Fuvu na Mifupa(Skull and Bones) Jamii ya Siri ya Kishetani inayoongoza Matukio ya Duniani

Kwenye UKIMWI Eiyer amenimaliza. Ni kweli Hakuna kitu kinachoitwa UKIMWI? TB inaenezwa kwa sexual intercourse? TB inaenezwa toka kwa mama kwenda kwa mtoto?
Hukusoma ukaelewa nilichoandika...

Nilisema kwamba watu waliwapachika watu waliokuwa wanaugua kwa series [mfuatano] maradhi ya kufanana kuwa walikuwa wana maradhi waliyoambukizana kwa ngono au damu.Walisema kwamba mtu aliyekuwa na ugonjwa huo na ukamhudumia bila kuwa mwangalifu anaweza kukuambukiza kama utakuwa na kidonda mkononi au ukapata kijijeraha kidogo mkononi na yeye akiwa na jeraha...

Watu hao walikuwa wakifariki kwa kuharisha,kukonda sana,kunyonyoka nywele na kuota madonda kwenye ngozi zao.Kama alianza kufa mume mke alifuata na pengine hata mtoto mchanga waliyekuwa naye au hata family member aliyekuwa akiwahudumia wakati walipokuwa wanaugua maradhi hayo...

Kitu watu walishindwa kujua ni kwamba,kwanza hizo dalili zilizotajwa nyingi ni za TB na wakati ule hakukuwa na elimu nzuri kuhusu maradhi hayo hivyo watu hawakuchukulia tahadhari wanapokuwa wanawahudumia wagonjwa wa maradhi hayo na wao waliambukizwa pia....

Ukiangalia mke na mume wanalala kitanda kimoja pamoja na mtoto wao mchanga.Wanajifunika shuka moja.Wakati wa kujamiiana wananyonyana ulimi na mengine meengi tu.Kama mwanandoa mmoja atakuwa na TB ni LAZIMA atamuambukiza mwingine hivyo ataugua aliyeanza kuwa nayo kisha atafuata mwingine naye ataugua kwa mtindo ule ule tu na mtoto wao naye watamuambukiza kwasababu TB huambukiwa kwa hewa pia....

Yule aliyekuwa anamhudumia mgonjwa naye atakuwa katika wakati mzuri zaidi wa kuambukizwa kwasababu hata kufua nguo za mjonjwa tu kunatosha kukufanya nawe uipate TB na kutokana na kutokuwa na elimu ya maradhi hayo kipindi kile hawa watu waliowahudumia wagonjwa hao walikuwa wakiambukizwa sana maradhi hayo na wao kufa baadaye...

Sasa basi,kwasababu hii watu waliamini kabisa kuwa kuna ugonjwa mpya uliokuwa unaambukizwa kwa ngono lakini haikuwa kweli kwasababu nilizozisema hapo juu.Kwa maana hiyo ni kwamba TB haiambukizwi kwa ngono bali hewa na mambo mengine mengi ambayo wanandoa au wapenzi wanashea kila siku...
 
Mkuu Eiyer,mimi binafsi swali langu ni kwamba kabla ya ujio wa wakoloni Afrika (1700s) hakukuwa na nyaraka zenye kuonyesha ukaribu kati ya Mwafrika na Mungu. Tunaona historia ya Mwafrika inaanza baada ya ujio wa mkoloni,imani ya mwafrika haikushabihiana na maandiko katika biblia bali kinyume chake. je,inawezekanaje utamaduni wa Mwafrika (wa kiimani) ukahamia bara Ulaya kwa asilimia 100% bila kuacha alama yoyote?
 
Reactions: ADK
Kosa kubwa tunal;olifanya Waafrika ni kufuata historia iliyoandikwa na wakoloni.Wakoloni wanataka tujione na tuonekane washenzi kabisa mbele ya macho yetu na dunia kwa ujumla wake.Wakoloni kama wa Afrika ya kusini walisema kwamba wakati wanafika Johanesbourg miaka 500 iliyopita wanasema walikuta ndege tu waliokuwa na viota vyao maeneo hayo.Wanataka kutufanya kuwa wao ndiyo walioleta "ustaarabu huku kwetu" kitu ambacho siyo kweli kabisa.....

Hivi hatujiulizi kwamba,mtu mweusi alikuwepo kabla ya ujio wa Wakoloni,kwanini historia yetu inaanzia kwenye ujio wa wakoloni na siyo kabla ya hapo?

Kwa mfano katika kitabu cha matendo ya mitume kuna mtu mmoja alitokea huku Afrika aliyekuwa na kitabu cha Isaya akielekea Jerusalem kuabudu,hiyo ilikuwa ni karne ya kwanza na mapema kabisa kwenye 68 A.D.Ni wakoloni walimpa kitabu cha Isaya huyu mtu?

