mtu au hata shughuli yako mwenyewe inayokuingizia kipato bado changamoto kwa wengi bado hujakutana na lugha chafu.. kufika tutafika ila bado sana.