Jamaa mdini sanaWewe ni mdini sana! Siwezi kukupa attention yoyote na acha kabisa kujificha nyuma ya tafiti uchwara hizo zilizojaa udini!
Yaani wewe ni mtu useless sana! siju kama wewe Mohamed Said ungekuwa ndo Dossa Azizi kina Julius Nyerere wangekunywa hata maji kwako!
Lakini kutoka na chuki ulizonazo ni dhahiri kuwa Maisha yako ni magumu sana!
Ndani yako kumejaa chuki sana hauwezi kuwa na mafanikio wewe !
You are useless and you deserve a useless life!
Mzee humu kuna watu hawako tayari kupokea maarifa. Unahangaika nao wengine wakati wanakokotoa vya kuandika wanagugo kwanza, ninakushauri wengine waache usiwajibu, hawa wenye maswali yenye tija na wanaokubali hoja kinzani wakaielew ndio tunaowataka hapa.
Wewe ni mdini sana! Siwezi kukupa attention yoyote na acha kabisa kujificha nyuma ya tafiti uchwara hizo zilizojaa udini!
Yaani wewe ni mtu useless sana! siju kama wewe Mohamed Said ungekuwa ndo Dossa Azizi kina Julius Nyerere wangekunywa hata maji kwako!
Lakini kutoka na chuki ulizonazo ni dhahiri kuwa Maisha yako ni magumu sana!
Ndani yako kumejaa chuki sana hauwezi kuwa na mafanikio wewe !
You are useless and you deserve a useless life!
Jones...Tunaomba utupe ushahidi usio na mashaka kwamba Huyo Kabaka aliubomoa kwa sababu zake binafsi (hasa chuki za kidini) na kukiuka taratibu zote za kimamlaka.
Haingii akili karne ya leo taasisi kubwa kama UDOM eti mtu avunje msikiti kisa tu ana chuki na waislam bila kujua ni madhara gani yanaweza kutokea katika jamii hasa msuguano wa kiimani.
Ndio maana tusema haya mambo yawekwe wazi ila hoja za kujificha ficha bila ushahidi usio tia shaka mnafanya watu waendelee Kuwaita 'lia lia' jambo ambalo halipendezi kwenye jamii ya watu waliostraabika.
Mrangi,Jamaa mdini sana
Ova
Mzee wangu,naona unacho kililia bado hujakifahamu,tatizo hulifahamuMrangi,
Mdini kwa kusema kweli kuwa tunalo tatizo nchini petu?
Au mdini yule anaeweka mikakati kuwadhoofisha wale ambao si wa imani yake?
Kwa nini unajibu wewe jambo ambalo hujashutumiwa wewe?
Serikali ndiyo ya kutoa majibu siyo wewe unaenufaika na hali hii.
Mbona wahusika walipopewa ushahidi waliotaka wakapewa kupitia kitabu cha Prof. Njozi wakakiiga marufuku kuwa kosa la jinai kukutwa na kitabu cha Mwembecha Killings...?
Ukweli uliwatisha.
Hawakuwa na majibu.
Inawezekana pengine haya huyajui.
Ati jamaa mdini sana.
Sasa kama wao walikuwa wanaweza kwanini walikuwa hawajaenda kuutafuta Uhuru huko mpaka Nyerere alipokuja? Wao walilidhika na bakora Nyerere ndiye akawashituaHuwa unatengeneza picha mbaya sana ya Nyerere kama mtu aliyesaidiwa sana na waislamu alipokuja Dar es Salaam. Kumbuka kuwa Nyerere alikuja Dar es Salaama siyo kama ombaomba, bali alikuja akiwa na digrii ya M.A kama mwalimu wa St Francis College. Kabla ya hapo alikuwa ameshafundisha St Mary's College huko Tabora (kwetu mimi na wewe); miaka hiyo ualimu ulikuwa ni kazi yenye hadhi sana. Asingejihusisha na siasa, Nyerere alikuwa ni mtu wa kuishi maisha mazuri tu wakati huo.
Mara zote unasema iwapo "wazee wetu" wa Dar es Salaama wasingemsaidia Nyerere lakini ulishasema wewe ni mtu wa Tabora, kwa hiyo uhusiano wako na watu wa dar es salaama ni dini zenu tu, na hapo ndipo tatizo lako lilipo.
Tangawizi,Sikio la kufa halisikii dawa
Ova
Ulweso,Sasa kama wao walikuwa wanaweza kwanini walikuwa hawajaenda kuutafuta Uhuru huko mpaka Nyerere alipokuja? Wao walilidhika na bakora Nyerere ndiye akawashitua
Kwa hiyo?!Ulweso,
Baada ya Dr. Kyaruzi na Abdul Sykes kuchukua uongozi wa TAA mwaka wa 1950 ikaanza mipango ya kuuunda TANU na kwenda UNO.
Tatizo lililokuwa linaikabili TAA ni kupata kiongozi atakaengoza harakati za uhuru baada ya kuubda TANU na mtu huyo asiwe Mswahili.
