G Malisa: Kamati Kuu ya CCM imewavua nyadhifa zao ndani ya chama viongozi wa UVCCM waliokubali teuzi mpya

Kamati kuu ya CCM imewavua nyadhifa zao viongozi wakuu wa umoja wa vijana baada ya viongozi hao kukubali uteuzi wa nafasi nyingine. Viongozi hao ni Mwenyekiti Kheri James, Makamu Mwenyekiti Tabia Maulid na Katibu mkuu Raymond Mangwala...
Mbona kwa sasa CHADEMA, wakina Malisa,na wengine wanashangilia move za CCM ?Je ,ina maana CHADEMA wamebaki watazamaji?Na washabiki wa makundi ya CCM?
 
huyu malisa huwa simwelewi kabisa.

amekuwa speaker ya michezo ya ccm kuliko chama chake.
 
Naona CCM ameamua kuachana na viongozi wote wajinga wajinga.
 
Mbona Chadema wanashangilia sana maamuzi anayoyafanya Mama utafikiri Chadema na ndo wanufaika wakubwa wa haya mabadiliko? Kwambe Kheri James mlimchukia nae akiharibu chama, Bashiru nae akiharibu Chama, Polepole akiharibu chama na Hayati akiwa kama Mwenyekiti akiharibu chama lakini hizi kauli wanasema Chadema sio CCM wenyewe wenye Chama chao..!! Utasikia wanasema sasa mama ndiyo anarudisha ile CCM yenyewe! Hipi? Ile iliyokatamalaki Rushwa?
Kiongozi juha ndani ya CCM, ana athari kwa watanzania wote, maana CCM ndiyo inaongoza serikali.
 
Mimi naomba kuelimishwa tu nimesoma sehemu kuwa kwa mujibu wa katiba ya chama huwezi kuwa na nafasi 2 kwenye chama na serikali je hii haimuhusu mfano Rais wa nchi maana ni mwenyekiti wa chama pia au watu kama Waziri mkuu na Zanzibar kushika nafasi serikalini na chama.

Mimi nauliza tu labda katiba inasema wanaruhusiwa Rais, PM, Speaker kuwa na vyeo viwili ndani ya chama na serikali. Siulizi kwa ubaya naomba kuelimishwa tu kuhusu katiba ya CCM.
 
Hv chadema akil zao huwa ziko wapi? Yaan wanajadli mambo ya CCM kuliko mambo ya chama chao..kwa nini mnakuwa wapinzani uchwara nyie..ebu pambanieni chama chenu kikue ili wananchi wawaamin kuwapa nchi hii.

Sasa kila kukichaaa mnayawaza mambo ya ccm..aiseee..sijaona upinzani wa ajab kama huu wa tanzania..yaan ni vichwaaa hewaaa kabisaaa...bora hata mboee na heche...

Kidogo wanakahekimaa na misimamo thabit kwa mbali..ila hz paka zingine kama kina sijui malisaa..upuuzi mtupu kabisaa..umbea umbea kutwa kuchaaa..aaahh..mnakeraa mazee.
 
Aise vijana wa CHADEMA wana shida. Baada ya hapa atakayeingia ni UVCCM ambaye naye kazi yake ni kuipigania CCM kwa kila namna. After all, huyu Herry James asingerudi kwenye hiyo nafasi uchaguzi ujao ndani ya CCM.

Sasa kipi bora, amalize mda wake akae benchi au hivi alivyopata UDC. Chongoro hadi anakuwa katibu mkuu alikuwa DC. So mwingine anaweza kuwa na mtazamo kuwa Herry James anaendelea kusogea na kukuwa kiuongozi kwani kwani ni kama ame graduate!
Labda kama ame graduate matusi,utekaji na kuunga mkono uuaji hadharani, ni mjinga tu ndie anaefikiri kama unayofikiri.
Mwerevu anajua kuwa huyo H. James kachomolewa KIAKILI na anytime anatenguliwa kimtego vilevile. Kutoka kuwa kiongozi wa kitaifa tena wa kuchaguliwa na kuwa kiongozi wa wilaya tena wa kuteuliwa!haihitajiki akili kubwa kujua hii ni demotion au promotion.
 
Watu walikuwa wanaleta maneno maneno, tukawaambia subirini apewe instruments of power tuone mtafanya nini.... ndio hivyo tena, hata kama Kheri angetaka kubaki kwenye UVCCM asingeweza, angewezzaje kukataa kazi aliyopewa na Mwenyekiti/President.
 
Brother wewe ndo mjinga, kwani hiyo nafasi ni ya kudumu, unajua Herry we James alikuwa amebakiza mda gani kwenye hiyo nafasi!? Kama nia ni kumchomoa unadhani angeshindwa kusubiri hadi amalize mda wake halafu ndo iwe imetoka na huo ukuu wa Wilaya asiupate!?
Labda kama ame graduate matusi,utekaji na kuunga mkono uuaji hadharani, ni mjinga tu ndie anaefikiri kama unayofikiri.
Mwerevu anajua kuwa huyo H. James kachomolewa KIAKILI na anytime anatenguliwa kimtego vilevile. Kutoka kuwa kiongozi wa kitaifa tena wa kuchaguliwa na kuwa kiongozi wa wilaya tena wa kuteuliwa!haihitajiki akili kubwa kujua hii ni demotion au promotion.
 
