Gamondi wachezaji wanakuangusha!

Gamondi wachezaji wanakuangusha!

Moshi25

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2022
Posts
2,555
Reaction score
4,118
Leo wachezaji wa Yanga hawakucheza kitimu kama mechi na mtani ya 5G, wakiendelea hivi na ubinafsi, makundi tu tutaumaliza mwendo,

Wao waliamua kutumia fursa kuonesha uwezo binafsi, kwa vile klabu bingwa inaoneshwa Dunia nzima, walikuwa anao anao tu mbwembwe kibao kulazimisha kupiga chenga za kijinga kijiji kizima , hawaangalii pembeni wala kutoa pasi.

Leo wamepoteza mipira mingi sana kila mmoja anataka sifa za kijinga za kufunga hasa Max, Pakome, Mzize na Aziz Ki walitaka tu kuonekana na Ahly kuwa wanajua mpira! Ili labda iwakumbuke kwenye ufalme wao.

Gamondi tafadhali weka chini wachezaji wako waambie Leo hawakutenda haki kwa mashabiki wa Yanga, waache ubinafsi wacheze kama timu!

Uzi tayari.
 
Wachezaji wa YANGA Wana shida ya kutetemeka miguu,pasi nyingi wanampa adui. Ukitaka kumuweza mwarabu lazima uwe na lijitu mbele lenye miguvu na mbio zaidi ya bolt. Lakini hivi vipas vya Moja Moja wajamaa wanajua kuziba nafasi hutoboi
 
Wachezaji wa YANGA Wana shida ya kutetemeka miguu,pasi nyingi wanampa adui. Ukitaka kumuweza mwarabu lazima uwe na lijitu mbele lenye miguvu na mbio zaidi ya bolt. Lakini hivi vipas vya Moja Moja wajamaa wanajua kuziba nafasi hutoboi
Upo sahihi kuna matukio machache walifanya hivyo Ila Kwenye takwimu za mwisho yanga waliizidi al ahly Kwenye asilimia za usahihi .
Kosa kubwa ni kuto kushuti wakifika karibu na goli ,walifika sana golini kuliko al ahly wakata kupiga chenga bila malengo .
Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi maalumu ya kushuti kwa mbali kama ya penalti
 
Ye mwenyewe kachelewa sana kufanya sub halafu Farid Musa huwa anacheza namba tatu vizuri zaidi ya kibabage ila inaonekana hayuko kwenye mipango yake
Musonda angeingia mapema na Mudathir game ingekaa poa
Farid alikua hata sub? Mara ya mwisho hata kumuona tu Farid Musa uwanjani ilikua lini?
 
Shida yetu ni kuwapa Elimu Watopolo kuwa kuingia robo fainali si jambo jepesi jepesi, hivyo Simba iheshimiwe kwa kuingia hatua hiyo mfululizo kwa miaka kadhaa.

Kumbuka:kuingia makundi tu umetumia takribani miaka 25.

Na bado hatoboi anaishia hapo hapo makundi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom