Gari yako ukiweka lita nane (mafuta ya 20,000) inatembea KM ngapi?

Gari yako ukiweka lita nane (mafuta ya 20,000) inatembea KM ngapi?

Hilo swali halija kamilika naona wengi mnakurupuka kasoro mmoja, nawasiwasi kamamnamiliki magari....au mnatumia za wazazi wenu au Ndugu...huwezi kujibu bila kujua mafuta ya diesel au petroli gari yenye engine cc 2500-3900 au hizi baby walkers cc 1200-1600. au ya mzigo fuso au trailer, Unaendeshea wapi rough road au rami.....ndo utajua Consumption ya gari lako
Kwa hiyo gari yenye cc 1200-1600 ni babywalker?
ARROGANCE at its best[emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Kwa wiki kwa wastani naendesha kama 400 km natumia just under $50 ~ Tsh 100,000. BMW X5 3 L

Hiyo sehemu kubwa ni misafara ya kwenda na kurudi kazini, ambayo naifikiria kuipinguza, japo kwa siku moja, kwa kufanya kazi kutoka nyumbani.

Hapo nimeweka na hesabu za weekend, kama vile ukitaka kwenda kuangalia sinema mpya kama ya Spike Lee ya sasa "BlackK Klansmann

CC Mshana Jr
 
Hilo swali halija kamilika naona wengi mnakurupuka kasoro mmoja, nawasiwasi kamamnamiliki magari....au mnatumia za wazazi wenu au Ndugu...huwezi kujibu bila kujua mafuta ya diesel au petroli gari yenye engine cc 2500-3900 au hizi baby walkers cc 1200-1600. au ya mzigo fuso au trailer, Unaendeshea wapi rough road au rami.....ndo utajua Consumption ya gari lako

Wewe sasa nahisi hauna gari bali ni fundi wa magari swali limekaa fupi na linaeleweka,

Mwenye kuleta uzi amezingatia gari yake bila kutaja cc wala aina ya fuel anayotumia ila amesema elfu 20 anatumia kwa hizo km alizotaja.

Hivyo kila mmoja bila kutaja aina ya gari anayotumia na cc kwa sababu kila mtu agari yake anaijua hivyo matumizi yake lazima ya fuel kwa mizunguko yake pia atakuwa anayajua.

Ila nimalizie kwa kusema mimi sina gari natumia baiskeli kila siku kwenye mizunguko yangu ya kila siku ya kuuza urembo.
 
Golf Touran ipo yenye 1.4L. Nayo ni babywalker? Hivi Xtrail nayo ni babywalker? Kitu kina almost 2L engine unaiita babywalker?
Mmmh!! kaka hivyo vigari vina engine capacity ndogo sana hapa tunaviita "babywalker" Japan vitaitwa "marginal economical vehicles" vya weekend shopping supermarket na vinamilikiwa na undergraduates (wanafunzi wa vyuoni) viingine haviruhisiwi kuingia katika major highways....ndo maana wanavi auctioniwa na kua damped in Africa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante kwa ushauri, ngoja nitafute nafasi nikafanye diagnosis.
Tena uwahi mkuu hizo gari consumption yake ni ndogo sana kama passo cheki wadau wa German car sio kila Garage utaongeza tatizo kuna mdau anaitwa 225jerry mcheki instagram atakusaidia akishindwa atakelekeza kwa wadau wengine wa German cars.
 
Mmmh!! kaka hivyo vigari vina engine capacity ndogo sana hapa tunaviita "babywalker" Japan vitaitwa "marginal economical vehicles" vya weekend shopping supermarket na vinamilikiwa na undergraduates (wanafunzi wa vyuoni) viingine haviruhisiwi kuingia katika major highways....ndo maana wanavi auctioniwa na kua damped in Africa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo babywalkers tu ndio zinakuwa auctioned na kuwa dumped in Africa? Hivi unajua hata UK wananunua used Japanese cars kutoka Japan?

Sent from my TA-1032 using Tapatalk
 
Kwa hiyo babywalkers tu ndio zinakuwa auctioned na kuwa dumped in Africa? Hivi unajua hata UK wananunua used Japanese cars kutoka Japan?

