G Malisa: Kamati Kuu ya CCM imewavua nyadhifa zao ndani ya chama viongozi wa UVCCM waliokubali teuzi mpya

G Malisa: Kamati Kuu ya CCM imewavua nyadhifa zao ndani ya chama viongozi wa UVCCM waliokubali teuzi mpya

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Kamati kuu ya CCM imewavua nyadhifa zao viongozi wakuu wa umoja wa vijana baada ya viongozi hao kukubali uteuzi wa nafasi nyingine. Viongozi hao ni Mwenyekiti Kheri James, Makamu Mwenyekiti Tabia Maulid na Katibu mkuu Raymond Mangwala.

Wamevuliwa vyeo vyao kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za CCM no.22 toleo la mwaka 2020 ambazo zinazuia kiongozi kuwa na nafasi mbili (kwenye chama na serikali). Tayari nafasi ya Katibu Mkuu imejazwa na Kenani Kihongosi, na nafasi nyingine zitajazwa baadae.

#MyTake:
Mama anaendelea kuupiga mwingi. Anapanga safu yake kwa akili kubwa sana. Akina Kheri walipoteuliwa kuwa MaDC hawakujua ni mtego. Wakakubali "kichwakichwa" na hatimaye wameliwa vichwa.

M/kiti wa UVCCM hata Katibu wake ni fursa kubwa kuliko UDC. Mkiti anaingia kwenye vikao vya Kamati kuu na halmashauri kuu ya chama. Katibu anaingia kwenye vikao vya sekretarieti. Hakuna siri yoyote ambayo Rais ataongea kwenye chama bila kujua. Akiongea kwenye Kamati kuu, Kheri atasikia na akiongea kwenye Sekretarieti, Raymond atasikia.

Sasa kaamua kuwapiga kanzu. Kuanzia leo Kheri hatakaa ajue chochote kinachojadiliwa na CCM taifa. Atasikia mambo ya CCM Kibangu au Kibamba kwa mangi (wilaya aliyopewa kuongoza). Na huko pia hana uhakika kwa sababu muda wowote mama anaweza kumtengua akitaka kufanya hivyo.

Kwahiyo mdogo wangu Kheri yupo kwenye wakati mgumu sana. Angekua na uwezo angeomba siku zirudi nyuma aukatae UDC ili abaki Mwenyekiti wa vijana, nafasi ambayo ilimpa fursa nyingi ambazo hawezi kuziota akiwa DC.

Mabilioni ya bajeti ya UVCCM yalipita kwake kwa ajili ya approval. Miradi yote inayosimamiwa na UVCCM kuanzia lile ghorofa la vijana pale Lumumba hadi zile fremu za kitimoto pale Iringa, zilikua chini yake.

Kheri alikua anaogopwa na Wabunge viti maalumu wa UVCCM kuliko wanavyoogopa Corona. Hii ni kwa sababu yeye ndiye alikua anapitia mkeka wa wagombea na kukata majina. Sasa hawezi kukata hata jina hata la mgombea udiwani.

Mwaka jana nilikutana na msafara wake mkoani Shinyanga. Polisi barabarani walijipanga kwa nidhamu eti M/kiti UVCCM anapita. Alipewa ulinzi mkali na king'ora kilimuongoza. Leo vyote vimeyeyuka kwa kutegwa na UDC. Mama anaupiga kama N'golo Kante.!

1624386454187.png
 
Hata kama “wangeukataa” uDC, Mama bado alikuwa na power za kuwachomoa kutoka UVCCM. Na hali zao zingekuwa mbaya zaidi huko mbele

Yaani Rais wa Nchi na mwenyekiti wa CCM amepewa mamlaka makubwa mnoo
 
Aise vijana wa CHADEMA wana shida. Baada ya hapa atakayeingia ni UVCCM ambaye naye kazi yake ni kuipigania CCM kwa kila namna. After all, huyu Herry James asingerudi kwenye hiyo nafasi uchaguzi ujao ndani ya CCM.

Sasa kipi bora, amalize mda wake akae benchi au hivi alivyopata UDC. Chongoro hadi anakuwa katibu mkuu alikuwa DC. So mwingine anaweza kuwa na mtazamo kuwa Herry James anaendelea kusogea na kukuwa kiuongozi kwani kwani ni kama ame graduate!
 
Aise vijana wa CHADEMA wana shida. Baada ya hapa atakayeingia ni UVCCM ambaye naye kazi yake ni kuipigania CCM kwa kila namna. After all, huyu Herry James asingerudi kwenye hiyo nafasi uchaguzi ujao ndani ya CCM. Sasa kipi bora, amalize mda wake akae benchi au hivi alivyopata UDC. Chongoro hadi anakuwa katibu mkuu alikuwa DC. So mwingine anaweza kuwa na mtazamo kuwa Herry James anaendelea kusogea na kukuwa kiuongozi kwani kwani ni kama ame graduate!
Kutoka UVCCM Taifa kheri basi angekua RC kama si balozi hata mdogo.
 
Andiko la chuki tu na hakuna kingine, Mama ameupiga mwingi sababu ya kubadili timu? Hivi hawa madogo wanajua wanataka nini kweli?
 
Sidhani kama suala la Kheri James kuteuliwa kuwa DC lilikuwa la utashi wa Kheri James kukubali ama kukataa, ninavyoelewa Rais ana mamlaka makubwa ya kumuhamisha ama kumtoa mteuzi katika nafasi yoyote akihitaji hivyo. Tuache ujuaji
 
Back
Top Bottom