Hakutakiwa Mswahili kwa kuwa hofu ilikuwa kuwaogopa Waingereza wasilete fitna kuwa chama cha TANU ni cha Waswahili na kwa fitna hiyo kuwataka Wengine na wao waazishe chama chao.
Abdul Sykes yeye chaguo lake lilikuwa Chief David Kidaha Makwaia lakini Hamza Mwapachu aimtaka Julius Nyerere.
Historia hii nimeieleza mara nyngi sana hapa.
Ndipo jina la Nyerere likapita katika kikao cha watu watatu nyumbani kwa Hamza Mwapachu, Nansio Ukerewe.
Walipitisha jina la Julius Nyerere walikuwa Hamza Mwapachu, Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika).
Wazee wenu na Nani.May Day,
Hivi unajua Nyerere kaja Dar es Salaam hana ndugu wala jamaa?
Unawajua waliompokea?
Unadhani endapo wazee wetu wamgekuwa wabaguzi wa dini au kabila Nyerere angefika hapo alipofika?
Wewe unaridhishwa na hii hali ya leo katika mgawanyo wa fursa 20:80?
Lombo,Mzee Mohamed Shikamoo!
Bila shaka umewahi kusoma kitabu Cha Abubakari Ulotu ..Historia ya TANU,Mimi nilikisoma nikiwa darasa la Saba !
Nasikikitika huwa nakitafuta kwenye maduka ya vitabu sikipati!
Nakumbuka Bwana Ulotu alibainisha harakati za Watanganyika wakati wa kuijenga TANU maeneo mbalimbali ya Taanganyika!
Sikumbuki Kama alieleza kuwa watu wa Pwani ,na kwa maaana yako wewe Waislam! walidhulumiwa baada ya Uhuru!
Wewe unakizungumziaje Kitabu hicho !?
Lombo,Kwa hiyo?!
Lombo,Mbona badhi ya hoja hujibu,hayo mengine umeshayasema na kuandika Sana!
Vipi unaonaj3 kitabu Cha Sheikh mw3nzio Ulotu Abubakar Ulotu, Historiaaya TANU nacho kimeandikwa na WAGALATIA!
Kwa maelezo yako kuhusu kitabu hiki ,ingawa nilikisoma nikiwa mdogo,Basi inadhihirisha akuwa wewe una amini kuwa TANU ilikiwa ni ya Wana Mzizima pekee...!Lombo,
Kitabu hiki nimekieleza katika kitabu cha Abdul Sykes:
''Kwa mara ya kwanza historia ya TANU ilitaka kuandikwa na Abdulwahid mwenyewe.
Baada ya kupatikana kwa uhuru mwaka 1961 na TANU ilipokuwa sasa inataka kujiimarisha kama chama cha umma, inasemekana Nyerere wakati ule Waziri Mkuu alimuomba Abdulwahid aandike historia ya harakati ya Waafrika wa Tanganyika dhidi ya ukoloni wa Waingereza.
Hii kwa hakika ndiyo historia ya TANU. Dr Wilbert Kleruu ambae ndiyo kwanza alikuwa ametoka masomoni Marekani alichaguliwa na TANU asaidiane na Abdulwahid katika utafiti na uandishi wa historia ile.
Abdulwahid alirudi kwenye ofisi za TANU makao makuu; kwenye ofisi yake ya zamani aliyokuwa akiitumia kama rais wa TAA.
Nyaraka zake binafsi,shajara zake na karatasi za baba yake nyingine kuanzia mwaka wa 1929 wakati wa enzi za African Association zililetwa pale kwa utafiti kama ushahidi wa yale yaliyopitika zama hizo.
Maelezo ya Abdulwahid katika kuanzishwa kwa Africa Association inasemekana hayakupendeza kwa baadhi ya watu, kwa kuwa mwanzo wa harakati dhidi ya ukoloni jina la baba yake Abdulwahid, Kleist Sykes, lilikuwa likitawala.
Halikadhalika ilipofika kueleza namna TAA ilivyokujabadilishwa kuwa TANU watoto wake wote watatu Abdulwahid, Ally na Abbas wakiongozwa na kaka yao mkubwa Abdulwahid halikadhalika likawa linatawala harakati zile.
Matatizo yakawa yanarundikana kila uchao.
Historia hii ikawa mtihani kwa Abdul Sykes na kwa Nyerere na kwa baadhi ya viongozi wa TANU.
Haukupita muda Abdulwahid akatambua kuwa viongozi wapya walioshika nafasi katika TANU kwa kweli hawakuwa na nia hasa ya kutafiti na kuandika historia ya Tanganyika ya kweli bali nia na azma yao ilikuwa kumfuta yeye na ukoo wake katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Abdulwahid alipong’amua hili haraka akajitoa katika mradi ule.
Hata hivyo Dr Kleruu aliendelea na utafiti na akaandika historia ya TANU. Historia hii iansemekana ilifuta mchango mzima wa akina Sykes katika kuunda TAA na baadae TANU.
Hata hivyo baada ya kazi hii kukamilika haikuchapishwa na ikabaki katika maktaba ya TANU, Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam.