Hatusikii kuhusu jeshi imara kabisa la Afrika lililotaka kuuangusha utawala wa Roma.Hatusikii kuhusu vyuo walivyovikuita huku AFRIKA wakati wanakuja na kutufanya koloni lao,Hawasemi kuwa walipokuja huku walitukuta tumestaarabika kuliko wao,hawasemi ni kwanini walivunja sanamu za wafuasi wa Yesu zilizojengwa na wanafunzi wa wanafunzi wa Yesu waliokuja huku AFrika na kuna wengine walifia huku....

Luka alikuja hadi Libya wakati huo ikiwa na watu weusi kabisa.Waarabu wakati wanakuja huku walikuta Ukristo upo zamani hata kabla ya ujio wa wakoloni lakini tunaamini wakoloni ndiyo wamekuja kutuletea "akili",inasikitisha sana....

Mkuu huwezi kutegemea adui yako akutengenezee kitu bora kwaajili yako,atakutengenezea kinachomtukuza yeye tu.Sisi Waafrika hatujui tu lakini hakuna anayetupenda hapa duniani kwasababu sisi ndiyo binadamu bora na tuliokamilika kuliko wengine wote....

Siku tukiujua ukweli huu tutarudia enzi zetu ambazo tuliitawala dunia,nadhani hili hulijui lakini tulishaitawala dunia miaka mingi tu.Mfano wa kuliona hili ni Misri,hii ilikuwa ni falme na super power ya watu weusi kabisa na ni mamlaka iliyodumu miaka mingi sana tena miaka ya 3000 B.C huko lakini bado tunajidharau tu na kuamini tulielimishwa na wakoloni....

Mkuu tujisomee sana ili tujiokoe kwenye huu upuuzi wa kuamini kuwa wakoloni ndiyo waliokuja kutuelimisha...
 
mkuu shukrani kwa kunifungua akili,basi la msingi naomba unitumie link zenye source ya historia chanya ya mwafrika kama ukipata muda tafadhali,nimeamua kuijua kweli kuanzia leo.
 
Mkuu Eiyer bado kuna kitu hujaniweka wazi japokuwa napata logic yako kwa mbali sana, je Hakuna ugonjwa wa UKIMWI ambao huambukizwa kwa kujamiiana, kuongezewa damu yenye maambukizi, kuchangia vitu vyenye ncha kali na mtu mwenye maambukizi nk?
Unataka kusema TB ndio iliboreshwa ki science ikawa UKIMWI? Ni kweli kuwa tunaambiwa mara Nyingi mwenye TB hachezi mbali na VVU , UKIMWI ndio TB? Ikiwa kwa sasa TB inatibika kwa nini UKIMWI hautibiki? Bado sijapata logic yako ya kukataa uwepo wa UKIMWI. Tafadhali naomba shule!!! Huko kwingine tunaenda sawa. Sina nia ya kuichepusha mada.
 
Reactions: ADK
Shukrani mkuu Eiyer mwanafunzi wako mtiifu niko hapa nakufuatilia vzr na kwa ukaribu tu,hapo ktk Africa niliwahi kusoma Dola ya Mlina( km cjakosea) huko kilwa ilikua inajulikana ENZI hizo hadi Rumi huko
 
Shukrani mkuu Eiyer mwanafunzi wako mtiifu niko hapa nakufuatilia vzr na kwa ukaribu tu,hapo ktk Africa niliwahi kusoma Dola ya Mlina( km cjakosea) huko kilwa ilikua inajulikana ENZI hizo hadi Rumi huko
Dolaza Kiafrika ambazo ziliwahi kuwa na nguvu kubwa sana duniani zilikuwa nyingi tu...

Lakini cha kushangaza sana tena sana ni kwamba ukifuatilia waliyoyafanya mashujaa weusi utakuta wamewaweka weupe.Mfano ni kiongozi na General wa Carthage aliyeitwa Hannibal,huyu jamaa alikuwa mweusi na alitawala kuanzia mwaka 247 hadi 183 B.C na huyu ndiye aliyetaka kuangusha utawala wa Rome.Lakini uki google hilo jina utaletewa picha za mzungu,hovuo sana hawa watu kwakweli....

Mkuu tuendelee kujisomea kutoka kwenye vyanzo huru tutajua mengi kutuhusu sisi ambao ni binadamu bora kabisa hapa duniani....
 
Ukimwi kwa maana ya upungufu wa kinga ya mwili upo lakini unatibika.UKIMWI kama kinga ya mwili kushuka inasababishwa na life style na siyo kitu kingine na unapokuwa na tatizo hilo unaugua maradhi mbali mbali na ukiyatibu na kubadilisha mtindo wa maisha unakuwa huna shida yoyote....

Hakuna upungufu kinga unaoambukizwa kwa ngono.Hakuna kirusi chochote kinahosababisdha upungufu wa kinga ya mwili kwasababu hadi sasa hakuna ushahidi wowote ule wa uwepo wa ikirusi huyo.HIV kwa upande wa pili ni kirusi hewa,hakijawahi kuonekana kwenye damu ya mgonjwa wala mahala popote duniani.Wanadai kuwa kirusi hicho ni jamii ya Retrovirus,kama ni hivyo hao retrovirus walikuwepo tangu enzi na enzi na hawakusababisha kinga ya mwili kushuka,huyu amekuwaje hadi asababishe? Kama wanasema kuna kirusi hicho specific,ushahidi wa uwepo wake uko wapi?

