Gardner G Habash: Najuta kuachana na mke wangu wa kwanza

Gardner G Habash: Najuta kuachana na mke wangu wa kwanza

gadner nae mbea, wakat anaendesha murano ya jide na range rover alikua hajutii? leo katoswa ndo anajifanya nyoko nyoko, atajibeba mwaka huu, ndio maana matapishi ya clouds
Watu kama ninyi mpo tayari kuona hata mtu anakulala jalalani au kulala sakafuni kisa tu alikosea, na ndio yafaa kua malipizi yake. Yeye mwenyewe ameishakiri kosa na kujutia yote aliyoyafanya huko nyuma, sasa ya nini kuonekana una Roho ya "korosho" na mwepesi wa malipizi. Laiti kama binadamu wote wangekua na Roho kama yako asingebakia binadamu yeyote katika ulimwengu huu.
 
Shangaa huyo mwanaume wa Rukwa huko hajui hata hili jukwaa ni la celebrities. ....halafu anamsema bi Warumi.
Au anataka kuhamia Dar nini
anatamani kuja dar sema nauli hana huyo
 
Bora Gadner hajazungumzia ya mtalaka wake maana angekua Sadifa hapo angemwagika kama urojo
ahahaha ila sadifa noma, yule ata akikununulia chupi anatangaza instagram
 
Mtangazaji wa Clouds FM, Gardner G Habash amesema miongoni mwa vitu anavyojutia katika maisha yake ni kuachana na mke wa kwanza aliyezaa naye mtoto wa kike, Karen, ambaye kwa sasa yupo mwaka wa pili chuoni.

Akiongea kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV, Gardner alisema kutokana na kubadilisha kazi ya awali na kuwa mfanyabiashara kipindi anaishi Mwanza, alijikuta akiiweka kwenye mawe ndoa yake kwa kukosa muda nayo.

“Yale mazingira niliyokutana nayo Mwanza ya kibiashara yalisababisha nikaachana na mke wangu wa kwanza, ni kitu ambacho najuta,”alisema staa huyo. “Nisije nikasema sana mwisho nikalia hapa bure,” alisisitiza.

Amesema mke wake huyo kwa sasa aliolewa japo wana mawasiliano mazuri sababu ya mtoto wao. Kuhusu kama anajuta kuachana na Lady Jaydee, Gardner alisema: Siwezi kusema najuta kwamba alitokea kwenye maisha yangu na siwezi kusema kwamba najuta tuliachana. Lakini ninachoweza kusema tu kwamba kwa suala la Jaydee ni suala ambalo nilichagua sana lisiwe ni jambo ambalo nalizungumzia au kulitolea comment kwasababu yule ni public figure unaposema kitu kuhusu yeye tafsiri zinakuwa ni tofauti na vile unavyotarajia.”

“Kwahiyo sina majuto yoyote, na sina aina yoyote ya chuki au uadui na nategemea hata yeye atakuwa anafeel the same,” alisisitiza.

Alidai kuwa yeye na Lady Jaydee hawana mawasiliano ya aina yoyote kwa sasa na mara ya mwisho walikutana kipindi wanakamilisha taratibu za talaka.

Kwa upande mwingine Gardner amedai kuwa maisha aliyonayo sasa ni ya furaha tele. Mtangazaji huyo amejiunga tena na Clouds FM akitokea EFM.

Daah!

TANGA, Kunani paler eh, Mbona Captain anasikitikaa?!

TANGA, Kunani palee eh, Mbona Jide ana ndi ndi ndi...!

Wakuu, Usiombe shetani ajue password yako, Utajuuuuta!!
 
Back
Top Bottom