Sent from my TA-1032 using Tapatalk
Ni kweli lakini Mitumba ya magari ya Japani ya UK. na yaTz nitofouti sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa wiki kwa wastani naendesha kama 400 km natumia just under $50 ~ Tsh 100,000. BMW X5 3 L

Hiyo sehemu kubwa ni misafara ya kwenda na kurudi kazini, ambayo naifikiria kuipinguza, japo kwa siku moja, kwa kufanya kazi kutoka nyumbani.

Hapo nimeweka na hesabu za weekend, kama vile ukitaka kwenda kuangalia sinema mpya kama ya Spike Lee ya sasa "BlackK Klansmann

CC Mshana Jr
Mkuu japokuwa lina Engine kubwa lakini inaonekana linatumia vizuri fuel nimepiga hesabu hapo ukilinganisha na prado au land cruser bas utapata jibu bora hiyo X5 kuna haja ya kutokuziogopa hizi gari we unaonaje?
 
Mshana Jr alianzisha uzi mzima wa kuelezea hilo la kwamba watu wanaziogopa tu BMW lakini zina utumiaji mzuri sana wa mafuta.

Mimi niliponunua hata sikufikiria sana utumiaji wa mafuta, lakini kadiri ninavyozidi kulitumia na kuangalia utumiaji wa mafuta, naona watu wanaogopa haya magari mengine bure tu as far as utumiaji wa mafuta.

I don't think that's too bad for a 3.0 engine.

I still get my vroom on the highway, and a decent fuel economy to.
 
mleta mada kwa MPG hyo bila shaka engine ya gari yako itakuwa inarange 2.0 ltr -2.5 ltr....

na chengine huwezi linganisha consumption ya gari yako na nyingine bila kusema unatumia gari gani na engine gani?

kama hapo mm kwa uzoefu nimeweza kujua hyo gari itakuwa ipo kwenye 2.0 engine hadi 2.5 ltr engine kutokana na ulaji huo wa mafuta
Hebu nifundishe kutambua ulaji wa mafuta say engine 2990 na nyingine engine 1990
 
Hebu nifundishe kutambua ulaji wa mafuta say engine 2990 na nyingine engine 1990

kwenya engine ya gari kuna vitu vinaitwa pistons na hizi huwa zinabidi zifanye rotation ili kuzalisha power na hyo rotation hufanywa kwenye chumba kiitwacho cylinder ... ukubwa wa clylinder mara nyingi ndio utafanya nguvu iwe nyingi na since power inavyokuwa kubwa na ndio mafuta hutukima mengi zaidi... na ukubwa wa clynder hupimwa kwa cubic cm na ndio hizo CC

sasa hadi hapo utakuwa umeshaona kuwa cc1990 itakuwa ina cylinder room ndogo kuliko ile ya 2990 na hata combustion chamber ya cc 2990 itakuwa ni kubwa kuliko ya cc 1990

kwa hyo hii ya cc 1990 itahitaji fuel kidogo na oxygen kidogo kukamilisha mapigo ya piston kuliko itakavyohitaji yenye cc 2990

lakini kwa jinsi technologia ilivyoendelea car manufactures wameanza kutengeneza engines kubwa ila zinazokula mafuta vizuri tofauti na zamani.

lakini pia sio kila gari yenye cc nyingi itakuwa na consumption kuliko yenye cc ndogo... sometimes huwa tofauti kutokana na technologia iliyotumika kutengeneza hizo engines mbili.

ila kitu cha uhakika ni hiki the break horse power and torque produced by the engine itareflect fuel economy ya gari..

more power produced more fuel burned

naweza toa mfano kwa altezza

altezza yenye engine ya 1G-FSE 6 cylinder inaproduce horse power 162

altezza yenye engine ya 3S-GE 4 cylinder ina produce horse power 210

na hata mafuta yenye 3s-Ge inakula kuliko yenye 1G sababu ya power produced..

kwahyo siyo mda wote wingi wa clynder au ukubwa wa engines utareflect ipi inatumia mafuta mengi..

lakini kwa asilimia 85 engines kubwa zinakula mafuta kuliko engines ndogo

kuhusu kujua MPG za engine hizi huwa mara nyingi ni standard na hata zikipishana hazipishani sana yani cc 1990 ya toyota na cc 1990 ya mitsubish zikipishana basi ni kama km 2 tu na huwa kila engine manufacture anakuwa ameweka detail za fuel consumption online

kwa wajuzi zaidi mnaweza nisahihisha mahali nilipokosea ili tuweze kupeana ujuzi zaidi
 
Back
Top Bottom