G Malisa: Kamati Kuu ya CCM imewavua nyadhifa zao ndani ya chama viongozi wa UVCCM waliokubali teuzi mpya

G Malisa: Kamati Kuu ya CCM imewavua nyadhifa zao ndani ya chama viongozi wa UVCCM waliokubali teuzi mpya

Hata kama “wangeukataa” uDC, Mama bado alikuwa na power za kuwachomoa kutoka UVCCM. Na hali zao zingekuwa mbaya zaidi huko mbele

Yaani Rais wa Nchi na mwenyekiti wa CCM amepewa mamlaka makubwa mnoo
wacha waliwe si ndo hao hao wanaolikumbatia likatiba la hovyo.ngoja wakae benchi nao akili ziwasogee kidogo.kazi iendelee.
 
Wewe unao
Kamati kuu ya CCM imewavua nyadhifa zao viongozi wakuu wa umoja wa vijana baada ya viongozi hao kukubali uteuzi wa nafasi nyingine. Viongozi hao ni Mwenyekiti Kheri James, Makamu Mwenyekiti Tabia Maulid na Katibu mkuu Raymond Mangwala.

Wamevuliwa vyeo vyao kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za CCM no.22 toleo la mwaka 2020 ambazo zinazuia kiongozi kuwa na nafasi mbili (kwenye chama na serikali). Tayari nafasi ya Katibu Mkuu imejazwa na Kenani Kihongosi, na nafasi nyingine zitajazwa baadae.

#MyTake:
Mama anaendelea kuupiga mwingi. Anapanga safu yake kwa akili kubwa sana. Akina Kheri walipoteuliwa kuwa MaDC hawakujua ni mtego. Wakakubali "kichwakichwa" na hatimaye wameliwa vichwa.

M/kiti wa UVCCM hata Katibu wake ni fursa kubwa kuliko UDC. Mkiti anaingia kwenye vikao vya Kamati kuu na halmashauri kuu ya chama. Katibu anaingia kwenye vikao vya sekretarieti. Hakuna siri yoyote ambayo Rais ataongea kwenye chama bila kujua. Akiongea kwenye Kamati kuu, Kheri atasikia na akiongea kwenye Sekretarieti, Raymond atasikia.

Sasa kaamua kuwapiga kanzu. Kuanzia leo Kheri hatakaa ajue chochote kinachojadiliwa na CCM taifa. Atasikia mambo ya CCM Kibangu au Kibamba kwa mangi (wilaya aliyopewa kuongoza). Na huko pia hana uhakika kwa sababu muda wowote mama anaweza kumtengua akitaka kufanya hivyo.

Kwahiyo mdogo wangu Kheri yupo kwenye wakati mgumu sana. Angekua na uwezo angeomba siku zirudi nyuma aukatae UDC ili abaki Mwenyekiti wa vijana, nafasi ambayo ilimpa fursa nyingi ambazo hawezi kuziota akiwa DC.

Mabilioni ya bajeti ya UVCCM yalipita kwake kwa ajili ya approval. Miradi yote inayosimamiwa na UVCCM kuanzia lile ghorofa la vijana pale Lumumba hadi zile fremu za kitimoto pale Iringa, zilikua chini yake.

Kheri alikua anaogopwa na Wabunge viti maalumu wa UVCCM kuliko wanavyoogopa Corona. Hii ni kwa sababu yeye ndiye alikua anapitia mkeka wa wagombea na kukata majina. Sasa hawezi kukata hata jina hata la mgombea udiwani.

Mwaka jana nilikutana na msafara wake mkoani Shinyanga. Polisi barabarani walijipanga kwa nidhamu eti M/kiti UVCCM anapita. Alipewa ulinzi mkali na king'ora kilimuongoza. Leo vyote vimeyeyuka kwa kutegwa na UDC. Mama anaupiga kama N'golo Kante.!

