Gaudensia Kabaka Mwenyekiti wa UWT?

Gaudensia Kabaka Mwenyekiti wa UWT?

Lombo,
Nakushukuru sana kwa makala hii yako.

Hakika umenisaidia pakubwa kwa kujaribu kuwagutusha wenye mamlaka. juu yetu kuhusu wajibu wao katika yale ambayo mimi nimekuwa nikiyapigania.

Nakupinga kusema kuwa nimekuwa nikiandika kwa kebehi historia ya Mwalimu Nyerere na jinsi alivyopokewa na wazee wangu.

Katika hili naomba kama unao ushahidi uweke hapa hayo maneno ya kebehi kutoka kwenye kalamu yangu.

Nataka nikusaidie uelewe vizuri historia ya elimu na matatizo yaliyowafika Waislam kuanzia mwaka wa 1961 Tanganyika ilipopata uhuru wake:

1968 EAMWS ilivunjwa na serikali ili kuondoa uwezekano wa kuendelea na mipango ya elimu na ujenzi wa Chuo Kikuu.

Miaka ya 1970s Organisation of Islamic Conference (OIC)ilitaka kujenga Chuo Kikuu Tanzania serikali ikakataa kutoa kibali.

OIC ikajenga chuo hicho Mbale Uganda.

1981 Warsha wakiwa ndani ya BAKWATA kwa kujipenyeza waligeuza baadhi ya shule za Kiislam kuwa seminari ili kuboresha shule hizo.

Serikali iliingilia mchakato huu na shule zile zikarejeshwa katika hali yake ya zamani.

Mambo hayakuishia hapo.

Vijana wa Warsha waliojipenyeza BAKWATA wakafukuzwa BAKWATA kwa amri ya serikali na kupigwa marufuku kuongoza taasisi yeyote ya Kiislam nchini.

Mlezi wa Warsha Sheikh Hussein Malik akafukuzwa nchini.

Warsha haikuvunjiks moyo wakajenga shule Masjid Quba serikali ikakataa kuipa tasjila.

Warsha wakaendesha shule hivyo hadi Prof. Malima akiwa Waziri wa Elimu alipoipa tasjila.

Mwaka wa 1987 Prof. Malima akiwa Waziri wa kwanza Muislam kuongoza Wizara ya Elimu aligundua yaliyokuwa yakifanyika ndani ya wizara hiyo na akamtaarifu Rais Ali Hassan Mwinyi.

Prof. Malima akaondolewa katika wizara hiyo baada ya kikao cha CCM Dodoma.

Miaka ya 1980s Darul Iman kutoka Saudi Arabia ilitaka kujenga shule ya ufundi Kibaha.

Kama kawaida njama zikapita.
Darul Iman wakaufuta mradi na kuondoka nchini.

Yako mengi pamoja na matatizo ya NECTA nk. nk.

Nasikitika hukuwa unayajua haya kwa hiyo hukuweza kuyafikisha kwa wahusika.

Nakubaliana na wewe kuhusu sumu kwa jamii.

Lakini sumu hii haikorogwi wala kupikwa na Waislam.

Kuhusu tuzo ya JF hili naona limekuchoma sana maana umekuwa ukilirejea.

Nina tuzo mbili kabla, hii ya JF ni ya tatu.

Hayo mengine naona niyanyamazie kwa sasa.

