Nitajitahidi kufupisha kwa namna nitakavyoweza ili nisiandike maandishi mengi japokuwa siyo jambo zuri maana kuna mengine hutayajua...
Bara la Atlantis ni bara lililokuwa kwenye bahari ya atlantic baina ya bara ulaya na Amrerica ya kaskazini.Bara hili lilijulikana kama kitovu cha maendeleo duniani na wakati huo dunia ilikuwa na maendeleo makubwa mara kumi ya sasa.Jambo hili linafichwa sana kwa sababu maalum.Bara hili waliishi magiant [Nephilims] ambao waliendesha utawala duniani utawala ambao ulimuumiza sana binadamu wa kawaida.Kulikuwa kukifanyika kafara za binadamu na viungo vya binadamu vilikuwa vikitumika kwa shughuli mbali mbali za nguvu za giza.Ilifikia mahali damu ya binadamu ilikuwa ikitumika kama kinywaji cha kawaida kwa hawa viumbe..
Unaweza kujiuliza hawa Nephilim ni nani au akina nani.Nephilims ni viumbe ambao walikuwa nusu binadamu na nusu malaika ambao walipatikana baada ya malaika waasi kufanya ngono na wanawake wanadamu.Malaika waasi ndiyo waliowafundishwa wanadamu elimu za unajimu,utoaji wa mimba,kutengeneza silaha na teknolojia nyinginezo ambazo ni za hali ya juu sana.Binadamu baana ya kupata ujuzi huu walianza kuuana wao kwa wao na ndipo Mungu alipoingilia kati na kuleta gharika lililowasambaratisha viumbe wote na kuwasalimisha walioingia kwenye safina...
Maisha ya wakati huu yalikuwa ya kishetani haswa.ni maisha ya kutisha sana maana binadamu alikuwa akiishi kama vile mbuzi leo maana alikuwa akiwindwa vilivyo hadi pale ambapo Mungu alipoamua kuingilia kati.Anayetaka kulirudisha bara hili na ustaarabu ule ni Semjaza,miongoni mwa malaika wakuu walioasi wanataka kuuleta ufalme wao hapa duniani wakishirikiana na binadamu wachache wasiojua ukweli na wanaoujua wachache sana lakini kwa umakini na udanganyifu mkubwa sana wa kisayansi....
Wanataka watawale dunia na jambo hili litatokea siyo miaka mingi kutokea sasa maana wanamalizia tu na wanataka kuwaleta tena hao malaika kutoka walipo kupitia kinachoendelea kule kwenye mitambo yao ya LHC [Large Hadron Collider] kwenye project yao maarufu ya Cern ambapo wanataka kufanya kitu ambacho dunia haitakuja kusahau kamwe...
View attachment 503610 View attachment 503611
LHC
Sananda ni kiumbe wa roho ambaye anajifananisha na Yesu,picha inayotumika kwenye makanisa na ambayo watu wanaamini kuwa ni ya Yesu ni ya Sananda,kuna mengi kumhusu huyu lakini kwa hapa inatosha kusema hivyo.Watu wanadai ni picha ya Cecare Borgia lakini ukweli ni kwamba ni picha ya Sananda.Kiumbe huyu ni miongoni mwa wale malaika waasi na huyu atatumika kudanganya watu wakati watakapo fake ujio wa Yesu.....
View attachment 503607 View attachment 503608 View attachment 503609 View attachment 503609
Sananda...
Sanat Kumara ni Azazel ambaye hujulikana kama Satan Kumara maana jina lake la kwanza limebadilishwa tu herufi.Huyu inasemekana ni Shetani mwenyewe au ni second in command kwenye himaya yao hawa malaika waasi....
Nadhani nimekupa mwanga angalau kidogo....