View attachment 1826928
Wewe unaokota kipi huko chadema?
Unaweza kuona huzuni kwenye nafasibya heri james kweli au?
Katupiwa mfupa angalau mdogo.

Yeye bado kavaa nguo wewe ambae uko uchi unaweza kumuonea huruma aliyevaa?
Tanzania na watu wake ni kazi kweli.
Unamcheka anayekula ili hali wewe hujui utakula lini.
 
Fact ipi sasa hapo?

Ni ujinga kufikiri teuzi anazofanya Samia ni kwa ajili ya kuwakomoa watu flani ndani ya chama

Kwa sisi wenye akili tunaona walioteuliwa udc wamepewa platforms za kuonesha uwezo wao kiuongozi na hatimaye kukwea ngazi za juu zaidi.

Bavicha mnafikiri kimajungu majungu sana kiasi kila anachofanya rais mnaanza kusema pale kafanya ili kumkomoa yule kiakili.

Dogo! Samia ana uwezo wa kumtoa yeyote ndani ya ccm bila kuzunguka zunguka na kupoteza hela za walipa kodi eti ngoja nmtoe kwa kumteua kuwa Dc!
Umeisoma katiba ya CCM kuhusu position aliyokuwa nayo James na namna anavyoweza kuondolewa?
Samia amejipambanua kuwa yeye ni mfuata sheria sio kama yule 'mtembea zake' aliewaaminisha kuwa Rais anaweza kufanya anavyotaka na yuko juu ya sheria. Ivyo sio kweli kuwa Rais angeweza tu kumuondoa James UVCCM. Katiba ya CCM hairuhusu huo ujinga unaosema!
Kwa ujinga huu wa baadhi ya wanachama wa CCM,no wonder mwendazake mlimfanya kama Mungu mtu
 
Umeisoma katiba ya CCM kuhusu position alivyokuwa nayo James?
Samia amejipambanua kuwa yeye ni mfuata sheria sio kama yule 'mtembea zake' aliewaaminisha kuwa Rais anaweza kufanya anavyotaka na yuko juu ya sheria. Ivyo sio kweli kuwa Rais angeweza tu kumuondoa James UVCCM. Katiba ya CCM hairuhusu huo ujinga unaosema!
Wewe ni punguani!

Basi baki na upunguani wako

Haya Kheri James kaondolewa na Samia kwa kumpa udc na sasa kesho atamtumbua!
 
Aise vijana wa CHADEMA wana shida. Baada ya hapa atakayeingia ni UVCCM ambaye naye kazi yake ni kuipigania CCM kwa kila namna. After all, huyu Herry James asingerudi kwenye hiyo nafasi uchaguzi ujao ndani ya CCM.

Sasa kipi bora, amalize mda wake akae benchi au hivi alivyopata UDC. Chongoro hadi anakuwa katibu mkuu alikuwa DC. So mwingine anaweza kuwa na mtazamo kuwa Herry James anaendelea kusogea na kukuwa kiuongozi kwani kwani ni kama ame graduate!
Lakini hoja ya Malisa G, ni kwamba Mazaa amempangua Kheri James kistaharabu, kama alivyo mpangua Kakurwa! Hoja hapa, Mazaa anasafisha ma-sukumagang kutoka kwenye system, kimtindo!
Pia ccm watamleta kijana mwingine, kama ambavyo sasa hivi kuna raisi mwingine, lakini ujue ni afadhali Mazaa kuliko mwendazake, (sore, marehemu)! At liest kwetu BAVICHA!
 
M/kiti wa UVCCM hata Katibu wake ni fursa kubwa kuliko UDC. Mkiti anaingia kwenye vikao vya Kamati kuu na halmashauri kuu ya chama. Katibu anaingia kwenye vikao vya sekretarieti. Hakuna siri yoyote ambayo Rais ataongea kwenye chama bila kujua. Akiongea kwenye Kamati kuu, Kheri atasikia na akiongea kwenye Sekretarieti, Raymond atasikia.
Vipi kuhusu maslah?
 