Lakini baadae kazi ile ilitoweka na ikachapishwa baada ya ‘’mwandishi’’ kufanya mabadiko kadhaa katika mswada ule ili usitambulike chanzo chake.
TANU iligundua kuwa ile ilikuwa historia yao iliyoandikwa na Dr. Kleruu wakafanya bidii kuzuia isichapishwe.
Kimya kimya TANU ikafanya juhudi ya kuzuia kitabu hicho kisitoke toleo la pili.
Lakini hili halikuwezekana na kitabu hicho kimechapishwa sasa mara kadhaa.
Uandishi wa kitabu kile haukutofautiana sana na kitabu cha TANU kilichotoka mwaka 1981 kilichoandikwa na Chuo cha TANU cha Kivukoni.''
Katika mswada wa kitabu ha Abdul Sykes mhariri wa kitabu changu alikataa nisitumie neno, ''wizi,'' kuwa mswada uliibiwa Maktaba ya TANU akasema naweza kushatakiwa na mimi sina ushahidi kuwa Abubakar Ulotu aliiba ule mswada.
View attachment 1987785
Mohamed mimi nipo kinyume na dhuluma ya aina yeyote hasa ukandamizaji sawa halijatugusa ila tambua hata sisi tuna ndugu wa kiislam kwa namna moja kama nyingine linatugusa.Jones...
Sikulaumu kwa kusema hayo.
Kuna tatizo kuhusu Baraza la Mitihani na Shule za Kiislam.
Unajua yaliyofanyika?
Inashangaza.
Waislam waliamua kufanya maandamano dhidi ya Dr. Ndalichako.
Serikali iliiga marufuku maadamano yale lakini Waislam aliamua kuandamana bila kujali vitisho vilivyokuwapo nje ya Msikiti wa Kichangani.
Ndipo husema haya matatizo huwezi kuyajua kama hayakugusi yanawagusa wengine.
Lambo,Kwa maelezo yako kuhusu kitabu hiki ,ingawa nilikisoma nikiwa mdogo,Basi inadhihirisha akuwa wewe una amini kuwa TANU ilikiwa ni ya Wana Mzizima pekee...!
Katika kitabu kile Ulotu ameeleza jinsi Watanganyika walivoipambania TANU!
Nina mfano wa wapamabanaji hao kutoka Mkoa wa Singida ambbao nawajua ,wengine walikuwa Watumishi wa Serikali ya Kikoloni,Viongozi wa Kanisa,na Masheikh na hawa walimpokea Nyerere na wenzake walipokuwa wakieneza Injili ya TANU,Kama wazee wako walivompokea Nyyerere alipoacha Ualimu!
Hawa hakuimbwa Sana lakini Historia imeandikwa,nafikiri Kama ambavyo imewatambua wazee wako...labda ulitaka wote wapewe madaraka baada yq Uhurru !
Jones...Mohamed mimi nipo kinyume na dhuluma ya aina yeyote hasa ukandamizaji sawa halijatugusa ila tambua hata sisi tuna ndugu wa kiislam kwa namna moja kama nyingine linatugusa.
Je mna ni ushahidi upi ili kuthibitishia jamii madai ya uonevu wa NECTA dhidi yenu (tuupate hapa ili sisi ambao hatukuguswa moja kwa moja tuweze kuelewa nini kilitokea) maneno matupu hayawezi kutoa justification ya madai yenu kwenye jamii kuwa ni ya kweli.
Na je baraza walishasema chochote kuhusu haya madai? na mlichukua hatua za zaidi kudai haki yenu mahakamani badala ya kuandamana tu??
Mzee tupe ushahidi wa wizi huu!Lambo,
Jambo kubwa katika maelezo yangu ni historia ya kuandikwa hicho kitabu.
Mswada umeibiwa Maktaba ya TANU Lumumba ukachapwa kitabu.
Waandishi wa kwanza wa mswada wa kitabu hiki ni Abdul Sykes na Dr. Kleruu.
Abdul Sykes akajitoa kwa kuwa nyaraka zake katika kueleza historia ya African Association na TANU zilikuwa zinawaudhi baadhi ya watu ndani ya TANU.
Baba yake Abdul kabla hajafa mwaka wa 1949 aliacha mswada wa kitabu ndani yake kaeleza historia ya vipi aliunda African Association pamoja na wazalendo wengine mwaka wa 1929.
(Mswada huu ulitolewa hadharani mwaka wa 1968 na ni seminar paper History Department University of Dar es Salaam mwandishi Aisha Daisy Sykes).
Unapatikana Maktaba ya Chuo Kikuu East Africana.
Haya hayakutakiwa na huyakuti katika kitabu cha Ulotu.
Ulotu si mwandishi wa kitabu hiki - Historia ya TANU.
Hii ndiyo sababu ya kuwa na historia ya TANU bila ya historia ya walioshiriki katika kuasisi African Association na TANU yenyewe.
Nilipokuja kufunguliwa Nyaraka za Sykes na nikaandika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes ndiyo kitabu kikashtua watu wengi.