Fursa za Kibiashara, Democratic Republic of the Congo

msumeno

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2009
Posts
2,826
Reaction score
1,734
Waungwana niko hapa DRC na leo nimeona ni vyema kushare fursa za kibiashara hapa.. Kwanza kabisa napenda kuwafahamisha kuwa kuwa Mtanzania hapa DRC hasa hapa Goma ni ujiko,, wacongo wanatupenda sana na wanadhani kuwa sisi ni watu waaminifu na wenye upendo na jasiri. kwa haraka haraka hizi ni bidhaa ambazo waweza uza bila kuwa na shaka

1. Khanga ,, akina mama wa ki congo wanapenda sana khanga ukileta utauza
2. Viatu vya kimasai... vyapendwa sana hapa... kwa wale wenye mitaji midogo hapa ni mahala pake
3. Nguo japo wameeanza kwenye China na Dubai , lakini bado wateja wa anguo jina la Tanzania linauza sana ( sijui kwa nini)
4. Mchele hakuna na kama upo si huu wa Tanzania wenye ladha.. na ukiupata bei haikamatiki wanakula akina fulani tu wengi wanjilia huu unaofanana na makande
5.maharagwe ya bukoba na kigoma utauza hapa
6. Alminium windows na door hakuna na ujenzi unaaza kwa kasi sana .. ukiwekeza utavuna pesa.. sijaona dirisha la alminum hapa.
7. Samaki na dagaa hasa wa mwanza -- waliwa sana hasa huko vijijini na Goma ndo soko kubwa

asante sana kwa leo n
 
Niliwahi kuku PM juu ya dhahabu per gram ikoje na upatikanaji wake ukoje? Haukuwahi kunijibu zaidi ulikaa kimya tu.
 
Na lugha inayotumika sana Goma ni ipi? Na hujaeleza njia rahisi kufika Goma ni ipi kama ni ile ya kupitia Ngara then Rwanda hadi gisenyi ndo uingie Goma au ile ya kupitia Burundi upande tex hadi Uvilla then uchukue boti hadi Goma ? Na terms za kufika hasa VISA ni shilingi ngapi? Na maisha yakoje exchange Rate kwa pesa ya Tanzania ikoje?
 
safi sana ungewaelea pia raia njia rahis na salama ya kufika uko

ndo suala nililomuuliza aeleze tu watu wachangamkie fursa Angalizo wale mnaopewa mchongo afu mnataka mtafuniwe kila kitu na mfikie kwa mtoa thread hua siwapendi na naomba ueleze pia lodge au hotel za Goma zinagharim kiasi gani?
 
Niliwahi Kupeleka TV kama mia hamsini hivi za mitumba basi jamaa waliiteka Boti na kula kichapo sana wakachukua zote na kuhamisha kwenye boti lao,nikabakia na Tv 20 tu ndio nikapata nauli ya kurudia.
Ni Kweli DRC biashara hizo na nyingine zinatoka sana,lakini usalama ndio tatizo.Utapeleka mara mbili basi ya tatu unaingizwa mtegoni
 
Jamani.......pole sana mpendwa wangu, kwa usalama wa nchi ni kila kitu kwa jamii nzima.
 
Tatizo huko ni hatari sana unaweza ukatekwa na msingi wote.
 
Niliwahi Kupeleka TV kama mia hamsini hivi za mitumba basi jamaa waliiteka Boti na kula kichapo sana wakachukua zote na kuhamisha kwenye boti lao,nikabakia na Tv 20 tu ndio nikapata nauli ya kurudia.
Ni Kweli DRC biashara hizo na nyingine zinatoka sana,lakini usalama ndio tatizo.Utapeleka mara mbili basi ya tatu unaingizwa mtegoni

Aisee!!!pole sana kweli kwenye biashara kuna changamoto nyingi sana watu tunakumbana nazo
 
Waungwana niko hapa DRC na leo nimeona ni vyema kushare fursa za kibiashara hapa.. Kwanza kabisa napenda kuwafahamisha kuwa kuwa Mtanzania hapa DRC hasa hapa Goma ni ujiko,, wacongo wanatupenda sana na wanadhani kuwa sisi ni watu waaminifu na wenye upendo na jasiri. kwa haraka haraka hizi ni bidhaa ambazo waweza uza bila kuwa na shaka

1. Khanga ,, akina mama wa ki congo wanapenda sana khanga ukileta utauza
2. Viatu vya kimasai... vyapendwa sana hapa... kwa wale wenye mitaji midogo hapa ni mahala pake
3. Nguo japo wameeanza kwenye China na Dubai , lakini bado wateja wa anguo jina la Tanzania linauza sana ( sijui kwa nini)
4. Mchele hakuna na kama upo si huu wa Tanzania wenye ladha.. na ukiupata bei haikamatiki wanakula akina fulani tu wengi wanjilia huu unaofanana na makande
5.maharagwe ya bukoba na kigoma utauza hapa
6. Alminium windows na door hakuna na ujenzi unaaza kwa kasi sana .. ukiwekeza utavuna pesa.. sijaona dirisha la alminum hapa.
7. Samaki na dagaa hasa wa mwanza -- waliwa sana hasa huko vijijini na Goma ndo soko kubwa

asante sana kwa leo n

Jaribu Na Muziki...........................!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Acheni woga waTZ mbona mimi niko hapa?? sizungumzii toka hewani ni hapa GOMA... hali tete iko vijijini lakini sio mijini .. kwa sasa hata huko vijiji si kivile maana vijana wa JK wamefanya kazi hapa
 
