Gari ulinunua milioni 10.5 mwaka 2020 halafu leo unataka kuliuza milioni 13.5?

Magari mengi haya tunanunua used pale Japan bei zake zilikuwa usd 70,000 mpaka 110,000 wakati yanatoka mara ya kwanza kule.

Yanapo depreciate ndio wanayauza kwa hizo bei chee huku Africa.
Watu hawafahamu, hawajiulizi kwanini 75% ya magari binafsi hununuliwa used?

Serikali au makampuni ndiyo wenye uwezo kununua unused cars (0 km) kwa oder maalum toka viwandani.

Mbongo gani akiambiwa IST (0 km) = M 60 atatoa Tshs?

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Nnje ya mada, Madalali huwa wana maendeleo kabisa kwa kazi zao au nao hawatofautiani na Wavuvi, wauza mikaa?

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Mkristo wa hovyo kabisa wewe. Ndo maana huko upande wa wapalestina.
Hapana niko upande wako sema tu umenipa mgongo ndio maana hunioni. Ila unanihisi najua ndio maana kutwa kunikumbuka
 
Nakupa sababu kubwa, mwaka 2020 Toyota IST ilikuwa inauzwa around 12m. Fast forward 2023 hiyo IST inauzwa 17m, kuna ongezeko la 5m hapo. Sasa unataka huyo aliyenunua 12m 2020 aiuze 7m? No way!!
Bongo matapeli wengi sana, Rafiki yangu alikuwa na Toyota Corolla tripu 1 mtaani tripu 1 gereji au kapaki home hadi apate hela alipeleke kwa Fundi, hatimaye aliamua kulifanyia renovation alimpata mnyonge kwa 9 M.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Bro, hiyo meza unayotingisha ina vinywaji vya bei ghali
 
ni uzwazwa sana kuleta thread kama hiii!

Acha kukariri kuwa gari ikinunuliwa indepreciate tu....! Gari unaweza kuiongezea thamani pia

nikupe mfano mmoja,
Mimi nimenunua gari mil 10, mwaka jana then baada ya kuja:
1- nimelikatia bima kubwa
2- nimefunga music system mkubwa
3-nimeongezea system ya gasi
4-nimeweka sports ream

Kama hufahamu magari utaishia kulalamika hap unayolalamika
 
Kodi zipo juu sana ndio maana tumebaki kuumizana humu humu na magari mabovu. Ki ukweli Mwigulu Waziri wa fedha ameshafeli.Na mwendazake pia

Ukiagiza ist ya mwaka 2010 kodi mil.9.3 gharama za gari,ukaguzi na usafirishaji milion9.1 Hapo Bado handling charge,agency fee,storage, clearing agent,n.k


Soon nchi yetu itakuwa Ina oldest car fleet kama Ulaya mashariki Cuba,Iran.....MTAANI model za magari zote ni zile za kizamani (Average miaka 19) kutokatana na mikodi iliyopitiliza
 
Reactions: Tsh
Hapa ndipo lilipo tatizo. Watanzania hawawezi miliki magari mapya na chakavu hawawezi.

Imagine Ist ingekuwa m8 mpaka unaishika mkononi nani angenunua ist namba DA mbovu m13 ya mkononi?
 
Kama kuna watu wananunua gari iliyouzwa miaka mitano nyuma kwa bei zaidi ya ile ya miaka mitano nyuma, basi ccm atatawala milele.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…