Kiongozi juha ndani ya CCM, ana athari kwa watanzania wote, maana CCM ndiyo inaongoza serikali.
Kwaiyo Chadema wanapenda Mama aendelee kufanya vyema? Ili?

Kuna kamsemo kanasema ukiona mpinzaniwako anakushangalia sana jitafakari.
 
Suala la Kheri James aliyekuwa Mwenyekiti UVCCM taifa kuwa DC ni hatua kubwa kwake kisiasa na kiuongozi.

Wengi wa wakuu wa mkoa au mabalozi, wabunge hadi mawaziri wamewahi kuwa wakuu wa wilaya.

Jakaya Kikwete
Majaliwa

Wote walikuwa maDC. Namuona mbali sana kijana Kheri James
 
Kamati kuu ya CCM imewavua nyadhifa zao viongozi wakuu wa umoja wa vijana baada ya viongozi hao kukubali uteuzi wa nafasi nyingine. Viongozi hao ni Mwenyekiti Kheri James, Makamu Mwenyekiti Tabia Maulid na Katibu mkuu Raymond Mangwala.

Wamevuliwa vyeo vyao kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za CCM no.22 toleo la mwaka 2020 ambazo zinazuia kiongozi kuwa na nafasi mbili (kwenye chama na serikali). Tayari nafasi ya Katibu Mkuu imejazwa na Kenani Kihongosi, na nafasi nyingine zitajazwa baadae.

#MyTake:
Mama anaendelea kuupiga mwingi. Anapanga safu yake kwa akili kubwa sana. Akina Kheri walipoteuliwa kuwa MaDC hawakujua ni mtego. Wakakubali "kichwakichwa" na hatimaye wameliwa vichwa.

M/kiti wa UVCCM hata Katibu wake ni fursa kubwa kuliko UDC. Mkiti anaingia kwenye vikao vya Kamati kuu na halmashauri kuu ya chama. Katibu anaingia kwenye vikao vya sekretarieti. Hakuna siri yoyote ambayo Rais ataongea kwenye chama bila kujua. Akiongea kwenye Kamati kuu, Kheri atasikia na akiongea kwenye Sekretarieti, Raymond atasikia.

Sasa kaamua kuwapiga kanzu. Kuanzia leo Kheri hatakaa ajue chochote kinachojadiliwa na CCM taifa. Atasikia mambo ya CCM Kibangu au Kibamba kwa mangi (wilaya aliyopewa kuongoza). Na huko pia hana uhakika kwa sababu muda wowote mama anaweza kumtengua akitaka kufanya hivyo.

Kwahiyo mdogo wangu Kheri yupo kwenye wakati mgumu sana. Angekua na uwezo angeomba siku zirudi nyuma aukatae UDC ili abaki Mwenyekiti wa vijana, nafasi ambayo ilimpa fursa nyingi ambazo hawezi kuziota akiwa DC.

Mabilioni ya bajeti ya UVCCM yalipita kwake kwa ajili ya approval. Miradi yote inayosimamiwa na UVCCM kuanzia lile ghorofa la vijana pale Lumumba hadi zile fremu za kitimoto pale Iringa, zilikua chini yake.

Kheri alikua anaogopwa na Wabunge viti maalumu wa UVCCM kuliko wanavyoogopa Corona. Hii ni kwa sababu yeye ndiye alikua anapitia mkeka wa wagombea na kukata majina. Sasa hawezi kukata hata jina hata la mgombea udiwani.

Mwaka jana nilikutana na msafara wake mkoani Shinyanga. Polisi barabarani walijipanga kwa nidhamu eti M/kiti UVCCM anapita. Alipewa ulinzi mkali na king'ora kilimuongoza. Leo vyote vimeyeyuka kwa kutegwa na UDC. Mama anaupiga kama N'golo Kante.!

View attachment 1826928
Kwani hii ni habari mpya? Mbona miaka yote ni hivyo!
Tatizo ni kuamini kila kinachofanyika kinakomoa watu kumbe NO! Katika hawa, wengine hata hawakuwa na ajira ya mshahara wa kila wiki, leo hii apewe u-DC akatae kwa ajili ya vazi la chama!

Malisa bwege!
 
Brother wewe ndo mjinga, kwani hiyo nafasi ni ya kudumu, unajua Herry we James alikuwa amebakiza mda gani kwenye hiyo nafasi!? Kama nia ni kumchomoa unadhani angeshindwa kusubiri hadi amalize mda wake halafu ndo iwe imetoka na huo ukuu wa Wilaya asiupate!?
Kwa nini wasisubiri muda wake uishe kisha wampe huo ukuu wa wilaya? Ni wazi kuwa kwa hujuma alizokuwa anafanya hakutakiwa awepo ofisi hiyo ya UVCCM ata kwa mwezi mmoja
 
Mkuu kubishana na hawa vijana wa Mbowe inataka moyo sana
 
Wewe ni mjinga!

