Fursa kwa wana IT: Wateja wanahitaji Kariakoo ya mtandaoni inayofanana na Alibaba.Com, kama una uwezo chukua hatua bila kusita

Mbona wapo wanaofanya biashara hiyo japo si kwa mtandao. Wao wanakataloji unachagua anakuletea, unamlipa bila mbambamba.
 
Hizo PDF hasa hio inayoelezea USER FLOW ina mambo mengi Sana (makelele) si rafiki kwa user na itamfanya aboreke, ungeandika Simple maelezo kirogo picha nyingi.

Ungetengeneza UI Design ya hizo sehemu au Kama haukua na UI Design hata unge screenshot then ungeweka screenshot hizo na maelezo kidogo.
 
Yas ni kweli

Kwa bongo tuna changamoto ya umakini na muda wa kutilia mkazo. 'Attention span' ni changamoto.
 
Una jicho la mbali
 
kwa hizi specs hapa, hii fursa kwa IT wa Bongo ! wallahi sahau
 
Sorry,nielezee namna wauzaji,wanunuzi na wasafirishaji watakosa nidhamu?
Wauzaji: uaminifu, kwa kuwa haupo pale kuchagua, anaweza kukuleta kitu kisicho na ubora, kisa anajua unaweza ona usumbufu kurudisha... pia wanatabia ya kuweka cha juu ambacho akiharisiki wakiamini kama wewe sio wa kwenda sokoni kuchagua basi kuna uwezekano mkubwa hujui bei halisi na una hela. Japo sio wote ila hizo ni baadhi ya kero za kawaida sana unaponunu kitu mtandaoni. Watatafuta tu namna ya kukuchakachua.
Wanunuzi: Kuna watu either hawajui wanachokitaka au sijui ni nini, unampelekea bidhaa bila kujua muda na gharama zako, anaweza kughairi wakati bidhaa ndo ishamfikia. Au anasema hicho alichokiagiza, Na vile issue ya physical address bongo bado changamoto, unapeleka bidhaa unafika karibu na eneo husika simu haipatikani, hupokelewi etc. bado kuna changamoto za kulipana kama ulitegemea kupokea cash bidhaa ikifika kwa mhusika, unafika unapigwa kiswahili, unapewa pungufu na mengineyo.
Wasafirishaji: mmewasiliana uletewe bidhaa muda fulani ni kawaida sana kukuletea visingizio lukuki kabla bidhaa kukufikia, unaweza kujikuta umepoteza siku nzima kububiri mtu wa derivery..
Japo japo sila mununuzi, muuzajia au mfanyabishara wa bongo yuko hivyo, ila wabongo kuheshimu muda watu, biashara ya mtu au hata shughuli yako mwenyewe inayokuingizia kipato bado changamoto kwa wengi bado hujakutana na lugha chafu.. kufika tutafika ila bado sana.
 
Lakini haya matatizo yote uliyoelezea hapa yanatatulika.Kwahiyo still there is chance
 
Huyu mleta uzi mwenyewe ni kijana wa hovyo na kujifanya mjuaji. Huyu aendelee kuwa winga tu. Kwa hii ego aliyo nayo anapoteza muda kufikiria jambo kama hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