Gari ulinunua milioni 10.5 mwaka 2020 halafu leo unataka kuliuza milioni 13.5?

Gari ulinunua milioni 10.5 mwaka 2020 halafu leo unataka kuliuza milioni 13.5?

Championship

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2019
Posts
5,500
Reaction score
10,616
Hivi Watanzania mna matatizo gani? Mnafahamu maana ya depreciation? Gari gani inaongezeka thamani baada ya kutumika?

Hivi mnajua hayo magari mnanunua kutoka Japan kwa Usd 3,500 yalipotoka yaliuzwa Usd 100,000 miaka 10 iliyopita?

Nashangaa kuona gari ina namba DSQ ambayo ilitoka January na February 2020 leo mtu anaiuza kwa bei kubwa kuliko aliyonunulia.
 
Mambugila ni wengi.

Tanzania hakuna consumer literacy tunajinunuliaga tuu vikitupendeza.

Ukitaka kuuua kabisa biashara ya shobo(udalali) weka jukwaa la elimu kwa watumiaji, kwisha habari yao. Maana tunaamini kwenye kupiganisha.

Ndio kazi za mawinga pale Kariakoo, Wapiga debe pale Mbezi, Madalali wa nyumba nk.. wanajipa umuhimu wasiokuwa nao. Na wanataka kujenge industry kwenye uongo uongo.

Kwa kifupi nataka kusema hivi usishangae atauza tuu ...maana kama nilivyoanza mambugila bado tuko wengi.
 
Demand and Supply kaka, mfano ukizingumzia magari kama toyota crown na nyinginezo gharama yake sokoni imepanda zaidi ilikuwa ni around 10m ila kwa sasa hupati kwa hiyo 10m aliyonunua miaka mitatu iliyopita
 
Nakupa sababu kubwa, mwaka 2010 Toyota IST ilikuwa inauzwa around 12m. Fast forward 2023 hiyo IST inauzwa 17m, kuna ongezeko la 5m hapo. Sasa unataka huyo aliyenunua 12m 2020 aiuze 7m? No way!!
Sasa hilo ongezeko linamhusu nini yeye? Mtu alinunua gari ikiwa na km elfu 75, leo kuna km laki na sitini halafu bei ipande kwasababu gani? Hiyo 7m ni halali kabisa.
 
Back
Top Bottom