Fursa ya safari ya kibiashara China (kwa wajasiriamali wenye mitaji midogo)

Kimepanda kimeshuka ntantarira nyingi. Unataka kuwapiga watu vihela vyao huna lolote
 
Halafu mkuu imagine mtu anaaminishwa 6m itamtosha kwenda na kurudi China huku akiwa kanunua mzigo. Nimesema hiyo hela si bora apewe yeye Mshana awaagizie watu ila baadae mitaji ikikua waende wenyewe? Bado wanabisha.
 
Halafu mkuu imagine mtu anaaminishwa 6m itamtosha kwenda na kurudi China huku akiwa kanunua mzigo. Nimesema hiyo hela si bora apewe yeye Mshana awaagizie watu ila baadae mitaji ikikua waende wenyewe? Bado wanabisha.
Nadhani tumpe muda mtoa fursa kwani amesisitiza information nyingi na ufafanuzi atautoa next week ambayo inaanza kesho.
 
BTW watanzania na hususani wajasiriamali walio wengi wamekuwa makini sana na taarifa za mitandaoni hivyo siyo mburura/ignorant kama mnavyowachukulia baadhi yenu. Utapeli wa biashara za china kwa wafanyabiashara hapo kariakoo umewafundisha wengi sana. Si rahisi mtu awe na zaidi ya 5M kwa Sasa ukamtapeli kirahisi. Waliotoa maoni kuhusu tahadhali za kuchukua kutokana na fursa iliyotolewa na Mshana Jr wamefanya vizuri tena kizalendo lakini hawapaswi kubeza idea yake. Watanzania tumekuwa tukitishana juu ya fursa ndo maana unakuta mtu ana kamtaji kake lakini kutokana na vitisho vya wengi anaambulia ama kughairi au kutochukua uamuzi na kutapanya mtaji wake. Tunachohitaji watu wawe wazalendo kwa nchi na watz wenzao, hata kama coordinator atapata chochote nae siyo mbaya ili mradi amewapa watu exposure nao wakapata pa kuanzia. Kwenda China siyo kama kwenda Kizimkazi, unahitaji watu wenye connection na exposure. Naomba tusimkatishe tamaa mleta idea na wale walionza kuhamasika japo tahadhari ni mhimu kwa Kila fursa.
 
Sasa Mshana Jr Mchina karibu atazindua kituo cha biashara hapo Ubungo ambacho kitakuwa kinatoa huduma za exhibition trading platform, cros-border E-commerce platform, commodity procurement platform kwa Made in China goods only

Hata huyo mfanyabiashara wa K/koo badala ya kwenda China anaweza kwenda Ubungo akajionea bidhaa anazopenda then akaenda kwa watu wa procure watakaokuwa na ofisi zao hapo hapo akafanya malipo akaagiza mzigo kutoka China. Ubungo itakuwa ni one stop wholesale center

Hii imekaaje?
 
Sina hakika kama bei ya mchina kukuagizia na kukuletea mzigo itakuwa cheap kiasi hicho au same as umenunulia china. Ikiwa kama unavyodhania basi flow ya watu kwenda China itapungua sana kibiashara na hii ni itakuwa na economic impact kwa both Tz na China. Ngoja tusubiri ikishafunguliwa but kwa mtazamo wangu pale watafacilitate mambo ya transport, logistics, shipping, marketing and procurement facilities.
 
Kama watafacilitate transport, logistics, shipping ipi itakuwa nafuu kufanya mfanyabishara mwenyewe au Mchina afacilitate?
 
Bora kama una mill 5 kushuka chini study vizuri alibaba kuna kila kitu mle na verified supplier...mambo ya Matapeli yapo lakini mimi sijawahi tapeliwa hata siku moja nina zaidi ya mwaka naagiza na vitu navoagiza vinafika salama kama nilivoagiza hata nikitaka niuze bei za kariakoo naweza uza...ukipata mtaji mkubwa kama 10 mill na zaidi nenda china...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…