Gamondi hamna kocha, Yanga ligi hachukui, atapoteza mechi zote kubwa, today I have seen the light

Yupo bado
Anafanya vizuri au ndio hivyo tuu!?
Wamtimue arudi tu jangwani kiukweli hakuna kocha niliowahi muelewa falsafa zake kama Nabi.
Muhimu ni ushindi pia alikua mgumu kuruhusu magoli.
 
Ungeandika kwa kiswahili kitupu pasipo kuchanganya lugha ungeeleweka vizuri.. Unahoja lakini uwasilishaji wako niwakilimbukeni

Mtoe nje "amna kitu hapa" muingize "hamna kitu hapa".
"Ana mipingo", hebu nitafsirie kwa kiswahili ili nielewe ni nini.
 
Anafanya vizuri au ndio hivyo tuu!?
Wamtimue arudi tu jangwani kiukweli hakuna kocha niliowahi muelewa falsafa zake kama Nabi.
Muhimu ni ushindi pia alikua mgumu kuruhusu magoli.
Ukienda kwa takwimu kati ya Nabi akiwa Yanga na Gamondi, za Gamondi zipo juu kwenye ligi kuu.
Tukija kwenye klabu bingwa, Yanga imekutana na test ngumu tatu
Medeama, Belouizdad na Al Ahly lakini timu imeweza kuruka kihunzi ila Nabi kakutana na Etoil du Sahel imemtoa mashindanoni.

Budget ya Far Rabat na Yanga, ya Rabat ipo juu lakini timu Yanga inacheza robo fainali ya klabu bingwa
 
KAtika takwimu kaka labda za magoli zipo juu.
Ila tukitizama idadi ya mechi kufungwa yule jamaa Nabi kafungwa mechi chache sana pia karuhusu magoli machache mnooo kuliko Gamondi.
Gamondi ukimuotea unamfumua kisawasawa,ila Yanga ya Nabi ilikua ukiiotea haichelewi kujirudisha mchezoni na kudhibiti madhara zaidi.
Mifumo ya Nabi migumu kuielewa hata El Merrekh si walimlalamikia na kumfukuza.
Huwenda Far Rabat pia wanapitia hiko hiko.
 
most of time huwa namuona kocha kama anazinguua ila watu ninaofanya nao mjadala wana utimu sana ..vitu tactical kuviona hawawezi....mzize namkubali sana na kuna baadhi ya mechi naona uhitaji wake lakini atangangana na kina msonda dakika za kufungia anamingiza...sio hilo tu kuna vingi vinavyoashiria hajui au hawezi kuwa kocha bora yanga anashambulia sawa ...kujilinda anasahau sana au kuheshimu mppinzani
 
with all due respect mpira umeanza kufuatilia lini?
 
Timu ilichoka, wachezaji wa Yanga wanatumia nguvu nyingi wanapokuwa uwanjani, aina ya mpira wa Gamondi ni wote mnatakiwa kuwa mabeki pindi mkiwa hamna mpira hivyo inawafanya wachezaji wa press kwa nguvu ili kuwin mipira na timu inakuwa inacheza kwa kasi sana. Ile kucheza mfululizo kumewafanya wachezaji wawe wamechoka. Ukiangalia magoli ya Azam waliofunga yote mawili ni ya kizembe kwa watu kuishia kukabia macho kitu ambacho sio kawaida kwa Yanga.
 
Kufungwa mara moja tu Gamondi anayooshewa kidole hivi. Kocha poa tu huyu.. Sasa sijui itakuwaje ikitokea Uto ikapigwa kwenye mechi zinazofuata nje ndani na Mamelody?
 
uwe mvumilivu bro,mpira ndio ulivyo
 
Kingine kinachonifanya nimvue vyeo ni kumchezesha Sure boy kama no.6 badala ya 8, najiuliza kina mkude na mauya waliwasajili wa nini!
 
Ntakukubalia kwa Gamondi maana sometimes anafanya makosa sijui kwa makusudi au bahati mbaya maana huwezi Anza na kibabage katika game ambayo unajua wapinzani Wana ma winger hatari kibabage faida yake ipo kwenye kushambulia tu ila kukaba hamna kitu na ndo maana baadhi ya makocha huko alikopita walikua wanamtumia kama winger.

Kosa kingine kubwa alilofanya ni Ile sub ya kingia Guede asee huyu mchezaji ni ovyo kabisa Yuko very slow na maamuzi yake kwenye kutoa pasi sio mazuri.

Lakini haya lazima yatokee Ili tujue panapovuja.
 
Kila siku . Panavuja tu
 
Kufungwa mara moja tu Gamondi anayooshewa kidole hivi. Kocha poa tu huyu.. Sasa sijui itakuwaje ikitokea Uto ikapigwa kwenye mechi zinazofuata nje ndani na Mamelody?

Huyu hadi sasa , watu wanamtafuta alternative yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…