Gari wanazohitaji waTanzania hazipatikani dunia nzima

Gari wanazohitaji waTanzania hazipatikani dunia nzima

Lexus ni Lexus na Toyota ni Toyota.

Hayo ni makampuni mawili tofauti na yana objective tofauti.

Ongelea bidhaa za Toyota na sio za Lexus.
Km ndivyo kuna hebu zungumza kuhusu Lexus na Harrier, hamna uhusiano
 
Km ndivyo kuna hebu zungumza kuhusu Lexus na Harrier, hamna uhusiano
1612791361096.png
 
Toyota wanatengeneza models tofauti kwa masoko tofauti ndio maana kuna salon zipo Japan lakini haziko UK wala USA,pia kuna trucks zipo USA lakini haziko nchi nyingine. Hii sio kwa Toyota hata car makers wengine pia wanafanya kama Toyota.
Hiyo ni michezo ya Toyota na Nissan tu. Unaweza kunitofautishia BMW 5 series iliyouzwa Bongo na iliyouzwa US ina utifauti gani?
 
Kuna majini, hizi zinazoletwa kwetu ni rafiki kabisa kwa mazingira yetu. Tulivyowapenda mitelezo BREVIS nae kaingizwa kwenye kundi la majini 😆 😆 😆 😆
Brevis kaingizwa kwenye list 😅 😅 😅
 
Wazungu wameshatengeneza gari zinachomoka kuliko hiyo skyline. Au unaposema "wanaitamani" unamaanisha nini?

Naipenda Nissan GTR Nismo.

Ndo gari pekee Japan naimezea mate.
Mkuu nawakubali wajerumani lakini Nismo nikiiona nasema "Shikamoo mjapan" ile mashine wazungu ulaya na amerika huwaelezi kitu wana jina lao wanaiita Godzilla 😅
 
Nataman siku moja nidrive ford ranger-wildtrak pickup. Nikiiona hiyo gari huwa nahis kufa ganz.

Jamaa mmoja anadai mafuta yake kwa mwezi eti labda nifungue kituo changu cha mafuta.
 
Nataman siku moja nidrive ford ranger-wildtrak pickup. Nikiiona hiyo gari huwa nahis kufa ganz.

Jamaa mmoja anadai mafuta yake kwa mwezi eti labda nifungue kituo changu cha mafuta.
Sio kweli.

Mzigo ni diesel.

Tank lake lina 80 liters. Unaweza toka Dar mpaka Arusha ukarudi Same kwa udereva ulio decent.

Au unaweza toka Dar mpaka Makambako bila shida kwasababu ya milima.

Ila ni gari ya kawaida sana kwa ndani, haina ile wooooow ukiwa unaendesha.

Nimeshaendesha mara 2 safari ndefu, halija-niimpress kama nilivyotarajia.

Labda muonekano wa nje ndo unakutia wazimu.
 
Kibongo bongo hiki kidude huwa kipo underrated sana, lakini shughuli yake field huwa ni 🔥🔥🔥🔥
1612888599227.png
 
Hiki kidude kinakimbia asikwambie mtu.

Ukiwa na hizi toyotaz, hesabu hiki kidude kukusumbua sana njiani.
Kapo vizuri sana, ukitaka urembo field za kukimbilia ndio hizo Ford rangers, Hilux revo. Kwa kazi dondoka hapo kwa Nissan NP300 kila kitu ni full manual mpaka 4WD yake.
 
Mtanzania anahitaji gari moja yenye sifa zifuatazo.

1-isiwe inakula mafuta, ikiwa inakula mafuta utasikia (jini hilo).
2-Gari ambayo ikiharibika vipuri vipatikane kwa bei nafuu.
3-Gari ambayo ina acceleartion kubwa na top speed kubwa mfano 220km/hr....300km/hr
4-Muonekano mzuri na imara.
5-Yenye gharama nafuu katika utengenezaji.
6-Iwe na uwezo wa kupita off-road.
7-Isiwe old model.
8-isiwe na mifumo na sensors nyingi za umeme (mfano bmw).

Na kinachonimaliza kabisa...

9-Iwe na bei nafuu.

Utabaki kuendesha ist na vitz mpaka unazeeka..

Ushauri kwa waTanzania wenzangu, tutabaki kuwapigia makofi na kuwasifia wanaume wenzetu wanaomiliki range rover na discovery,bmw x6,v8, benz n.k...
Huwezi hata siku moja kupata gari yenye hizo sifa zote thats why bara bara zimejaa ist, wish, crown, harrier n.k

Kumbuka unapokwenda kununua gari fahamu gari haitumii mtori wala uji, gari inatumia mafuta, brevis tu zimewashinda kila siku mnapiga kelele, mtamiliki gari gani nzuri yenye kasi, luxury, comforatable na speed kama mnakimbia majukumu?

Badilikeni ndugu zangu, acheni maisha ya kukariri, kwa East Africa naona sisi ndio tunamiliki gari za kishamba kuliko wote.

1200px-2018_BMW_X6_xDrive30d_M_Sport_Automatic_3.0_Front.jpg

2021-Tundra-1-copy.jpg

USC90JES052F021001.jpg
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119]
 
Back
Top Bottom