HALI YA KISIASA MKOANI SONGWE
SONGWE : Haya inaonekana ndani ya Songwe, makada wa CCM viongozi wake wateuliwa na wabunge wa CCM pia wa migogoro sana huko SONGWE
23 April 2021
Mbunge Jimbo la Songwe Amtuhumu DC kupanga njama za kumuua kwa Risasi
Tuhuma nzito katika kikao Samuel Jeremiah DC wa Songwe atuhumiwa mbele ya RC. Mbunge wa CCM anaogopa kuingia ofisi ya DC. Mivutano imefika mpaka ktk vikao vya RCC . Mbunge Philipo agusia ya DC kutumia utawala wa mabavu n.k mfano kubomoa nyumba za wananchi barabara zijengwe. Mkuu wa mkoa aingilia apanga kuwasuluhisha DC wa Songwe Samuel Jeremiah na mbunge wa Songwe ili suala hili zito lipate ufumbuzi..
Source : Haroub TV
Madai ya mbunge Mulugo kutishiwa maisha na mkuu wa wilaya yatua polisi
Saturday April 24 2021
By Elias Msuya
More by this Author
IN SUMMARY
- Mbunge wa Songwe (CCM), Philip Mulugo amedai kutishiwa maisha na mkuu wa Wilaya ya Songwe, Samuel Jeremiah akimtaka mkuu wa Mkoa huo, Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela kuingilia kati.
Advertisement
Dar es Salaam. Mbunge wa Songwe (CCM), Philip Mulugo amedai kutishiwa maisha na mkuu wa Wilaya ya Songwe, Samuel Jeremiah akimtaka mkuu wa Mkoa huo, Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela kuingilia kati.
Mulugo alitoa malalamiko hayo Alhamisi Aprili 22, 2021 kwenye mkutano wa CCM uliofanyika mkoani humo, akimlalamikia pia Jeremiah kudharau viongozi wa chama tawala na Serikali.
Leo Jumamosi Aprili 24, 2021 Jeremiah alipoulizwa kwa njia ya simu na Mwananchi Digital kuhusu tuhuma hizo, ametaka waulizwe polisi kwa kuwa ndio wanashughulikia madai hayo.
“Hayo mambo ya kutishiana maisha ni ya kipolisi ndio wanaoshughulikia, siwezi kuyazungumzia. Wao ndiyo wanaoshughulikia usalama wa raia,” amesema Jeremiah akibainisha kuwa hata madai ya CCM hawezi kuyazungumzia.
Wakati Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, George Kyando akiieleza Mwananchi Digital leo kuwa tuhuma za Mulugo hazijaripotiwa polisi, Brigedia Jenerali Mwangela amesema madai hayo yameshafikishwa polisi na yanachunguzwa.
“Hizo tuhuma amezitoa hapo, kabla ya hapo zilikuwa hazijaripotiwa. Tofauti kati ya Mulugo na Jeremiah ni matatizo tuliyokuwa tunayamaliza ndani. Tulishasuluhisha chama Mkoa, mimi kama mkuu wa Mkoa nilishasuluhisha yanaonekana yamekwisha. Lakini yametokea tena tumefanya kikao cha ndani na suala hilo sasa liko Polisi linasuluhishwa,” amesema Mwangela.
Madai ya Mulugo
Akizungumza katika mkutamo huo wa juzi, Mulugo amedai tofauti na kazi ambayo mkuu huyo wa wilaya ametumwa wilayani hapo, haonyeshi ushirikiano,
“Huyu kaka yangu Jeremiah ameteuliwa na rais kuja kutuongoza sisi lakini alipokutuma kuja kutuongoza sisi hutakiwi kutumia mabavu wala bunduki,” amedai Mulugo.
Huku akidai kuwa mkuu huyo wa wilaya hashirikiani na viongozi wa CCM na Serikali amesema, “mkuu wa Mkoa naomba na wewe nikuseme kidogo, inawezekana wewe ndio unayasababisha haya kwa sababu mkuu wa wilaya anayofanya unayajua. Na huwa unatuambia kwenye simu na kwenye RCC (mikutano ya halmashauri).”
Advertisement
Mulugo amesema mwaka 2020 Mwangela alimuita pamoja na viongozi wa CCM na Jeremia na kuwasema kuhusu kubomoa nyumba ili kupanua barabara.
“Ulituita na ukamwonya mkuu wa wilaya aache hiyo tabia ashirikiane na viongozi wenzake wilayani, lakini mpaka leo amenifungia mlango. Kama nilivyosema siwezi kuingia ofisi ya mkuu wa wilaya mimi naogopa.”
“Kwa hiyo nataka ujue mambo mengi yaliopo Songwe. Viongozi wanaweza wasielewe mambo yanayoendelea Songwe. Mimi natafutwa na ninaweza kupigwa risasi wakati wowote,” amedai.
Madai ya CCM
Katibu wa CCM wilaya ya Songwe, Gerald Mwadalu amesema uhusiano kati ya mkuu huyo wa wilaya na viongozi wa CCM si mzuri na hata walipofanya juhudi za kumuita kutafuta suluhu imeshindikana.
“Baada ya utangulizi wa kamati ya siasa ya halmashauri kuu, tulipotoka kwenye uchaguzi tulimeguka. Tulitumia saa 12 kusuluhisha na watu walikuwa wanasimama tupigane.”
“Tukagundua kwamba madiwani hawa wana neno na mkuu wa wilaya kwa kusema, tukakubaliana kwenye kamati kwamba tuwaite madiwani, tumwite mkuu wa wilaya tukutane naye tuone hitilafu ya hawa dhidi ya kiongozi wao. Bahati mbaya sana akatuomba ruhusa akasema ameitwa na mkuu wa Mkoa. Tukamwambia atutajie tarehe ya kukutana, akatutajia tarehe lakini hakupatikana,” amesema Mwadalu
Source :
Madai ya mbunge Mulugo kutishiwa maisha na mkuu wa wilaya yatua polisi | Mwananchi
23 Juni 2021
DC SIMALENGA Akikabidhiwa Ofisi na AliyeKuwa Mkuu wa Wilaya SONGWE Samwel Jeremiah Atema Cheche
Source: Jay TV Songwe
15 May 2021
Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela astaafu
https://www.mwananchi.co.tz › ...
Rais Samia apangua wakuu wa mikoa, ateua wapya - Mwananchi
15 May 2021 — Omary Mgumba ameteuliwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Songwe akichukua nafasi ya Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela aliyestaafu