Wenye maono ya mbali hiyo ni opportunity kwake maana anaweza kupanda hivyo akawa RC mwishowe mbunge hadi waziri mkuu kabisa!

Tatizo la vijana wa Mbowe ni akili fupi huona mwisho zinapoishia nyayo zao tu
 
Kwa mimi kuwa na wazo fulani linaloungwa mkono na watu usiowataka wewe may be kwa ujinga wako tu,haina maana mimi ni mfuasi wa watu hao. Facts ndo kigezo changu
 
Mbowe anaingiaje hapa?
H. James has been demoted and he has been subjected into appointed job in which he can be removed anytime as the president pleases. In former position the president wasn't able to remove him,since he is foolish enough to accept DC position,his doom is obvious!
Kwa hiyo Bashiru na Polepole nao wanasubiri kupanda vyeo?🚮🚮
 
Kwa mimi kuwa na wazo fulani linaloungwa mkono na watu usiowataka wewe may be kwa ujinga wako tu,haina maana mimi ni mfuasi wa watu hao. Facts ndo kigezo changu
Fact ipi sasa hapo?

Ni ujinga kufikiri teuzi anazofanya Samia ni kwa ajili ya kuwakomoa watu flani ndani ya chama

Kwa sisi wenye akili tunaona walioteuliwa udc wamepewa platforms za kuonesha uwezo wao kiuongozi na hatimaye kukwea ngazi za juu zaidi.

Bavicha mnafikiri kimajungu majungu sana kiasi kila anachofanya rais mnaanza kusema pale kafanya ili kumkomoa yule kiakili.

Dogo! Samia ana uwezo wa kumtoa yeyote ndani ya ccm bila kuzunguka zunguka na kupoteza hela za walipa kodi eti ngoja nmtoe kwa kumteua kuwa Dc!
 
Kamati kuu ya CCM imewavua nyadhifa zao viongozi wakuu wa umoja wa vijana baada ya viongozi hao kukubali uteuzi wa nafasi nyingine. Viongozi hao ni Mwenyekiti Kheri James, Makamu Mwenyekiti Tabia Maulid na Katibu mkuu Raymond Mangwala.

Wamevuliwa vyeo vyao kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za CCM no.22 toleo la mwaka 2020 ambazo zinazuia kiongozi kuwa na nafasi mbili (kwenye chama na serikali). Tayari nafasi ya Katibu Mkuu imejazwa na Kenani Kihongosi, na nafasi nyingine zitajazwa baadae.

#MyTake:
Mama anaendelea kuupiga mwingi. Anapanga safu yake kwa akili kubwa sana. Akina Kheri walipoteuliwa kuwa MaDC hawakujua ni mtego. Wakakubali "kichwakichwa" na hatimaye wameliwa vichwa.

M/kiti wa UVCCM hata Katibu wake ni fursa kubwa kuliko UDC. Mkiti anaingia kwenye vikao vya Kamati kuu na halmashauri kuu ya chama. Katibu anaingia kwenye vikao vya sekretarieti. Hakuna siri yoyote ambayo Rais ataongea kwenye chama bila kujua. Akiongea kwenye Kamati kuu, Kheri atasikia na akiongea kwenye Sekretarieti, Raymond atasikia.

Sasa kaamua kuwapiga kanzu. Kuanzia leo Kheri hatakaa ajue chochote kinachojadiliwa na CCM taifa. Atasikia mambo ya CCM Kibangu au Kibamba kwa mangi (wilaya aliyopewa kuongoza). Na huko pia hana uhakika kwa sababu muda wowote mama anaweza kumtengua akitaka kufanya hivyo.

Kwahiyo mdogo wangu Kheri yupo kwenye wakati mgumu sana. Angekua na uwezo angeomba siku zirudi nyuma aukatae UDC ili abaki Mwenyekiti wa vijana, nafasi ambayo ilimpa fursa nyingi ambazo hawezi kuziota akiwa DC.

Mabilioni ya bajeti ya UVCCM yalipita kwake kwa ajili ya approval. Miradi yote inayosimamiwa na UVCCM kuanzia lile ghorofa la vijana pale Lumumba hadi zile fremu za kitimoto pale Iringa, zilikua chini yake.

Kheri alikua anaogopwa na Wabunge viti maalumu wa UVCCM kuliko wanavyoogopa Corona. Hii ni kwa sababu yeye ndiye alikua anapitia mkeka wa wagombea na kukata majina. Sasa hawezi kukata hata jina hata la mgombea udiwani.

Mwaka jana nilikutana na msafara wake mkoani Shinyanga. Polisi barabarani walijipanga kwa nidhamu eti M/kiti UVCCM anapita. Alipewa ulinzi mkali na king'ora kilimuongoza. Leo vyote vimeyeyuka kwa kutegwa na UDC. Mama anaupiga kama N'golo Kante.!

View attachment 1826928
Hii inaitwa tupishe tufanye yetu!! Ila uzuri ni kuwa zimwi likujualo ...............! U-DC si haba!!
 
Back
Top Bottom