Gari ulinunua milioni 10.5 mwaka 2020 halafu leo unataka kuliuza milioni 13.5?

Gari ulinunua milioni 10.5 mwaka 2020 halafu leo unataka kuliuza milioni 13.5?

Hayo yatabaki kua maumivu yako binafsi mkuu, sisi usitutoe kwenye reli kabisa.kesho nimwaka mpya nawatu washaanza kuweka status picha ya pombe kali. Apo ushanielewa.
 
Sasa hilo ongezeko linamhusu nini yeye? Mtu alinunua gari ikiwa na km elfu 75, leo kuna km laki na sitini halafu bei ipande kwasababu gani? Hiyo 7m ni halali kabisa.
Kumekuwa na inflation ya bei mkuu, ndani ya miaka motatu bei za magari zimepanda so usitegemee bei za mkononi kubakia kama zamani.
 
Watanzania wengi hatuna elimu ya biashara basically. Kwa mfano eneo hili la kuuziana magari wengi huwa wanachoangalia ni anapata faida kwa kuuza gari alilotumia.

Huwa tunawaona other nationals kama Indians, wachina, waarabu, wazungu na kadhalika, wanapookuwa wanauza mali zao kwa bei ya chini tunawaona kama mafala ile hali wanakwenda na kanuni za uchakavu (depreciation) ili kusiwe na ulanguzi.

Unakuta mtu amenunua gari miaka 10 iliyopita halafu anataka kuuza bei sawa au pungufu ya milioni 1 ya bei aliyonunulia yeye hapo anajitoa ufahamu kuhusu uchakavu na gharama ya matengenezo atakayoingia huyu mnunuzi mpya kuifanyia service kubwa ili iwe imara kwa matumizi zaidi.

Hii elimu inabidi itolewe ili kuepusha ulanguzi huu wa kuuza mali chakavu kwa bei ya juu na kudisregard issue ya uchakavu na bei.
 
Hivi Watanzania mna matatizo gani? Mnafahamu maana ya depreciation? Gari gani inaongezeka thamani baada ya kutumika?

Hivi mnajua hayo magari mnanunua kutoka Japan kwa Usd 3,500 yalipotoka yaliuzwa Usd 100,000 miaka 10 iliyopita?

Nashangaa kuona gari ina namba DSQ ambayo ilitoka January na February 2020 leo mtu anaiuza kwa bei kubwa kuliko aliyonunulia.
Lakini ni biashara huria. Wewe usinunue kwake, acha ahangaike na mkweche wake, kama kweli ni overpriced kiasi hicho, hatapata mteja.
 
Nakupa sababu kubwa, mwaka 2010 Toyota IST ilikuwa inauzwa around 12m. Fast forward 2023 hiyo IST inauzwa 17m, kuna ongezeko la 5m hapo. Sasa unataka huyo aliyenunua 12m 2020 aiuze 7m? No way!!
Mmmmmmhmn IST imeanza kuuzwa bei ya milioni 12 miaka hiyo kweli? Maana nakumbuka kama IST kipindi zinaanza ingia bei ya juu ilikuwa ni milioni 6 hadi 7. Baada ya uber kuingia ndio shida ikaanza zikaanza kuuzwa kuanzia kati ya milioni 8 hadi 12 kwa IST kali sana.
 
Watanzania wengi hatuna elimu ya biashara basically. Kwa mfano eneo hili la kuuziana magari wengi huwa wanachoangalia ni anapata faida kwa kuuza gari alilotumia.

Huwa tunawaona other nationals kama Indians, wachina, waarabu, wazungu na kadhalika, wanapookuwa wanauza mali zao kwa bei ya chini tunawaona kama mafala ile hali wanakwenda na kanuni za uchakavu (depreciation) ili kusiwe na ulanguzi.

Unakuta mtu amenunua gari miaka 10 iliyopita halafu anataka kuuza bei sawa au pungufu ya milioni 1 ya bei aliyonunulia yeye hapo anajitoa ufahamu kuhusu uchakavu na gharama ya matengenezo atakayoingia huyu mnunuzi mpya kuifanyia service kubwa ili iwe imara kwa matumizi zaidi.