Ikitokea fursa In Shaa Allah tutayazungumza.
Hongera kwa maelezo mazuri,ktk yote ninakukubali isipokiwa tu bado nakuona una Udini,kwa Hilo tukubaliane kutokukubalina !
Kuna mambo ,naomba unisaidie ...hivi ukihojiwa na hizo TBC ,AZAM huwa unaeleza kinagaubaga haya unayo andika hapa JF!
Mf.suala la Mama G.Kabaka,suala la 20:80,
Kama unayaelezaaga ' kwa uwazi Basi kongole!
Kama ndivyo ...Basi ktunatatizo.kama.Taifa!
Jambo la Pili,sijaonakweye maandishi yako ukieleza kama hili la Ukatili' wanaofanyiwa Waislam kielimu,kuwa umeisha au una3ndeelea?!
Mara kadhaa nilikutolea Mfano was Kisarawe ya miaka 2000s ambapo UNICEF walwekeza Hadi Wilaya hii iliukuwa nyuma ikaingia kwenye Wlaya Bora,! Sijui unasemaje katika hili kwa kuzingatia hoja yako !
Nashukuru kwa kukiri kuwa Udini ni Sumu,Ila umekana kuwa sio Waislam wanaeneza ...labda unawajua!?
Naendelea kusisitiza hujamtendea Haki,mama Kabaka hata kidogo...!
Kama Wenyewe hawatakuchukulua hatua itakuwa no ajabu Sana!
JF naamini ni Jukwaa linajali Kulinda na Kutetea Haki za Binadamu na Uhuru wa kipashana Habari,kukupa Tuzo Mwandishi unaye Hukumu watu (Kama Mama Kabaka) kwa tuhuma nzito za Kidini sio sawa.Na wao Wataonekana wanaunga mkono!
Labda kama walikupa Tuzo kwenye Eneo au kazi Mahsusi!
Jioni njema
 
Toka asubuhi nilijua hutofika mbali na mimi.
 
Lombo,
Toka asubuhi nilijua hutofika mbali na mimi.
Nitafikaje mbali Mkuu ikiwa una vimelea vya Ubaguzi was Kidini was kiwango hicho!
Hoja zilezile umekariri!
Nakuuliza Kisarawe ilipoongoza 20:80 ilikuea wapi hujibu!
Kimsingi wewe umeamua kuwafanya wenzio wajinga,!
Muislam mwerevu hawezi kukusikiliza!
Inawezekana hata Mamlaka zingine Imekuacha ujilishwe upepo!
 
Nilijua utarudi tena.

Lakini bahati mbaya ulishaniaga na mimi nimeshafunga mjadala.na wewe.
 
Fuma...
Udini ni kukandamiza wale wasiokuwa imani yako na kuwanyanyua wale wa imani yako.
Unaijua hali ya Waislam wa Tanzania katika elimu?

Unaijua historia yake?
Soma historia hii utarudi hapo kujadili kwa adabu na heshima wala hutatukana.

Utatambua kuwa lipo tatizo.

Prof. Hamza Mustafa Njozi baada ya Rais Mkapa kutaka apewe ushahidi wa kisayansi Njozi aliandika kitabu, ''Mwembechai Killings...''

Yaliyomo ndani ya kitabu hiki ulitisha serikali.
Iliamua kukipiga marufuku kitabu.

Waliokipiga kitabu marufuku si Waislam kwani wanapenda tatizo hili liwe wazi na lijadiliwe kwa amani na salama ili haki itendeke.

Tatizo hili linataka ujuzi si matusi.
Kitabu kilikuwa cha kichochezi hiki
 
GAUDENSIA KABAKA MWENYEKITI WA UWT?

Mwenyekiti wa UWT Gaudensia Kabaka ndiye aliyehusika kuwafukuza Waislam 11 Chuo Kikuu cha Dodoma na kusimamisha ujenzi wa msikiti hapo chuoni ambao ujenzi wake ulishaidhinishwa.

Leo yupo katika sherehe za kumuenzi Bi. Titi Mohamed.

Huyu ndiye kiongozi aliyewafukuza wajukuu wa Bi. Titi hapo chuoni na kuzuia ujenzi wa msikiti.

Kwa yale aliyopigania Bi. Titi Mohamed na wanawake wote katika TANU ya enzi zile huu ni msiba mkubwa.

Huyu Mama hastahili kuongoza wala kunasibishwa na umoja huu ulioasisiwa na mama zetu akina Bi. Titi, Bi. Hawa bint Maftah, Bi. Zarula bint Abdulrahman kwa kuwataja wachache.