Huyu Malisa Mbona yupo busy kuzungumzia sana mambo ya chama chakavu kuliko chama pendwa cdm? Au anataka mama amuone apewe uteuzi.
Hawa vijana sio wa kuwaamini kabisA
Huyu Malisa Mbona yupo busy kuzungumzia sana mambo ya chama chakavu kuliko chama pendwa cdm? Au anataka mama amuone apewe uteuzi.
Hawa vijana sio wa kuwaamini kabisA
Aisee mkuu jamaa anajipendekeza sana aisee. Anatumia wings ya kushoto ya Sukumagang kustrike(kujipendekeza) .

Hajitambui kabsaaa. Huu ni wakati wa kujenga Chama chake cha Cdm.
 
Wewe ni punguani!

Basi baki na upunguani wako

Haya Kheri James kaondolewa na Samia kwa kumpa udc na sasa kesho atamtumbua!
Ujinga wenu unawamaliza,kaanza PolePole akafuata Bashiru na sasa Herry James!
Na hawa wote mnawatolea hoja nyepesi eti wamepewa fursa ili wapate vyeo zaidi, ni mjinga tu wa level yako ndo haelewi mchezo wa wenye akili ulivyo. Ndio maana kwa akili zenu ndogo na nzito inawapa taabu kuwaelewa watu wenye akili. Mjinga umuelewa mjinga mwenzake,mwenye akili anaeleweka kwa wenye akili wenzake. Ivyo dunia ya wajinga na wenye akili ni sawa na Mbingu na ardhi.
 
Wamebadilishwa vyeo lakini matendo yao ni yale yale
80% ya wateuliwa hawafai kulipwa pesa za walipa kodi kwa kuwa ni
Wanyanyasaji wa walipa kodi
Waongo
Wabinafsi
Wamekosa maadili
Wabinafsi
Elimu Uelewa mdogo
Wahuni tu
Dhuluma chuki visasi ndio sifa ya kuwa kiongozi kwa watawala
Fadhila zinaliangamiza Taifa

Tulipo
Serikali ijiuzulu
Bunge livunjwe
Katiba Mpya
Uchaguzi Uitishwe

Tuanze Upya

**mods tafadhalini sana msifute kila 'kukosoa na kusema ukweli
Taifa Jipya linahitajika kwa kuwaambia ukweli wahusika
Leo akina mobetto sijui samatha wanapewa wadhifa kuhusiana na pesa za walipa kodi ... this is a joke
 
Mbona Chadema wanashangilia sana maamuzi anayoyafanya Mama utafikiri Chadema na ndo wanufaika wakubwa wa haya mabadiliko? Kwambe Kheri James mlimchukia nae akiharibu chama, Bashiru nae akiharibu Chama, Polepole akiharibu chama na Hayati akiwa kama Mwenyekiti akiharibu chama lakini hizi kauli wanasema Chadema sio CCM wenyewe wenye Chama chao..!! Utasikia wanasema sasa mama ndiyo anarudisha ile CCM yenyewe! Hipi? Ile iliyokatamalaki Rushwa?
Mama anakula na nyie sahani moja, mlizoea kuendesha nchi kihuni na kijambazi, mimi ni ccm kwa taarifa yako
 
Wewe ni mjinga!

Wenye maono ya mbali hiyo ni opportunity kwake maana anaweza kupanda hivyo akawa RC mwishowe mbunge hadi waziri mkuu kabisa!

Tatizo la vijana wa Mbowe ni akili fupi huona mwisho zinapoishia nyayo zao tu
Hiyo takataka iwe Waziri Mkuu?
 
Mama anakula na nyie sahani moja, mlizoea kuendesha nchi kihuni na kijambazi, mimi ni ccm kwa taarifa yako
Anakula nao sahani moja?

Kivipi maana anawatoa hapa na kuwapeleka kwenye ulaji zaidi
 
Back
Top Bottom