Lombo,
Kitabu hiki nimekieleza katika kitabu cha Abdul Sykes:
''Kwa mara ya kwanza historia ya TANU ilitaka kuandikwa na Abdulwahid mwenyewe.
Baada ya kupatikana kwa uhuru mwaka 1961 na TANU ilipokuwa sasa inataka kujiimarisha kama chama cha umma, inasemekana Nyerere wakati ule Waziri Mkuu alimuomba Abdulwahid aandike historia ya harakati ya Waafrika wa Tanganyika dhidi ya ukoloni wa Waingereza.
Hii kwa hakika ndiyo historia ya TANU. Dr Wilbert Kleruu ambae ndiyo kwanza alikuwa ametoka masomoni Marekani alichaguliwa na TANU asaidiane na Abdulwahid katika utafiti na uandishi wa historia ile.
Abdulwahid alirudi kwenye ofisi za TANU makao makuu; kwenye ofisi yake ya zamani aliyokuwa akiitumia kama rais wa TAA.
Nyaraka zake binafsi,shajara zake na karatasi za baba yake nyingine kuanzia mwaka wa 1929 wakati wa enzi za African Association zililetwa pale kwa utafiti kama ushahidi wa yale yaliyopitika zama hizo.
Maelezo ya Abdulwahid katika kuanzishwa kwa Africa Association inasemekana hayakupendeza kwa baadhi ya watu, kwa kuwa mwanzo wa harakati dhidi ya ukoloni jina la baba yake Abdulwahid, Kleist Sykes, lilikuwa likitawala.
Halikadhalika ilipofika kueleza namna TAA ilivyokujabadilishwa kuwa TANU watoto wake wote watatu Abdulwahid, Ally na Abbas wakiongozwa na kaka yao mkubwa Abdulwahid halikadhalika likawa linatawala harakati zile.
Matatizo yakawa yanarundikana kila uchao.
Historia hii ikawa mtihani kwa Abdul Sykes na kwa Nyerere na kwa baadhi ya viongozi wa TANU.
Haukupita muda Abdulwahid akatambua kuwa viongozi wapya walioshika nafasi katika TANU kwa kweli hawakuwa na nia hasa ya kutafiti na kuandika historia ya Tanganyika ya kweli bali nia na azma yao ilikuwa kumfuta yeye na ukoo wake katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Abdulwahid alipong’amua hili haraka akajitoa katika mradi ule.
Hata hivyo Dr Kleruu aliendelea na utafiti na akaandika historia ya TANU. Historia hii iansemekana ilifuta mchango mzima wa akina Sykes katika kuunda TAA na baadae TANU.
Hata hivyo baada ya kazi hii kukamilika haikuchapishwa na ikabaki katika maktaba ya TANU, Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam.
Lakini baadae kazi ile ilitoweka na ikachapishwa baada ya ‘’mwandishi’’ kufanya mabadiko kadhaa katika mswada ule ili usitambulike chanzo chake.
TANU iligundua kuwa ile ilikuwa historia yao iliyoandikwa na Dr. Kleruu wakafanya bidii kuzuia isichapishwe.
Kimya kimya TANU ikafanya juhudi ya kuzuia kitabu hicho kisitoke toleo la pili.
Lakini hili halikuwezekana na kitabu hicho kimechapishwa sasa mara kadhaa.
Uandishi wa kitabu kile haukutofautiana sana na kitabu cha TANU kilichotoka mwaka 1981 kilichoandikwa na Chuo cha TANU cha Kivukoni.''
Katika mswada wa kitabu ha Abdul Sykes mhariri wa kitabu changu alikataa nisitumie neno, ''wizi,'' kuwa mswada uliibiwa Maktaba ya TANU akasema naweza kushatakiwa na mimi sina ushahidi kuwa Abubakar Ulotu aliiba ule mswada.
View attachment 1987785