Fursa ya safari ya kibiashara China (kwa wajasiriamali wenye mitaji midogo)

Nadhani hii si safari mpya , niliziona kuanzia septemba 2023 , shida moja iliyojitokeza , hasa baada ya mamluki kupata taarifa hizi waliomba viza nyingi sana kwenye ubalozi wa China , wakapewa na kusafiri , lakini hawakupokelewa china na mamlaka za Wajasiriamali , walitokomea mitaani
 
This time ni tofauti maana wahusika wa huko wako hapahapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hapo kwenye mali kauli sasa.. me na mtaji kidogo nawaza ninunue mzigo alibaba ila naona kuna element za kupigwa unaeza nipa abc kidogo mkuu
 
Huu unaofanya ni ubatili, nitasema kwa nn na yoyote aliyekua excited na hii fursa awe makini sana

Umeiweka fursa kwa namna nzuri ya kuvutia, haya hufanywa na wote wanaiona fursa ndani ya fursa kama ilivyokua kwa Ontario, mr kuku, jatu, mr vanilla, kalyinda and the likes

Ukweli mchungu fursa yoyote nzur inayolipa haishirikishi watu public hivi. Kikawaida binadamu sisi ni wabinafsi, hiki niliwahi kumueleza Ontario kuwa Kama kweli forex inalipa hivyo unapata wapi muda wa siku nzima kufundisha watu? Huo muda si ungekua unatumia kuingiza hizo pesa za forex ili uwe bilionea zaidi? Kwamba pesa umezichoka?

Sasa mshana, ww unatafuta watu uwape semina na uwaeleze kuhusu kwenda china kuchukua bidhaa na utawasaidia kuanzia process za visa kusafiri watapofikia hadi masokoni wataponunua bidhaa. Muda wote huu utaoutumia ww malipo yako ni nn?umejitolea? Ukisema umejitolea hapa ndio umeandaa ubatili niliosema mwanzo
Kama kuna malipo basi ilipaswa kuyaweka wazi mapema kabisa.

Nimeona umesema utawapa pia watu bidhaa za mali kauli, hii ni namna ya kuvutia fursa uliyotangaza. Hii ni ubatili, labda ulikua unatania. Mali kauli haiwi rahisi hivi kama ulivyoiweka. Wapo wataoona nipo negative sababu tu ya kuvutiwa na maneno yako. Wabongo wengi ni rahisi kuwatapeli mtandaoni ukiweza tu kuwaaminisha watapata utajiri au fursa nzuri bure au kwa gharama ndogo

Msaada mkubwa na mzuri ulipaswa uweke post ueleze kuanzia mwanzo wa anavyotakiwa kufanya kukata ticket na gharama average zipo vipi, kuproces visa na njia ipoje na gharama zipo vipi, kusafiri, hotel huko average gharama zipo vipi, wapi pa kufikia, masoko yalipo na masoko yalipo contacts zao, watumie kampuni ipi kwa shipping
Kutokea hapo anayetaka angejipima, na kwa msaada zaidi angekutafuta pale alipokwama. Lakini hii yako haina tofauti na kina Ontario, mr kuku, jatu n.k
 
Hii ya mali kauli imekaaje??
 
Kuagiza on-line kwa kweli muda mwingine shipping costs zinakuwa kubwa sn. Unakuta bei ya kununulia ni ya kawaida Ila shipping balaa. Labda uwe unapata za free shipping. Mimi ni mteja mzuri wa AliExpress, wako poa sn.
 
Good analysis comred
 
hii ni Light on Dark aise kwa tusojua chochote kuhusu jambo hili...

ile shauku ambayo iko na wengi kwenda China for business, kwa fundisho hili lenye tahadhari kama zote,

ata ukipigwa pesa zako kuna wa kumlaumu kweli ndrugu zango?

ni vizuri sana kua makini na wale wote wenye nia njema za kuinua jamii kiuchumi na hata huyu mjamaa hajamkataza mtu wala kumkatisha mtu tamaa ila kwa kiasi kikubwa ameonyesha mwanga kwa mifano,

for sure amewasha Nuru Gizani kwetu sote ngoja tumsubiri mtoa hoja kwa mrejesho na muongozo zaid ili tupate undani wa hatua ya mwanzo, kuingia, kuishi china na kurudi home kwa salama na amani...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…