Watanzania wengi ni matomaso, ukiwasimulia tu hivi hivi, hawaamini. Nashauri gari ya TAL isibadilishwe muonekano wake baada ya kupigwa risasi, matundu ya risasi yabaki, gari itengenezwe injini tu na sehemu muhimu, ila sehemu zenye matundu ya risasi zibaki.
Hii itafanya watu wakifika katika mikutano ya hadhara, kwanza wapate somo lwa kuliangalia gari, kisha watajikumbusha madhira ya awamu ya tano. Gari hiyo itembezwe mitaa yote ambako mikutano inatarajiwa kufanyika, wananchi wayaone matundu ya risasi, halafu waamue wenyewe kuhusu awamu ya tano, na walinganishe na awamu ya SSH ambayo Lissu anazurura huku na kule akimtukana kwa uzanzibari wake
Pili, Lissu asipande gari hilo, kwa kuwa tayari lomeshaingia nuksi, ni sawa na jeneza.