Mimi nimeshawahi kukatisha, treni ikiwa karibu sana, na gari haikuzima.
Ilikua Buguruni kwa mnyamani, kuelekea barakuda, ilikua siku yangu ya kwanza kupita barabara ile, mbaya zaidi, wafanya biashara wamesongomana, kiasi kwamba huwezi kuona leri kwa mbali.
Hivyo nilipokaribia nilimkuta yule mwenye kitambaa, hakaninyooshea kitambaa chekundu juu, ishara ya Simama ikiwa karibu kabisa na leri, ila kama kuna treni Sikuweza kuiona, kutokana na kuzibwa na mabanda ya biashara.
Sasa kosa alilofanya yule mwenye kitambaa alishusha kile kitambaa kwa kukata mithiri ya wafanyavyo marefa wasaidizi alafu akasegea pembeni huku akiongea na Simu.
Nikajua ameniruhusu, naingia tu kwenye leri ndiyo naiona treni mita 50 toka nilipo.
Wakati nakatiza nikasikia mayowe ya wa mama wanauza samaki na bidhaa zingine kulia kwangu kufuata njia leri, kwakua nilivuka salama sikusimama.
Ila pale ni hatari sana pamebanana sana tren haionekani haraka kwa mwenye gari.