Lombo,
Vitisho vya nini ndugu yangu?
Babu yangu mkuu kaingia Tanganyika kutoka Belgian Congo kabeba silaha kama askari katika jeshi la Wajerumani lakini mwanae babu yangu Salum Abdallah kapigania uhuru wa Tanganyika.
Hii ni historia inayofahamika na ni katika athari za ukoloni.
Umemtaja Kleist Abdul Sykes, Meya wa Dar es Salaam.
View attachment 1988488
Kulia ni mimi, Yusuf Zialor, Kleist Sykes, Bubby Bokhari, Abdallah Tambaza.
Waliochuchumaa kulia Abdul Mtemvu, Wendo Mwapachu na Kaisi 1968.
Kleist alikuwa na miaka 20 mimi 18.
Nadhani umeona kuwa sisi wazee wetu walikuwa katika harakati za siasa za kupigania uhuru wa Tanganyika.