Gari gani poa ya ''kifamilia?''

Gari gani poa ya ''kifamilia?''

Showroom haizidi 12m kwa sasa but kwa kumvua mtu mil9 mpk 8 unapata, dada angu analo hilo gari so nimeliendesha sana aliliagiza cost ilifika 14m mpaka tunaendesha kitaani mwaka 2014.
Mafuta inanusa baba Kilimo, engine ni vvt-i so unapiga misele vya kutosha 13kms per litre na hata taa ikiwaka still una uwezo wa kuchapa mwendo mpk ukafika unapotaka pasipo gari kuzima huwa ina reserve ya 4ltrs baada ya taa kuwaka. Its a very economical car jamaa angu na kana nafasi ya kutosha ndani with 3rd row seats unaweza kuwaweka watoto wako ama ukazikunja kuongeza compartment ya kueka mizigo.
 
  • Thanks
Reactions: MC7

Thanx.
 
Mkuu hayo yote magari yaliyotanjwa hakuna hata moja family car mkuu. Gari ya family na ambayo inaimili halisi ya barabara za kwetu na spears zake zinapatikana kwa urais na pia ni rais sana kuliuza kama umechoka kulitumia .lipo sokoni sana mkuu ni Toyota Noah model 1999.hii car sisi macardeal tunaiita roho ya paka ni gari ngumu sana na hata mafuta inatumia vizuri sana
Ushauri Mzuri Sana, Hutojuta Kununua Noah Old Model SR 40, Jitahidi Lisiwe 4WD
 
Wakuu,Labda mie ndio ninatatizo la kutokupenda gari za chini.
Gari za chini Dar kwenye Foleni zinatesa sana kwa joto,hasa ukiwa katikati halafu huku kuna Scania na upande wa pili Scania lazima uwive kwa joto,inabdidi utumie AC sana
Mie nakushauri nunua Noah old model ni nzuri sana kwa Familia pia.

Ushauri wa ziada ni kwamba baada ya kupata maelezo humu,jaribu kwenda na fundi mzoefu wakati wa kununua,kuna vitu vya zaida vya kitaalam atakushauri,maana kwenye Show rooms pale kuna watu wanauzoefu wa magari na wanajua sana kuimbisha hasa wakikuona huna Ideas nzuri za magari,unaweza wewe kwenda na wazo la Cc tu kichwani kishaukapewa gari yenye cc kama hizo lakini vitu vingine ni vya kitaalam zaidi kwa fundi kuweza kujua kwa uimara wa gari na ustahimilivu wake.
kweli mkuu noah old model nzuri sana...isitoshe ukiishiwa unakula vichwa vya buku buku from job to home unapata pesa ya mafuta
 
Passo haina Mvuto jamani..... uwwwiiiii!!!
Hahaha,aisee kweli,Passo na Vitz Old Model,Spacio Old model,Raum yaani vimekaa kama komba au vicheche(Samahanini wenye kumiliki gari hizi),ila havina mvuto yaani bora Probox mara mia.
 
Wakuu wajuzi wa JF,

Naombeni mnishauri mimi na wadau wengine watajifunzia hapa. Mwaka jani niliagiza Chaser GX 100,C.C 2300 ya kuanzia maisha,kiukweli nilikurupuka sana wadau.

Wese lilikuwa linachuruzika balaa,sometimes nalazimika kupaki! Sasa naja kwenu kwa unyenyekevu kijana wenu mnipe ushauri ni gari gani poa ya kifamilia inayofaa,in terms of spare parts na fuel consumption.

Nina bajeti ya Shs.8,000,000!

Asanteni wadau
Sio kwel, hakuna GX100-, ya cc 2300
 
Mkuu samahani,nimejaribu kuingia Befoward na kufanya bargaining,wasiwasi wangu gani itakuja nzima,mwenye experience please
wataalam wanasema Si ina advantage zaidi kuliko Ti kwakuwa body size ratio ya si ni sawa na power yake ukilinganisha ti body size ratio na weight ni kubwa kuliko power yake. hivyo fuel consumption ya si na ti ni kama sawa tuu japo si ni cc1790 .pia zinatumia tecnolojia ya learn burn inayopunguza fuel consumption hasa katika speed ndogo mafuta kidogo na gari inakuwa na power ya kwenda. Tumezoea sana kuangalia cc lakini nafikiri other tecnical stuff lazima zifikiriwe.
 
Kama familia kubwa nunua toyota wish cc 1800 vvti engine. Mm kwa sasa nimeagiza corolla axio 1500cc CVT engine hizo za 4AT nimezipa kisogo kwanza. Tatizo wabongo na cc hatutak kujaribu mambo mapya kila cku kuigana tu
Samahani kiongozi. Hivi vvti engine na vct engine maana yake nini?
 
Samahani kiongozi. Hivi vvti engine na vct engine maana yake nini?
VVT-i, is the Variable Valve Timing with intelligence (valve zilizoboreshwa ili kufanya kazi kwa ufanisi na kula mafuta kidogo) na CVT ni continuously variable transmission- is an automatic transmission that can change seamlessly through a continuous range of effective gear ratios (kwa maana yenyewe haina gear option kwa mfano, hizi gari za engine automatic nyingi zinakuwa na gia nne mfano passo, vitz zinakuwa na 4AT, lakini engine ya CVT haina option ya gia yenyewe inatiririka tu ndo mana wakati wa kuendesha hutosikia gari ikibadili muungurumo kwa kubadili gear.)
 
Kwa kuongeza hizo CVT lakini pia ni VVT-i
 
Kwanza hakuna Noah SR40 ambayo ni 4WD, pia utuambie ubaya wa Noah SR50-4WD ni nini???
Nilishalitolea Ufafanuzi, Nikamwambia Akiona SR50 Aliogope Maana Ni 4wd, Pia Nilimwambia Zinakula Mafuta Zaidi Na Diff Zake Zinasumbua Na Mafundi Wetu Bado Wanapatashida Kuzikarabati
 
Back
Top Bottom