Fursa ya safari ya kibiashara China (kwa wajasiriamali wenye mitaji midogo)

Fursa ya safari ya kibiashara China (kwa wajasiriamali wenye mitaji midogo)

Kutakuwa na safari ya kibiashara kwa wajasiriamali wenye mitaji kidogo nchini China mji wa YI WU mwezi wa tatu mwaka huu wa 2024 tarehe kumi hivi
Safari itakuwa ya pamoja kwa watu wasiopungua 10 na wasiozidi 20.. Faida ya safari hii ya pamoja
.Kupata barua ya mwaliko kwa bei nafuu
. Kupata tickets kwa bei nafuu
. Malazi ya pamoja ya bei nafuu uwapo huko
. Usafiri wa bei nafuu
. Ukalimani
. Mtandao wa maduka ya jumla makubwa na madogo
.Kupata connection mbalimbali za wafanyabiashara na wazalishaji wa China
. Gharama nafuu za chakula, vinywaji matembezi nknk
. Gharama nafuu na za uhakika za kusafirisha mizigo kurudi nchini..

Hii ni fursa mpya na wale watakaoweza kwenda ndio watafungua pazia kwa wengine huko mbeleni
Yale mambo ya kuagiza online ama kumuagiza mtu na kuishia kutapeliwa sasa yanafika mwisho.. Lakini vilevile kununua kitu kwa picha nayo yamafikia ukomo wake

Nitaweka mawasiliano rasmi kwa wale wote walio tayari.. Dirisha la waendaji litafungwa wiki ya pili ya mwezi February siku ya wapendanao

Nyongeza:
Kwa vijana wasio na mishe naweza kuwapa mizigo ya mali kauli kama wakitimiza vigezo na masharti

Sent using Jamii Forums mobile app
Ok
 
Wewe sasa ni wa sita

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimetoka kununua mzigo mkubwa kupisha chinese new year mzunguko mpaka mwezi wa 5.,...hizo document zote ninazo na nikisema niemde siendi kujaribu? Ni kununua tu.
Mi nitaenda mzunguko wa pili...may be kuamzia mwezi wa 5
Yaani ungepost mapema singenuunua mzigo mkubwa bile.
Hivi ni soko,la yiwu tu?.
Unasafirisha na cargo gani?
 
Barua ya mwaliko inalipiwa huu utapeli
Kwani kuna shida gani ikilipiwa?
Angalia:
1. Anayekualika si ndugu yako wala hana maslahi nawe ya moja kwa moja. Yeye atake risk bure ya kujifunga kuwa ndiye aliyekualika? Ujue yeye anakuwa kama mdhamini wako ukiwa huko China. Ukivurunda ukiwa huko inaweza kumsababishia shida

2. Vipi na rasilimali zake atakazotumia kama muda, n.k. kukuandikia hiyo barua?

Hata huku Tanzania, watu wanapotaka waandikiwe barua za utambulisho na wenyeviti wa vitongoji n.k, baadhi huwatoza hela ya "karatasi".

"Hakunaga" cha bure mkuu!
 
Na hii ni Platform ya biashara sio chama cha misaada au hisani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi mwenyewe mzee sana tu.
Majina yenu nayafahamu kitambo.

Id yangu ya miaka ya nyuma niliacha kuitumia kwa mwaka nikasahau neno la siri
UNGEWAOMBA MAMODS WAKUELEKEZE KUIFUNGUA HIYO PASSWORD YAKO ULIYOISAHAU
 
Back
Top Bottom