Gamondi aambiwe ukweli plan za klabu bingwa sio kama unaenda kucheza na Dodoma jiji

Gamondi aambiwe ukweli plan za klabu bingwa sio kama unaenda kucheza na Dodoma jiji

Mkuu hiki ndicho nilichokiona, Yanga walikosa heshma kwenye hii game. Hawa waarabu ni wazuri ila wanafungika. Jana Yanga alifunguka sana, tungekuwa na nidhamu ya kulinda tungeweza pata hata draw. Timu inashambulia inasahau kujilinda, Yanga kafungwa magoli ya counter karibia yote. Lomalisa anapanda afu anachelewa kurudi, goli mbili zilipita humo.
Kwenye mechi kubwa Yanga wapunguze mbwembwe na wacheze mchezo wa kasi na pasi ndefu.
Kwa timu zinazolingana kiuwezo ni ngumu sana kuwafunga kwa njia hii ya kujenga mashambulizi ya taratibu kuanzia nyuma. Gamond atafute clips aangalie vile Nabi alikuwa anacheza hizi game.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
Hii ni Club bingwa wala siyo shirikisho
Shirikisho ukicheza ule mchezo wa Yanga kupata ushindi ni chap maana kule kuna wabovu wote kwahiyo anatafuta mbovu mwenye afadhali.
Champion league ni ligi ya mabingwa kwahiyo anayetafutwa ni bingwa zaidi yaani kadri unavyosonga mbele ndivyo unakutana na timu nzuri zaidi.
 
Wanaweweseka na kipigo kitakatitfu cha November 5
Mngefanya kama ile timu waliyoifunga Argentina kombe la dunia. Wenzenu walifanya sherehe kwao na watu hawakwenda makazini kusherekea ushindi.
Nanyi mfanye sherehe na mtengeneze documentary kukumbuka ushindi wa Simba.
Mkikutana na wababe wenzenu wanaotoa dozi 5 kama nyie manaogelea magoli. Ushindi wenu ni kwa NBC league tu?
 
Kwamba yeye aliye kwenye tasnia halijui hilo??

WEwe mdau , shsbiki au mpenzi.. baki kwenye mipaka yako. Soka itaendelea.

Ukipewa hiyo timu UTAIWEZA kufundisha na kupanga?
 
GAMONDI AAMBIWE UKWELI PLAN ZA KLABU BINGWA SIO KAMA UNAENDA KUCHEZA NA DODOMA JIJI.

Yanga ilikosa Heshima Kwa Mpinzani wake CR BELOUZDAD Jinsi ambavyo iliamua kuuendea Mchezo Huu Hali iliyopelekea Kuruhusu Magoli Matatu Kwa Mtungi Ugenini

Hakukuwa na Haja ya Kufunguka Katika Mchezo wa Ugenini Plan Kubwa Ambayo ingetumika Ingekuwa ni Counter Attack na Kuzuia

GAMONDI Aambiwe Ukweli kuwa hii ni Michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika na Sio Kombe la Shirikisho Wala NBC PREMIER LEAGUE

Ukweli Usemwe Huwezi Kucheza na Cr Belouzdad kama unaenda Kucheza na Dodoma jiji Yanga ilifeli kwenye Game Plan ya Ugenini

Mchezo unaofata Dhidi ya Al Ahly ni Mgumu Zaidi ya Huu waliocheza na CR BELOUZDAD Isipojipanga kisawasawa tutarajie ikienda Kupoteza Mchezo mwingine wa pili
Acha boli litembee, Acha atembee na falsafa yake. Yeye kama kocha anajua akifanyacho.
 
Hii ni Club bingwa wala siyo shirikisho
Shirikisho ukicheza ule mchezo wa Yanga kupata ushindi ni chap maana kule kuna wabovu wote kwahiyo anatafuta mbovu mwenye afadhali.
Champion league ni ligi ya mabingwa kwahiyo anayetafutwa ni bingwa zaidi yaani kadri unavyosonga mbele ndivyo unakutana na timu nzuri zaidi.
Hio shirikisho mlicheza na huo mpira wenu wa champions League mlifika wapi?
 
Yanga waliachiwa wacheze mpira kwa lengo la kuwahadaa, walipojaa kwenye plan hiyo wale jamaa wakawafunua kisha wakawachungulia mara tatu
Acha ujinga!
Hakuna timu duniani iliyowahi kufanya huo upuuzi wa kumwacha adui acheze,
Hicho kitu hakipo
Ukiona timu ipo nyuma ujue imezidiwa possession!
Timu gani inamuacha adui acheze na wakati huohuo wachezaji wanapambana kunyang'anya mpira?
Na wakiupata mpira wanapambana wasinyang'anywe?
Kauli hizi hua za kijinga Sana!
Possession ya mpira Ni uwezo wa timu, na husababisha timu ipande muda wote!
Kukaba na kushambulia kwa kaunta inawezekana tu pale ambapo unayecheza nae ana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira

Possession ni factor ya kwanza ya ushindi!
Kwenye ligi zote duniani, timu zenye uwezo wa possession ndizo kwa kawaida zinazobeba ubingwa wa ligi
Yanga alifika fainali shirikisho sababu ya possession
Pamoja na kupigwa tatu, kwenye mchezo wake wa juzi, Ila technically Yanga ndiye alikuwa na nafasi ya ushindi
Unamwachaje mpinzani acheze ili upigwe 5?
 
Back
Top Bottom