kutokana na Deni la taifa kupaaa, tinaiomba Serikali ihakikishe inadhibiti na kubana matumizi yasiyo ya lazima kwa mfano;
1. Safari za nje zisizo za lazima zizuiwe/zipunguzwe.
2. Vikao vya Bunge zipunguzwe, ratiba ya vikao iangaliwe upya kuanzia mwakani.
3. Matumizi ya magari ya V9/v8 ambayo ni gharama kubwa kuyahudumia,
4. Semina na vikao visivyo vya lazima vipunguzwe.
5. Mishara mikubwa kwa baadhi ya watendaji ipunguzwe, isiwe zaidi ya milioni 10 kwa mtendaji 1.
maana kuna baadhi ya taasisi za serikali watu wanalipwa hadi milioni 15 kwa mwezi.
Kama kweli Serikali yetu pamoja na watendaji wake wana uchungu na watanzania basi lazima wafanye kitu ili kuinisuru nchi na kuelemewa na madeni.
haiwezekani nchi imeandamwa na madeni mpaka puani halafu kuna baadhi ya watu/watendaji wanazidi kunyonya tu bila huruma.
hapana, tunataka kuona hatua zinachukuliwa haraka.