Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
1. Wahitaji export license/Certificate ya Tanzania na hiyo utaipata kutoka wizara ya viwanda na biashara.Mkuu, Vibali gani inahitajika kuwa na vyo ili uweze ku export bidhaa nje?
Kwenye suala kama la viny'ago nafikiri wizara ya maliasili pia yahusika kwa issue ya bidhaa zitokanazo na miti.
Pia wahitaji import licence kule unakopeleka bidhaa na kufuata sheria zao kama vile
1. Sheria ya kuingiza bidhaa za kutoka nje ya Ulaya
2. Kuna namba maalum importer hupewa yaitwa EORI yaani Economic Operator Registration Identification Number ni lazima uwe nayo.
3. Biashara yako iwe imesajiliwa na ni jambo la uzuri kuwa na mshirika wa biashara wako alie ndani ya nchi ufanyayo import.
Hii inasaidia kwenye kulipa tax na mambo mengine kama ofisi na kadhalika.
Unaweza kuwatafuta watu waingizao bidhaa Ulaya kama bwana mmoja maarufu aitwa Dewji nafikiri bado afanya hizi biashara za import.
4. ufahamu kila bidhaa ina Code au namba maalum kwa ajili ya tax.
5. Uwe makini na labelling, marking na sheria zote za masoko.
6. ufahamu namna ya kutoa mizigo kutoka customs au utumie kampuni mwenyeji.
Na mwisho, ufahamu namna ya kuweka invoices na rekodi zote za biashara yako.
Mkuu, fika ofisi za Dar-es-Salaam Chambers of Commerce kwa elimu zaidi au TanTrade watakusaidia kukupa mwanga zaidi.
Mimi nimekupatia dondoo kiasi, ila watakiwa kujiandaa khaswa.