Watu wanaugua na wanakufa kwa mtindo fulani,hili lipo,wao wameamua kusema ni sababu wana HIV kwenye damu zao,kwanini hawataki kutuonesha hata picha ya huyo HIV? Watu wanougua wanaugua maradhi mengi sana na tofauti tofauti.TB ilikuwepo na itaendelea kuwepo na haijaboreshwa na kuitwa HIV bali huko nyuma ilisingiziwa hivyo,yaani mtu aliyekuwa na TB alisemwa kuwa ana UKIMWI ule wa kusababishwa na kirusi.Kitu ambacho ni uongo mkubwa....

Kwanza nakubali kuwa mtu akifikia hatua ya kupata TB anakuwa na UKIMWI,lakini huo ukimwi hajaambukizwa kwa ngono au damu bali kaupata kutokana na mtindo wake wa maisha tu na huyu anaweza kutibiwa akapona kabisa.Hao wataalam wa afya wanajua kuwa huwezi kupata TB kama kinga yako haijashuka na kuna ambao wamewapima wakawa HIV- na bado wana TB....

Kinachowaua watu leo ni ARVs.hizi dawa zinasababisha ini kufeli,figo kufeli,kansa,upungufu wa damu,kuota madonda kwenye ngozi n.k.Kimsingi yapo maradhi mengi sana ambayo wanaugua wale wanaotumia ARVs lakini wale wasiotumia hayo madawa hawaugui.....

Walichokifanya ni kwamba wametengeneza dhana ya kuwepo ugonjwa hewa kisha wakawatisha watu kuwa unaua kikatili kisha wakaleta dawa ambazo kimsingi ndizo zinazosababisha matatizo makubwa waliyoambiwa na pengine zaidi ya hayo...

Tatizo siyo UKIMWI bali ARVs ambazo zinasababisha UKIMWI usiotibika...

Ukiwauliza ni kwa vipi HIV anasababisha kansa hawawezi kukueleza lakini hapo hapo wanaotumia ARVs wanaugua kansa,sasa sijui wameipata wapi...

Yaani haya mambo ni shida tu.Watu wanaangamaia kwa kukosa maarifa....
 

Una mzungumzia uyu?Naomba Source zako na mimi nikajionee kama alikuwa Ni Black kweli..Ninachokijua ni kwamba wazazi wake walikuwa na Hasiri ya arabs,Walio ishi Northern Africa kwa Muda mrefu.
 
Kwa hili naweza kukuvaliana na wewe mkuu, siku zote siamini kama kuna kitu kinaitwa UKIMWI
 
Mkuuu nimefuatilia thread zote Na nimeingiza vitu kichwani nilivyokuwa sivifahamu pia naomba unieleweshe kuhusu mnara wa Babel zumuni lake inasemekana ndo chanzo cha luga zilipoanzia je ni kweli Na kama ni hivyo vipi kuhusu hilo ulilosema kuwa walijenga kwa ajili ya kuhofia mafuliko kujitokeza hebu niweke wazi mkuuu
 
Sasa hapo kuna hoja? Tuekee ushahidi wa hicho unakiandika hapa, nani alienda kwenye hiyo miji na kupanda hizo treni, hakuna na haitakaavitokee hiyo technology unayoizungumza mpaka dunia itaisha hii
. Vipo vitu vya kujengewa hoja sio hizi porojo unazowapumbaza watu hapa
 
Nimekuelewa
 
Mkuu kwenye post uliyosoma kuhusu mafuriko mbona nimeandika dhumuni la mnara wa Babeli?

Soma tena utaona majibu yake mkuu...
Pia ukimaliza hilo naomba unijuze monalisa alikuwa ni nani aliyezungumziwa Na huyu da Vinci code
Ishu ya Monalisa ni mada nyingine mkuu,tutalijadili wakati mwingine kwenye mada husika...

Tuombe uzima mkuu.....
 
Nilitaka tu nidhibitishe namna yako ya kufikiri na nimeshajua...

Haya mkuu kila lakheri...
 
Mkuu jaribu kuanzisha uzi. Japo uelezee kwa ufupi.
Nimegundua kuna mengi tunaweza kujifunza kutoka kwako
 
Mkuu Eiyer nakushukuru kwa elimu murua, naendelea kupata darasa mubashara.
 
Mkuu jaribu kuanzisha uzi. Japo uelezee kwa ufupi.
Nimegundua kuna mengi tunaweza kujifunza kutoka kwako
Mkuu,ni kweli lakini nashindwa hata niandike kitu gani maana ni mengi sana.Nitajitahidi kufikiria cha kuandika siku moja mkuu ambacho kitakuwa na nyama za kutosha ili msomaji aweze kusoma na kuelewa mkuu....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…