Gamondi aambiwe ukweli plan za klabu bingwa sio kama unaenda kucheza na Dodoma jiji

Hii ni Club bingwa wala siyo shirikisho
Shirikisho ukicheza ule mchezo wa Yanga kupata ushindi ni chap maana kule kuna wabovu wote kwahiyo anatafuta mbovu mwenye afadhali.
Champion league ni ligi ya mabingwa kwahiyo anayetafutwa ni bingwa zaidi yaani kadri unavyosonga mbele ndivyo unakutana na timu nzuri zaidi.
 
Wanaweweseka na kipigo kitakatitfu cha November 5
Mngefanya kama ile timu waliyoifunga Argentina kombe la dunia. Wenzenu walifanya sherehe kwao na watu hawakwenda makazini kusherekea ushindi.
Nanyi mfanye sherehe na mtengeneze documentary kukumbuka ushindi wa Simba.
Mkikutana na wababe wenzenu wanaotoa dozi 5 kama nyie manaogelea magoli. Ushindi wenu ni kwa NBC league tu?
 
Kwamba yeye aliye kwenye tasnia halijui hilo??

WEwe mdau , shsbiki au mpenzi.. baki kwenye mipaka yako. Soka itaendelea.

Ukipewa hiyo timu UTAIWEZA kufundisha na kupanga?
 
Acha boli litembee, Acha atembee na falsafa yake. Yeye kama kocha anajua akifanyacho.
 
Hio shirikisho mlicheza na huo mpira wenu wa champions League mlifika wapi?
 
Yanga waliachiwa wacheze mpira kwa lengo la kuwahadaa, walipojaa kwenye plan hiyo wale jamaa wakawafunua kisha wakawachungulia mara tatu
Acha ujinga!
Hakuna timu duniani iliyowahi kufanya huo upuuzi wa kumwacha adui acheze,
Hicho kitu hakipo
Ukiona timu ipo nyuma ujue imezidiwa possession!
Timu gani inamuacha adui acheze na wakati huohuo wachezaji wanapambana kunyang'anya mpira?
Na wakiupata mpira wanapambana wasinyang'anywe?
Kauli hizi hua za kijinga Sana!
Possession ya mpira Ni uwezo wa timu, na husababisha timu ipande muda wote!
Kukaba na kushambulia kwa kaunta inawezekana tu pale ambapo unayecheza nae ana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira

Possession ni factor ya kwanza ya ushindi!
Kwenye ligi zote duniani, timu zenye uwezo wa possession ndizo kwa kawaida zinazobeba ubingwa wa ligi
Yanga alifika fainali shirikisho sababu ya possession
Pamoja na kupigwa tatu, kwenye mchezo wake wa juzi, Ila technically Yanga ndiye alikuwa na nafasi ya ushindi
Unamwachaje mpinzani acheze ili upigwe 5?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…