Gari ya kifahari GX V8 husafirisha kiti cha Rais

Gari ya kifahari GX V8 husafirisha kiti cha Rais

Gari ya kifahari aina ya GX V8 ndiyo husafirisha kiti cha Rais wa nchi popote aendapo.
Nadhani sasa tunaanza kuboa.

Mnataka rais akalie kigoda?

Tuna issues za njaa, inflation, high taxaction, social insecure and uongozi wa usioheshimu Katiba na Sheria
Mnajadili viti, magari, pisikali na kuchakatana

Sijui tumelogwa na nani walah
 
Ni Ujinga pia huko mikoani hakuna viti? Nyerere, Mkapa hakuwahi kuingia na Presidential Chair Makanisani
Presidential chair hadi mbinguni au. Mwenda alitarajia cheo huko, na kiti cha mkuu wa malaika.
 
She is a Head of State jamani kama hamtaki hizo gharama tafakarini nn kitatokea. Amepotea Magu mnataka tupoteze viongozi kwa makosa ya usalama?
Tunaweza kuvumilia gharama zinazohusiana na afya na usalama wa raisi hata ziweje. Kama kiti kipo kwa jinsi hiyo sawa. Unajua tozo na ufahari sijui kama vinaendana.
 
Upo sahihi kabisa mkuu, lakini hebu jaribu kuwaza 'kiafrika' ...

Kiti kwa namna yoyote kuna uwezekano kimewekewa ule utaalamu wetu...
Kwanini wasiuweke kwenye Ushungi ?!!!!

Huwa naghadhabika sana kuona our hard earned cash inatumika ndivyo sivyo.... Hata kama ni protokali its about time zibadilishwe
 
Gari ya kifahari aina ya GX V8 ndiyo husafirisha kiti cha Rais wa nchi popote aendapo.
Je!
Kwenye hiyo gari huwa kimejaa kiti peke yake bila watendaji wengine wa kiserikali wanaoambatana na msafara husika?

Je mleta mada Suzy Elias wewe ungependa kisafiri kwa usafiri wa fuso au pick up?

Je! Mleta mada ulitaka vichongwe viti vingi vya vyenye nembo ya Ikulu na kusambazwa wilaya zote nchini ili Rais awe akivikuta huko?

Je!
Kama Rais anatumia usafiri wa Land Cruiser V8 unadhani usafiri gani utumike kubeba kiti chake ili kiti pia kifike pale anapokwenda kwa wakati ili akikalie?

Baadhi yenu tukisema mnabomoka kisera mnabisha.....
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kwahiyo hiko kiti kinakua na dereva wake? Yani dereva anakiita kiti "boss". Hata safari ikiwa ndefu dereva anasimama njiani ili kiti kichimbe dawa [emoji848]
 
Je!
Kwenye hiyo gari huwa kimejaa kiti peke yake bila watendaji wengine wa kiserikali wanaoambatana na msafara husika?

Je mleta mada Suzy Elias wewe ungependa kisafiri kwa usafiri wa fuso au pick up?

Je! Mleta mada ulitaka vichongwe viti vingi vya vyenye nembo ya Ikulu na kusambazwa wilaya zote nchini ili Rais awe akivikuta huko?

Je!
Kama Rais anatumia usafiri wa Land Cruiser V8 unadhani usafiri gani utumike kubeba kiti chake ili kiti pia kifike pale anapokwenda kwa wakati ili akikalie?

Baadhi yenu tukisema mnabomoka kisera mnabisha.....
Kama kiti kina maana sana nadhani next time tuchague kiti tu na sio mtu....; Ingawa kuna watu wanatumia muda kuongelea non issues lakini wengine kama wewe nadhani mna-justify the unjustifiable...

Kwamba akikalia kitu ambacho hakina nembo anakuwa sio Rais ?!!!
 
Back
Top Bottom