Jesusie
JF-Expert Member
- Aug 29, 2021
- 1,466
- 766
Kwamiezi michache tu ya awamu ya sita Rais Samia ameongeza Jumla ya wanafunzi wanufaika wapya 29,117 wa HESLB,Mtakumbuka miaka mitano ya awamu ya tano tuliongeza wanafunzi wapya 32,583,God's Good
===Mpaka awamu ya nne inaondoka madarakani FY2015|16 kulikuwa na Jumla ya wanafunzi 98'300 walionufaika na mikopo ya elimu ya juu ( HESLB ),
Lakini pia mpaka mwishoni mwamuhula wa kwanza wa awamu ya tano FY2020|21 wanafunzi wanufaika wa HESLB walifikia 130'883 sawa na ongezeko la wanafunzi wapya 32,583,
Ongezeko hili ni kwa miaka yote mitano mfululizo ya awamu ya tano,
Maajabu ni hii miezi michache ya Rais Samia Suluhu idadi ya wanufaika wa HESLB imefikia 160,000,
Idadi hii mpya ya wanafunzi ni sawa na ongezeko la wanafunzi wapya 29,177 hii ni kwa miezi hii michache ya Mama Samia ,Hakika Mama anastahili maombi ya nguvu sana,
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ilitangaza orodha ya Awamu ya Kwanza yenye wanafunzi 37,731 wa mwaka wa kwanza,
Idadi hii ya kwanza ya wanafunzi iligharimu thamani ya mikopo yenye thamani ya TZS 99.9 bilioni kwa mwaka wa masomo 2021|2022,
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru alitaarifu kuwa kati ya wanafunzi hao (37,731), wanaume ni 23,379 sawa na 62% na wanawake ni 14,352 sawa na 38%.
Badru aliongeza kuwa HESLB ilianza kupeleka fedha za wanafunzi waliopangiwa mikopo katika vyuo mbalimbali nchi kwa wakati,
“Orodha hiyo ya kwanza ilijumuisha wanafunzi wenye sifa zikiwemo kuwa wahitaji, wameomba kwa usahihi na wana udahili wa chuo kimoja,"
Badru alisema " tulikamilisha uchambuzi wa maombi mengine na tulitoa orodha ya pili ndani ya siku mbili"
TZS 570 Bilioni zilitengwa kwa mikopo ya elimu ya juu FY2021|2022 Kutoka 450BL za FY2020|21 au 348.7BL za mwaka 2015|16,
Hii ni sawa na kusema Rais Samia kwa muda mfupi ameongeza TZS 120BL wakati awamu iliyopita kwa miaka mitano iliongeza TZS 101.3BL tu kwa miaka mitano,
Kwa mujibu wa Badru, Serikali ilitenga TZS 570 bilioni kwa ajili ya mikopo ya jumla ya wanafunzi 160,000.
Aidha, Kati yao wanafunzi 70,000 watakuwa ni wanufaika wapya na wanafunzi zaidi ya 90,000 ni wale wanaoendelea na masomo baada ya kufaulu mitihani yao ya mwaka.
Wakati huohuo, Badru alisema HESLB ilipokea fedha kwa wakati kwa ajili ya malipo ya wanafunzi na taratibu za malipo zilianza haraka ili fedha hizo ziwafikie wanafunzi vyuoni kwa wakati,