Pre GE2025 Gambo ajibu mapigo ya Makonda "mimi nimeenda shule"

Pre GE2025 Gambo ajibu mapigo ya Makonda "mimi nimeenda shule"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kama madiwani ni wawakilishi wa wananchi , mbunge ni muwakilishi wa nani!? Sio kazi ya madiwani kuamua nani awe mbunge au huyu hafai kuwa mbunge, hiyo ni kazi ya wananchi. Hata Rais ana nguvu ya kulivunja Bunge pia, je wabunge wanakuwa hawafai!?
Hongera kwa kuvunja record ya kuandika comment ya kipuuzi tangu jf ianzishwe
 
Paul Makonda a.k.a Albert Bashite Malyangili, yeye ndiye mwenye shida. Anaingilia majukumu ya Mbunge ktk namna ya hujuma kwa kutumia madaraka yake ya ukuu wa mkoa kumhujumu mbunge aliyechaguliwa na wananchi...

Anafanya hivi kwa sababu naye anautaka ubunge akidhani anaweza kuupata...

Na hii tabia, ndiyo iliyomponza mwaka 2019 akiwa RC wa DSM wakati huohuo akilitamani jimbo la Kigamboni ambalo alishindwa kwenye kura za maoni tu ndani ya chama chake na kwa sababu hiyo akaukosa ubunge na kuupoteza ukuu wa mkoa kwa wakati mmoja...

Paul Makonda hawezi kuwa mbunge wa Arusha hata afanyeje...!!
Kama Gambo ameuweza ubunge Makonda hawezi kuushindwa.
 
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mrisho Gambo, amejibu mashambulizi yanayohusiana na wito ulioibuliwa na baadhi ya madiwani wa jiji la Arusha wakimuomba Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, kuchukua fomu ya kugombea ubunge wa jimbo hilo.

Gambo amesema kuwa yeye anatekeleza majukumu yake kama mbunge kwa ufanisi na kujivunia elimu yake, akisisitiza kuwa hakuna aliye na haki ya kumzuia kufanya kazi aliyopewa na wananchi.

Soma, Pia: Kumekucha: Madiwani Arusha waomba Paul Makonda agombee Ubunge jimbo la Arusha Mjini

"Tofauti kati ya mtu aliyeenda shule na mtu ambaye shule yake ni ya mashaka ipo wazi," alisema akisisitiza kuwa ni muhimu kwa kiongozi kuwa na elimu ya kweli ili kuhakikisha kuwa anatekeleza majukumu yake ipasavyo na kusisitiza kuwa

"Ni lazima ifike mahali uoneshe tofauti ya mtu ambaye amekwenda shule na mtu ambaye shule yake ni ya kubabaisha au ni ya mashaka. Kwa sisi ambao tuna uhakika na shule zetu, kila jambo linapotokea tunahitaji kutafakari na kufikiria na kuangalia athari ya kila kinachofanyika," aliongeza.

Katika kujibu wito wa baadhi ya madiwani ambao walimuomba Makonda achukue fomu ya kugombea ubunge, Gambo amesema kuwa hakuna mtu anayekatazwa kugombea ubunge, lakini akasisitiza kuwa mbunge anachaguliwa na wananchi na sio madiwani.

"Kama mtu ana ndoto ya kuwa mbunge, aache njia za mkato. Asubiri utaratibu na aje kwenye uchaguzi, aone kama ngoma ya kitoto inakesha," alisema kwa kujiamini.

Gambo amebainisha u pia shutuma za kwamba watu wanajaribu kutumia mamlaka zao kuingilia mchakato wa uchaguzi na kutaka kumchafua.

"Kuna watu wanaona kazi inakwenda na wananchi wanatukubali, wanataka kutumia mamlaka yao kutuchafua na kuleta ajenda zisizo na msingi.

Mbunge huyo pia amekosoa vikali hali ya baadhi ya wanasiasa kutoa machozi kwa sababu ya kushindwa kupata fedha walizokuwa wakitarajia kutumika kinyume na utaratibu.

"Kama kuna mtu analia kwa kupoteza fedha alizokuwa akitarajia, machozi hayo ni ya halali kwa sababu walijua wazi kuwa wangezitumia kwa manufaa yao binafsi," aliongeza.

Kwa kumalizia, Gambo amekumbusha kuwa yeye ni mbunge anayetekeleza majukumu yake kwa manufaa ya wananchi wa Arusha Mjini, na hakutakuwa na mtu yeyote atakayemzuia kufanya hivyo kwa kufuata utaratibu.
View attachment 3249376
Gambo ana shule gani? Ulimwengu huu bado kuna first degree holder anayejiona msomi? Degree zimekua kama certificate tuu.
 
Hawa wote wanangu! battle hii nimeshindwa kujigawa! ila wakae chini wamalize Tofauti zao! kama ni Jimbo Mwanangu Makonda njoo Kigamboni njia nyeupeeee! Gambo aendelee kuwanyoosha Atown.
 
Aise! Gambo anatonesha majeraha sasa!
Nadhani kila mtu afanye kazi yake aliyoitiwa kuifanya Arusha.
Mbunge afanye kazi zake kama Mbunge,RC afanye kazi zake kama RC!
Changamoto nayo iona wote ni Vijana,wanasukumwa na mihemko ya Ujana.
Mama Abdul atatue mgogoro huo!
Atatue vipi sasa na hawa wote shida yao ni ubunge,awape wote ubunge?.
 
Kwa mtazamo wangu, ukiwa msomi wala huna haja ya kujitangaza bali matendo yako yatawaonyesha watu kuwa wewe ni msomi!! Kwa majibu ya namna hii na kujigamba kwingi, hapo shule hamna! Zaidi anaendeshwa na mihemuko!!!
Hayo majigambo yake ndio ulipo mtego utakaomuangusha. Anao uhaya wa kujivuna.

Sio mbaya kuwa na huo ujivuni ikiwa unao pia unyenyekevu na ile hali ya kujishusha, kwa bahati mbaya hana sifa hiyo.
 
Sasa naelewa ile sintofahamu mbele ya waziri wa ujenzi.... Joto la 2025 😂😂😂
 
Back
Top Bottom