Mkuuu kawe sehemu gani ?tupige research kwa Mara ingine,Tufanye kazi, pia inaweza kusaidia kujua masingira halisi ya kazi .Niliwahi kumiliki hii biashara miaka fulani maeneo ya Kawe. Asee kuna mzazi alikuja kunivamia ghafla sina hili wala lile eti namkosesha mwanae hafanyi homework akirudi shule ni game tu.
Tulipigana mpk kwenda kuamuriwa serikali za mtaa.[emoji23]
Kuna dogo mmja mshua nilikuwa nampa mashine moja yote na Pad anaenda kucheza nyumbani kwao ananilipa hesabu ya siku nzima elfu 30 hapo nakuwa na uhakika plus hesabu ya umeme sina.
Nilikuwa napendwa na madogo na kuchukiwa na wazazi.
Ikifika usiku masela wanakuja kucheza kamali wanaweka hela ukifungwa unalipa hela ya mchezo na hela ya bet.
Ni biashara nzuri ila siwezi kuifanya tena sababu ya ugomvi na wazazi na kuitwa serikali za mtaa lakin pia age yangu sasa kudeal na watoto ni ngumu.
Nahitaji Sana kuwekeza