Wakuu, njia ingine nzuri zaidi ya kutoka nje na kujitayarisha kuwa mfanyabiashara wa bidhaa.
Ila lazima uwe mfanyabiashara smart unaelewa biashara na masoko, sheria mbalimbali na viwango vya nchi husika na kadhalika.
Bidhaa nyingi Ulaya sasa hivi zimekuwa haba kutokana na masuala kama ugonjwa wa UVIKo-19 ambao umesababisha biashara nyingi ndogo kufa.
Kwa mfano waweza kuamua kuwa wasafirisha nje, bidhaa ambazo ni "hot cake" katika maduka ya huko kama maparachichi, na sasa hivi kama kule UK wanahitaji sana Viazi kwa ajili ya chips.
Suala ambalo wazungu siku zote wanataka ni viwango, kuanzia kuvuna hadi kupakia bidhaa kwa viwango vinavyoridhisha.
Kwa mfano ukipaki parachichi wengine wataki upaki nne katika kifurushi na uweke alama zote muhimu kwenye kifurushi chako.
Maparachichi yanahitajika sana lakini ukumbuke washindana na wazalishaji wa nchi zingine hivyo uwe smart.
Bidhaa kama Viazi ni haba kwa sasa khasa Uingereza ambapo jamaa zangu waliko pale wasema viazi vimeadimika.
Hivyo ukiwa Tanzania watakiwa kuwa na storage, na packaging yako iwe katika viwango na uweze kuwa wahifadhi viazi vya kuweka kwenye ubaridi frozen chips ambapo vyaweza kuingia moja kwa moja kwenye kikaangio.
Hizi biashara zipo maana wahindi, wachina na raia kutoka nchi zingine za Afrika kama Ghana na Nigeria hupeleka kule bidhaa kama mihogo, mchicha na mbogamboga zingine.
Ila kama ambavyo nimekuwa nikisema humu siku zote, hizi shughuli zatakiwa kuanzia kwanza nyumbani Tanzania kisha wajijenga na kuanza kusafirisha bidhaa hizo ndani ya nchi kisha waweka "base" ya wateja na baadae kuendelea nje ya nchi.
Lakini masuala kama kuvuna, kupakia, kufanya "labelling", kuwashirikisha shirika la viwango, na mamlaka zingine ni jambo la muhimu kabla hujasafirisha bidhaa nje.
Ila kwa sasa suala la ugonjwa wa UVIKO-19 limewapa sababu nchi nyingi za Ulaya na Marekani kutumia nafasi hiyo kuzinyanyasa nchi maskini nyingi zikiwa za Afrika kwa kuziweka katika orodha jhyekundu au RED LIST.
Hiyo yaleta taabu kwa kiasi kikubwa kwani ni wale wenye fedha na matajiri ndo watoweza kujitenga mahotelini kwa gharama za kwao.