Kagera Babu ulienda?? kupambana na Idd Amini? Msumbiji kule kuokoa ndugu zetu? ushelisheli nako je! Zimbabwe? tuanzie hapo!! mwenzako babu Makongoro Nyerere alienda na huyo hapo karudi!!
nasikia kuna watanzania mlitorokaga kujiunga na JKT,JW, weye ulikuwa kambi gani babu! kwanza mwenzako kawawa alienda na jk mwenyewe! weye kambi gani? ukinithibitishia hapa najua ulikuwa kamanda siyo maneno tupu
si unamuona mzee mwenzako ulimwengu yule mzee bana mpaka UNO kaenda yule!! na picha zake ziko humu!! ktk story zako zooote sijawahi kusikia ukimtaja Ulimwengu!! wala kwenda mstari wa mbele km kina maerehem Hashim mbita!
STORY zako laini laini tuuuuuuuuu
Nyaru...
Kwa kawaida ninapomuona mtu ananishambulia mimi kwa kejeli na maneno yasiyo na maana huwa sijibu kuepusha shari ingawa ningependa kumnasihi kwa maneno mazuri ya kiungwana.
Lakini kwa kuwa napenda tufahamiane nakujibu na nakuwekea hapo chini makala ambayo naamini itakuzindua asa kheri huenda ikakusaidia ukawa mwerevu na kuwa kijana mwema mwenye heshima na adabu:
"JENERALI ULIMWENGU KATIKA KUMWELEZA MAALIM SEIF
Konganano la Maalim Seif lilihudhuriwa na watu wengi ambao wana mchango mkubwa katika maendeleo ya fikra Tanzania.
Kuanzia wasomi maarufu kama Emiritus Prof. Issa Shivji hadi viongozi wa dini waliosimamia haki bila hofu kama Sheikh Ponda Issa Ponda.
Walikuwapo watangazaji wa Radio na TV maarufu kama Hamza Kassongo na Charles Hilary.
Na kulikuwa na viongozi wa juu wa Tanzania kama Rais Amani Karume, Joseph Warioba na Joseph Butiku.
Kwa siku mbili ukumbi wa Kongamano la Uzinduzi wa Maalim Seif Foundation ulielemewa na mazito yaliyopita Zanzibar na yote hayo Maalim Seif akiwa katikati yake.
Kuna wakati wasikilizaji walifurahi wakapiga makofi kwa furaha na wakati mwingine ukumbi mzima ulijiinamia kwa kuona aibu na kuingia simanzi kuwa tumefikaje katika hali hiyo ya kufedheheka kama taifa.
Hapo wanajiuliza ingekuwaje kama Maalim asingetumia busara.
Tungejikuta na vifo vya watoto na wanawake maiti zimelaliana nje ya Hoteli ya Bwawani.
Jenerali.
Nilikuwa na Jenerali meza moja tukila chakula cha mchana.
Nikamwambia kuwa nimejaribu sana kuiga staili yake ya uandishi hasa lugha yake ya Kiingereza bila mafanikio na nimekata tamaa kwa ajili umri wangu umesonga mbele tabu kujifunza.
"Mohamed wewe ni wa kuniambia mimi maneno hayo?"
Kwa hakika niliyasema maneno yale kumuambia Jenerali kwa dhati ya nafsi yangu.
Jenerali akacheka akaniambia, "Basi bakia hivyo hivyo."
Huenda Jenerali hajui lakini yeye amekuwa na mchango mkubwa sana kwangu katika safari yangu ya uandishi.
Jenerali hakupata hata siku moja kuacha kuchapa makala zangu katika magazeti yake yote aliyoanzisha na kumiliki.
Kwa wanaonifahamu hasa katika miaka yangu ya mwanzo ya uandishi watakumbuka makala zile.
Makala ambazo wahariri wengine wasingethubitu kuzigusa.
Jenerali hakuwa na shida na kalamu yangu.
Jenerali alipokaribishwa kuzungumza akarekebisha kauli iliyomtambulisha kama mwanasiasa.
Jenerali akasema kuwa mwanasiasa ni yule anaefanya siasa kuwa ajira.
Jenerali akasema kuwa yeye anashughulika na siasa lakini si kama ajira bali anafanya na kazi nyingine.
Jenerali akaanza kueleza hali ya siasa ilivyokuwa Tanzania si muda mrefu uliopita.
Jenerali hakubabaisha wala kubabaika.
Kisha akaingia katika uchaguzi.
Hakufika mbali sana sauti ya Mzee Warioba tukaisikia sote ikiingia kati kwa upole na unyenyekevu mkubwa ikisema kuwa si lazima Jenerali aseme yote.
Nina hakika ni kuwa aliyetafadhalisha alikuwa Mzee Warioba laiti kama kauli ile ingetoka kwa mwingine...
Huyu ndiye Jenerali.
Kuna kitu cha miaka hii ya karibuni kinaitwa Streisand Effect.
Barbra Streisand alikuwa mwanamama mcheza senema na pia muimbaji na mimi nikipenda muziki wake katika miaka ya 1980.
Barbra alikwenda mahakamani ili mahakama iwazuie watu fulani kuweka nyumba yake hadhir kwa kila mtu ajue ilipo.
Barbra Streisand kafanya vile baada ya hawa jamaa kukaidi.
Kesi ilipokwenda mahakamani ikawa ndiyo kiama cha Streisand kwani jambo lenyewe sasa likawa bayana kila mtu analisoma kwenye magazeti na kuangalia kwenye TV; na kujua hiyo nyumba ilipo ilhali yeye alitaka nyumba yake iwe na stara.
Hii ndiyo Streisand Effect.
Mahakama hazina faragha.
Alilotaka Streisand liwe faragha mahakama likalimwaga uwanjani.
Nimesoma kuwa Jenerali kapewa onyo kali na Spika wa Bunge akimtuhumu kushambulia Bunge.
Baada ya onyo hilo ghafla jambo limegeuka kuwa burudani ya aina yake.
Kichekesho.
Nadhani katika hivi vichekesho kuna jambo la kujifunza hasa ukigeuza shingo nyuma kuangalia yaliyomfika Barbra Streisand.
Barbra Streisand kataka kadha kapata kadha wa kadha."