FY2021/22 Serikali kutoa Trilioni 11 kulipa madeni ya nyuma

FY2021/22 Serikali kutoa Trilioni 11 kulipa madeni ya nyuma

CM 1774858

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2021
Posts
5,621
Reaction score
5,029

||FY2021|22 Rais Samia kutoa Jumla ya Trilioni 11 kulipa madeni ya nyuma yaliyoaachwa na mtangulizi wale,​

===

Rais Samia Suluhu Hassan kimyakimya ameendelea kulipa madeni mbalimbali kwa makampuni binafsi au taasisi.

Kwakuanzia tu mwaka huu pekee Rais Samia analipa madeni yenye thamani ya Jumla ya zaidi ya TZS11.17623Trilioni.

Watanzania mnapoambiwa Rais Samia ni levels zingine muelewe pamoja na kulipa madeni yote haya miradi yote ya maendeleo Mipya na yazamani inaendelea kwa speed, Pitia hii listi ya malipo

1 . Mama ametoa Jumla ya fedha kiasi cha TZS 111.41BL ili kuwalipa watumishi wa Serikali wanaoidai Serikali,

Tunafahamu malipo haya yataongeza ari na nguvu zaidi kwa watumishi hawa wa Serikali kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kuwatumikia Watanzania ambao ndio waajiri wao, Je! hili si jambo jema?

2. Mama ametoa Jumla ya fedha kiasi cha TZS 264.23BL kwaajili ya kuwalipa wakandarasi wetu mbalimbali wa nje na ndani waliokuwa wanaidai Serikali.

Hii itaongeza imani na uaminifu kwao katika kuendelea kutoa huduma kwa Serikali yetu ya JMT, Je! hili si jambo jema?

3. Mama ametoa Jumla ya fedha kiasi cha TZS 70.49BL kwaajili ya kuwalipa Wazabuni wetu mbalimbali waliotoa bidhaa na huduma kwa Serikali yetu.

Sote ni mashahidi Wazabuni wengi walikuwa wakilalamika kudaiwa mikopo benki naamini wamefuraha sasa na Wataendelea kutekeleza ilani ya CCM ya 2020-2025 bila kinyongo, Je! hili si jambo jema?

4. Mama ametoa Jumla ya fedha kiasi cha TZS 2.17BL ili kuwalipa watoa huduma mbalimbali waliokuwa wanaidai Serikali kutoka katika Wizara mbalimbali.

Hakika mama huyu anajicho la pekee kama hujaelewa unakwenda wapi na Rais Samia basi ni wazi wewe hujui unakotaka kwenda-Je! hili si jambo jema?

5. Mama ametoa Jumla ya fedha kiasi cha TZS 67.93BL kwaajili ya hukumu na fidia mbalimbali ambazo Serikali inadaiwa baada ya kushindwa kesi mbalimbali ili kutengeneza imani kwa wawekezaji wa ndani na nje pamoja na watu binafsi,Je! hili si jambo jema?

6. Mama ametoa Jumla ya fedha kiasi cha TZS 10.66Trilioni ili kulipia deni la Serikali pamoja na mikopo mingine kwa uwezo wa Manani kupitia Rais Samia na timu yake tutafika tena kwa kuwahi sana.

Je, hili si jambo jema?

316658ce7f9d5000c44620b6fe87a53d.jpg
 
Tulisema tukaonekana wendawazimu, Leo nyie ndio mmethibitisha kuwa MNA matatizo makubwa, niwakumbushe tu kuwa jengeni mifumo na sio mtu, SSH akiondoka mtamsema pia. Samia hatoi pesa na wala haipaswi kutamkwa hivyo ila kwakua ujuaji mwingi hamtakubali
 
Samia mwisho wake ni 2025.

Hayo madeni yameletwa na chama gani? Hata yeye bado ataacha madeni mengi tu, kwa hiyo atakae chukua nchi baada yake na yeye ajisifu, sio? Ama hiyo mikopo atailipa kabla hajaondoka?

Ccm hata wakipewa miaka 1000 ngonjera ni hizi hizi.
 
Huwa naona kama wana ccm Sana matatizo makubwa, hayo madeni makubwa ni yameletwa na chama gani?
Ninafikiri huyu ni Samia mwenyewe anajipigia promo..maana post zake ni kujikweza tuuu mwanzo mwisho.

Fanya kazi mama, ni wajibu wako. Huna sababu ya kujinadi kiasi hicho.
Kibaya kinajitembeza ila kizuri siku zote hujiuza.
 
Samia mwisho wake ni 2015.

Hayo mafeni yameletwa na chama gani? Hata yeye bado ataacha madeni mengi tu, kwa hiyo atakae chukua nchi baada yake na yeye ajisifu, sio? Ama hiyo mikopo atailipa kabla hajaondoka?

Ccm hata wakipewa miaka 1000 ngonjera ni hizi hizi.
Chadema kama chama tu kinawashinda nchi vipi?
 
Huwa naona kama wana ccm Sana matatizo makubwa, hayo madeni makubwa ni yameletwa na chama gani?
CHADEMA umebaki wewe na Mbowe tu,

Madeni ya Serikali sio madeni ya mtu binafsi,

Tunaposema Rais Samia tunamaana ya Taasisi ya "uRais " ila sio Mhe Samia as an entity,

Hayo madeni hata wewe yalikunufaisha naamini,


#KAZIIENDELEE
 
Serikali za wenzetu zinawezaje kufanya mambo ya kunufaisha wananchi huku zikiendelea na miradi mingine ya kiteknolojia
 
Huyo ni chawa wa watu fulani yupo hapa kwa maslahi ya hao.

Asivyojitambua atakwambia yeye ni CCM ukimuuliza hayo madeni yaliletwa na kiongozi wa chama gani ama atapanic ama atamshambulia Magufuli binafsi
Chawa ni wewe, niwapi nimemshambulia mtu hapa?

Soma vizuri between the line mama acha kurukaruka,
 
Hivi dau ni lile lile buku saba au wameongeza kidogo?!
 
Back
Top Bottom