Fursa ya ufugaji wa ng'ombe wa asili kwa ajili ya nyama na maziwa kwa maeneo yaliyokaribu na soko

Fursa ya ufugaji wa ng'ombe wa asili kwa ajili ya nyama na maziwa kwa maeneo yaliyokaribu na soko

BARA BARA YA 5

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2009
Posts
1,174
Reaction score
835
Wajasilimali wenzangu msije mkasema sijawaambia,iko hivi kama una shamba karibu na Dar,maana ya Mkuranga, Bagamoyo nk fikiria mradi huu unalipa.Nimeiba idea hii kwa jirani yangu kupitia meneja wake nikaone ni FURSA muhimu.

Iko hivi kwa mfano:
Kama una eneo lako hata kama ni ekari moja tu ya shamba na uko eneo ambalo jirani zako wana shamba ambalo hawaliendelezi, basi unaweza kutumia fusra hii kubadili maisha yako.

Mchanganuo wa biashara hii ni kama ifauatvyo:

A: INVESTMENT COST
1. Nenda Mikoani nunua mitamba 80,000 kwa 250,000@ = = 20,000,000
2. Nunua madume 4 ya kisasa au Boran ambayo yataanza kupanda baada ya mwaka @ 300,000 = 1,200,000
3. Ujenzi wa Zizi na Nyumba ya mfanyakazi (Lumpsum) = 2,000,000
4. Mabomba ya kuogeshea 2 na Vifaa tiba @ (Lumpusm) = 200,000
JUMLA = 23,400,000
B: RUNNING COST

1. Mishahara ya wachungaji 2 Sh 200,000 X miezi 12 = 2,400,000
2. Walinzi 2 x 200,000 X Miezi 12 = 2,400,000
3. Madawa ya kuogesha na Tiba 50,000 X Miezi 12 = 600,000
4. Chakula wafanyakazi (Sembe +maharage) 100,000 Miezi 12 = 1,200,000
5. Supervisor 300,000 x miezi 12 = 3,600,000
6. Dharula 50,000 X miezi 12 = 600,000
JUMLA 10,800,000
JUMLA KUU A + B 34,200,000


BAADA YA MWAKA MMOJA

  • Ngombe 70 watatoa 140 litres X 1000/= Sawa na 140,000/day 4,200,000 /month sawa na Tsh 50,400,000/YR
  • Baada ya Miaka 3 utauza ng'ombe 50 X 700,000 35,000,000/YR

NOTE
Hii ina maana baada ya mwaka 1 unarejesha hela yako imerudi na faida ya kutosha. Hakikisha unampata meneja/Supervisor mzuri na umpe motisha ukifika hatua ya kutengeneza faida. Swala la ulinzi na afya ya mifugo lichukulie kwa umakini mkubwa sana. Ninae andika hii hoja ni mtoto wa mfugaji wa ng'ombe wa asili na sasa mfugaji wa ng'ombe wa kisasa..Uzoefu 100%

Hayo ni maoni yangu.

Karibuni kwa maoni.
 
Asante mkuu ni fursa nzuri sana mimi nimeanza tayari nipo mkoani huku
 
Wajasilimali wenzangu msije mkasema sijawaambia,iko hivi kama una shamba karibu na Dar,maana ya Mkuranga, Bagamoyo nk fikiria mradi huu unalipa.Nimeiba idea hii kwa jirani yangu kupitia meneja wake nikaone ni FURSA muhimu...
Hii idea yako mkuu uoni ikiwa ni ya ng'ombe wa kisasa itakua na faida zaidi
 
Asante mkuu ni fursa nzuri sana mimi nimeanza tayari nipo mkoani huku
Safi mkuu. Ila kwa mkoani naona changamoto inaweza kuwa soko la maziwa ambalo ndilo linasaidia kuendesha gharama baada ya mwaka mmoja. Hata hivyo kama unaweka marketing strategy nzuri bado kuna potentia nzuri sana.
 
Hii idea yako mkuu uoni ikiwa ni ya ng'ombe wa kisasa itakua na faida zaidi
Ng'ombe wa kisasa shida yake ni kwenye management..ili uone thamani yake lazima uweke chakula cha ziada kama pumba,mashudu.makiliki na mambo mengi,pia magonjwa na stress hasa za hali ya hela.

Ng'ombe wa asili wanakabiliana na changamoto zote nilizotaja hapo na faida yake bado inafanana kabisa na hao wa kisasa. Hata hivyo nimesema hawa asili weka madume ma 4 ya kisasa, maana yake baada ya muda kama wa miaka 3 utaanza kuwabadilisha na kuwapata chotara ambao wataongeza maziwa matra dufu.
 
Ng'mbe wengi
Ng'ombe wa kisasa shida yake ni kwenye management..ili uone thamani yake lazima uweke chakula cha ziada kama pumba,mashudu.makiliki na mambo mengi,pia magonjwa na stress hasa za hali ya hela. Ng'ombe wa asili wanakabiliana na changamoto zote nilizotaja hapo na faida yake bado inafanana kabisa na hao wa kisasa. Hata hivyo nimesema hawa asili weka madume ma 4 ya kisasa,maana yake baada ya muda kama wa miaka 3 utaanza kuwabadilisha na kuwapata chotara ambao wataongeza maziwa matra dufu.
Ni kwel ila tz kwa sasa ngombe wa kisasa wengi wavinasaba vya hao wa kienyeji hivo kwenye management aisumbui kuna watu wanafuga bila hata shida lakini concept yangu iko hivi imagine unang'mbe kumi wa kisasa wanatoa lita 10 kwa siku utapata lita 100 kwa siku lakini kwa ngombe wa kienyeji hpo utahitaji wastani wa ng'ombe 50 kupata hizo lita 100 hao ng'mbe hamsini utahitaji nguvu kazi kubwa, hivo utaongeza cost kweny kuajir wachungaji wengi, kujenga mabanda, hatari kukosa malisho ya kutosha hasa kipindi cha kiangazi, cost za chanjo na madawa pia hao ng'mbe wa kienyeji wanachelewa kufika maturity utatumia mda kupata faida stahiki.
 