Hii elimu inabidi itolewe ili kuepusha ulanguzi huu wa kuuza mali chakavu kwa bei ya juu na kudisregard issue ya uchakavu na bei.
Sasa alienunua Brevis miaka nitatu iliyopita na Alienunua Premio zote leo zinamuonekano mzurii nani Atauza kwa bei ya hasara????

Sio suala la tamaa ila Soko ndo linaamua bei na thamani ya kituu unaweza nunua bei ndogo soko likikubali japo ushatumia ukauza bei kubwa.. Soko likigoma hata nusu bei huwezi uza.
 
Mmmmmmhmn IST imeanza kuuzwa bei ya milioni 12 miaka hiyo kweli? Maana nakumbuka kama IST kipindi zinaanza ingia bei ya juu ilikuwa ni milioni 6 hadi 7. Baada ya uber kuingia ndio shida ikaanza zikaanza kuuzwa kuanzia kati ya milioni 8 hadi 12 kwa IST kali sana.
I meant 2020 mkuu!
 
Lakini ni biashara huria. Wewe usinunue kwake, acha ahangaike na mkweche wake, kama kweli ni overpriced kiasi hicho, hatapata mteja.
Usiseme biashara huria bana. Huria haimaanishi bila kuzingatia sheria na kanuni za kibiashara ambazo zinazunguka huo uhuria wenyewe.

Usiishi kimazoea. Ni sawa na mtu anapokwambia karibu nyumbani kwake halafu akakwambia jisikie upo kwako, haimaanishi sasa umshike tako mkewe, na kutumia kitanda chake bali anamaanisha jiachie ila ndani ya mipaka ya mgeni mwenyeji na sio kujiona mwenye nyumba.

Sasa wewe kwasababu biashara ni huria ndipo wewe unaamua kuingiza utapeli na ulaghai ndani yake?

Kwani wewe mwenyewe utafurahia kuuziwa kitu kilanguzi, hauoni tunapotezeana muda kwanza kwa kujibizana, kuviziana, na tunapoteza pesa na fursa za kufanya biashara?

Ndio maana wahindi wanatoboa sana sababu hawazipi longolongo biashara zao.

Unakuta anauza IST milioni 7 au 6 net no stories na ipo vema haina vipengele, mtu anapesa yake analipia paap.

Sasa wabongo bwana dah [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hivi Watanzania mna matatizo gani? Mnafahamu maana ya depreciation? Gari gani inaongezeka thamani baada ya kutumika?

Hivi mnajua hayo magari mnanunua kutoka Japan kwa Usd 3,500 yalipotoka yaliuzwa Usd 100,000 miaka 10 iliyopita?

Nashangaa kuona gari ina namba DSQ ambayo ilitoka January na February 2020 leo mtu anaiuza kwa bei kubwa kuliko aliyonunulia.
Gari gan dada?
 
Mwaka 2021 nliagiza IST ya mwaka 2006 kwa 11m....mwaka huu mwezi wa 3 nikauza 13.5m.... Kwann haiku depreciate kwa sababu sasa hiv ist zimepanda sana ist ya mwaka 2006 unaipata kwa 17m-20m
 
Ukizungumzia depreciation angalia na thamani ya pesa unayozungumzia. TZS inashuka kwa kasi, ukiweka depreciation muuzaji anakua amepata hasara Mara mbili. USD 5000 za 2018 kwa TZS sio sawa na USD 5000 za 2023.

Lakini pia, ithaminishe hyo Gari kwa USD kutoka mwaka alionunua, utagundua Kuna depreciation ndani yake. Pesa imeshuka thamani.
 
Nakupa sababu kubwa, mwaka 2020 Toyota IST ilikuwa inauzwa around 12m. Fast forward 2023 hiyo IST inauzwa 17m, kuna ongezeko la 5m hapo. Sasa unataka huyo aliyenunua 12m 2020 aiuze 7m? No way!!
Kama kutoka mwaka 2020 hadi 2023 lililikuwa tu yard na halitumiki hata kidogo, nakuunga mkono
 
Back
Top Bottom