Jaribu Na Muziki...........................!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Muziki kivipi?? mimi hapa nina kazi yangu nimeajiriwa hapa na INGO moja inanilipa vizuri namshukuru Mola wangu ... si kosa ku share fursa na kama wewe unaona ni upuuzi basi sawa na hauna haja ya kunikejeli mimi nimetimiza wajibu wangu wa kwa tanzania wenzangu
 
ndo suala nililomuuliza aeleze tu watu wachangamkie fursa Angalizo wale mnaopewa mchongo afu mnataka mtafuniwe kila kitu na mfikie kwa mtoa thread hua siwapendi na naomba ueleze pia lodge au hotel za Goma zinagharim kiasi gani?

hotel ya kawaida ni 20 usd kwa night.. zipo mpaka za 15 usd ila zinakuwa kulee ''manzese'' so usalama ni shida .. ukiwa na mtaji zipo mpaka za 50 usd.. chakula kwa mama ntilie ni dola 5 wali nyama na kisamvu na maji ndogo.. kuhusu kufika kwangu haiwezekani mimi ni expat hapa ni shirika limeniajiri na kunipa house lakini shared so siwezi invite mtu .. hizi si family missions.. kwa hapa DRC Kinshasa peke yake ndo familiy mission,, kwa Goma hapana
 
safi sana ungewaelea pia raia njia rahis na salama ya kufika uko

DRC ni kubwa nitakuelezea kuhusu GOMA na BENI na BUTEMBO maana ndo maeneo niliyopo... kwa Goma unapitia kwa Mjomba Kagame pale Rwanda kigali then unapanda bus au taxi mpaka Mkoa wa Gisenyi, Gisenyi na Goma nikama zimeungana tu ni kama Esebania na Sirari sijui nauli kwa bus toka dar mpaka Kigali lakini kwa ndege ni chini ya dola 400 return ticket na dola 7 kwa bus mpaka gisenyi na 90 kwa taxi
 
Na lugha inayotumika sana Goma ni ipi? Na hujaeleza njia rahisi kufika Goma ni ipi kama ni ile ya kupitia Ngara then Rwanda hadi gisenyi ndo uingie Goma au ile ya kupitia Burundi upande tex hadi Uvilla then uchukue boti hadi Goma ? Na terms za kufika hasa VISA ni shilingi ngapi? Na maisha yakoje exchange Rate kwa pesa ya Tanzania ikoje?

visa chukua dar 60 usd... lugha kiswahili na french
 
Niliwahi kuku PM juu ya dhahabu per gram ikoje na upatikanaji wake ukoje? Haukuwahi kunijibu zaidi ulikaa kimya tu.

Dhahabu sikushauri ... ziko sana hasa kwa waasi ilawanakuuzia then wanawatonya washikaji wanakuja kuzichukua baadae.. na ujue pia kwa rwanda ukikamatwa 20 years jela unless upitia serekarini ambako sina ujuzi nako.. wapigaji wanatoka lakini ni risk sana.. si dhahabu hata alimasi na mawe menigine GOMA ndo kwao...
 
haukunielewa hakuna aliyesema afikie kwako ndugu, Kenya Airways walikua na route ya Nairobi To Goma hvo nadhani kama umenunua mzigo unawezapitia Nairobi then ukaanza safari nyingine btw asante kwa maelezo yako.
 
Wewe ndo hukunielewa,,, biashara ya dhahabu ipo na wanaoifanya lazima wawe wazoefu maana huko WALIKALE na maeneo mengine ni mbali sana toka hapa Goma na wengine huchukulia hapa kwa watoto wa mujini waliotoa kule bush.. shida tu ni kamba wanaokuuzia ndo hao hao wanaokuja kuichukua baadae labda uwe mzoefu na unafanya na watoto wa mujini wa hapa na mnaaminiana sana.. kuna jamaa alipigwa dolla 25000 (kama kweli) yuko hapa sasa hhana kitu tena... kuhusu kufikia kwangu nime combine majibu sikuwa na kulenga wewe... ila nimeeleza ninavyoishi hapa .... interest yangu si ya kimaslahi ila ni ku share tu nijuacho na ninaweza kuwa wrong pia... Kenya Airways haiko hapa hapa ndege tunapandia Rwanda... ila local flights zipo kibao lakini ni dani tu... kutoka hapa mpaka kigali ni kama masaa 3 hivi kwa gari na toka kigali kuna option kama mbili Kenya Airways and Rwandair
 
Back
Top Bottom