Ng'mbe wengi Ni kwel ila tz kwa sasa ngombe wa kisasa wengi wavinasaba vya hao wa kienyeji hivo kwenye management aisumbui kuna watu wanafuga bila hata shida lakini concept yangu iko hivi imagine unang'mbe kumi wa kisasa wanatoa lita 10 kwa siku utapata lita 100 kwa siku lakini kwa ngombe wa kienyeji hpo utahitaji wastani wa ng'ombe 50 kupata hizo lita 100 hao ng'mbe hamsini utahitaji nguvu kazi kubwa ,hivo utaongeza cost kweny kuajir wachungaji wengi ,kujenga mabanda, hatari kukosa malisho ya kutosha hasa kipindi cha kiangazi, cost za chanjo na madawa pia hao ng'mbe wa kienyeji wanachelewa kufika maturity utatumia mda kupata faida stahiki.
Nakubaliana na wewe. Ila nitawabadilisha kwa kutumia dume la kisasa. Ila bado utakubaliana na mimi..ng,ombe wa kisasa ni kazi kuwahudumia.
 
Kuna jamo sijakuelewa mkuu, you mean ngombe 70 wanatoa 140 litres of milk per day, which means kila ngome ni 2 litres per day? Nchi jirani yetu ya kenya, ngombe wa kisasa anatoa upto 28-30 litres of milk per day, so so kaa nimekuelewa poa ya nini nijipe majukumu ya 70 cows, 140 ltrs a day? with nikiwa na ngombe 5 pekeee wa kisasa wananipa over or abaut 150 litres of milk kwa siku,je unaona tofauti ya operating cost ya 70 cows na only 5 cows ni kubwa muno? Nafikiri ni bora kuwa na ngombe wa kisasa wa maziwa, kama ni nyama unaweza deal na ngombe wa nyama pekee we na ile tunaita feedlots
 
Kuna jamo sijakuelewa mkuu, you mean ngombe 70 wanatoa 140 litres of milk per day, which means kila ngome ni 2 litres per day???????nchi jirani yetu ya kenya, ngombe wa kisasa anatoa upto 28-30 litres of milk per day, so so kaa nimekuelewa poa ya nini nijipe majukumu ya 70 cows, 140 ltrs a day? with nikiwa na ngombe 5 pekeee wa kisasa wananipa over or abaut 150 litres of milk kwa siku,je unaona tofauti ya operating cost ya 70 cows na only 5 cows ni kubwa muno?nafikiri ni bora kuwa na ngombe wa kisasa wa maziwa, kama ni nyama unaweza deal na ngombe wa nyama pekee we na ile tunaita feedlots
Natamani kujua Kenya wanatumia mbinu gani au ni utaalamu gani unatumika
 
Huko sahihi mkuu njia anayotaka kutumia jamaa kwenye mradi wake aiko valuable kabsa
Kuna jamo sijakuelewa mkuu, you mean ngombe 70 wanatoa 140 litres of milk per day, which means kila ngome ni 2 litres per day???????nchi jirani yetu ya kenya, ngombe wa kisasa anatoa upto 28-30 litres of milk per day, so so kaa nimekuelewa poa ya nini nijipe majukumu ya 70 cows, 140 ltrs a day? with nikiwa na ngombe 5 pekeee wa kisasa wananipa over or abaut 150 litres of milk kwa siku,je unaona tofauti ya operating cost ya 70 cows na only 5 cows ni kubwa muno?nafikiri ni bora kuwa na ngombe wa kisasa wa maziwa, kama ni nyama unaweza deal na ngombe wa nyama pekee we na ile tunaita feedlots
 
Karibuni kwa ujenzi bora wa mabanda ya bei rahisi
Pia kupatia project nzima kuhusu ufugaji kwa gharama nafuu na faida ya kutosha
Kwa waliotayari nitafute via +255620764565
 
Hii idea yako mkuu uoni ikiwa ni ya ng'ombe wa kisasa itakua na faida zaidi
Inesemekana ngo'mbe wa kisasa Wana chamgamoto Sana mkuu, ningependa kujua kwanini unasema ngo'mbe wa kisasa wangekuwa na Faida kuliko wa kienyeji?
 
Inesemekana ngo'mbe wa kisasa Wana chamgamoto Sana mkuu, ningependa kujua kwanini unasema ngo'mbe wa kisasa wangekuwa na Faida kuliko wa kienyeji?
Ng'mbe wa kisasa wanafaida kuliko wa kienyeji kwa sababu uzalishaji wao uko juu zaidi kwenye maziwa hata nyama
Ukuaji pia ni wa haraka wanamatured mapema
Bei zake pia zipo juu so ukiuza mfano ndama au mtamba unapata faida .

Changamoto sio sana kama unavosikia ukipata elimu ya management yao utafurahia ufugaji wako
 
Back
Top Bottom