Angalieni picha hiyo ya kwanza hapo chini pcha iliyopigwa na Mohamed Shebe ya mkutano wa TANU 1955 wakati wazee wetu wanautafuta uhuru wa Tanganyika.

Angalia huo umma Viwanja Vya Mnazi Mmoja na tazama hiyo sehemu nyeusi.

Hayo ni mabaibui ya bibi. mama, na shangazi zetu wamekuja kuujaza uwanja na kumtia nguvu Mwalimu Nyerere.

Mama zetu wameitika mwito wa "kuno kuno."

Hapo ndipo walipokuwa wakiimba nyimbo za lelemama kuhamsisha wakiimba."

Muheshimiwa nakupenda sana....Insha Allah Mungu yupo Tanganyika tutajitawala.''

Tujitawale halafu iwe nini?

Gaudensia anyanyase Waislam, Gaudensia avunje misikiti yetu?

Gaudensia awafukuze chuoni wajukuu wa hawa wanawake unaowaona hapo chini kwenye picha?

Picha ya pili hao wote mbele hapo wanaongoza maandamano ya akina mama mimi mama zangu.

Hao ndiyo msingi wa UWT.

Yupo Bi. Mwamvua bint Mrisho (Mama Daisy), Bi. Titi Mohamed na Bi. Zainab Tewa.

Serikali tu haina dini iweje shule /vyuo vya serikali ziwe na dini. Wee mzee unazeeka vibaya
 
As long hajavunja sheria za nchi sio tatizo. Mzee Said anareclaim the forgotten/deleted history
Ni kweli

Ni ule ubaguzi wa kidini tu ndio unaondoa the best flavor in his work
 
Saint...
Hapana hatuoti.

Tulikuwa na mipango mizuri sana ya elimu chini ya EAMWS na tukafikia kutaka kujenga Chuo Kikuu lakini EAMWS ikapigwa marufuku na serikali na kuundwa BAKWATA.

Huu ukawa mwisho wa mipango yetu ya elimu.

Juu ya haya hatukukata tamaa tukajenga shule kila mtu pale alipo na hizi ndizo shule zilizohujumiwa na NECTA na tukaandamana.

Nimekieleza kisa hiki hapa.
Ushahidi wa mandamano hayo na hisia za Waislam ni hizo hapo chini kwenye picha:

y2bjzzo5_GwKWqCA6fl1z3bTWUikmN0urr0CLf2QOT-YS878Wd22wcNoLY3r77V-Cr1vEw5ji8tsGVdKTUGOBguP-8gy2kWelxvbk6OAdra44K58F1ZGKItRUPADxF8_BQRS6YbzPV0JjSb8NBDD0K0zk_txNV1mQs3J1_LjjKtnrVZ1HoQWYyr1zLN_olO-B7RQvCV_BtGLN0s4UjHJx6-zjCwmnKb9JheTiTUOScTBztdoJuatvJMCilmhkfhYdS8Kq8M-oFduEc0Z4tpe5aq6hmwMOpcBZKCKFO2grJ596oASPZwk_FNYC8bCeHrRzUm3rk0owjaD7PJKAAR8IhddZomSxEJy_osaqWezmKF-ghme-aaL2UDguw2JSKjx3q0Jm4j-mS1cZupOOaJnd7my5p6OwfMQWslGNdhMQr41ZE2B04sVuOGcOZdHOD4JUtyqzDB6EluicyV73RWpADO6dE89UizGMdlGccmFRbebSDBn9kx5JmbXgpFnjankugidk0102zliFiR2XsWoKXj__XAyP6dAir_643ENtAeN1212aHytwCz57FMrrJi0B-QatIpH4U_Yu2m3KVgNfnclqucwJWvSqI_COC1v_nvHgGsxaRzlkJYUAhiQ7PgH9iTpswmd_YHWB20OQ9f_ipQuFWXQZj1miYvjYcLx6OT0KfMBTP0qyngiNOzYKvyI1s964mTzXJteY9kIhrxVOeU=w480-h320-no

Moja ya bango katika maandamano ya kupinga NECTA.
Andamaneni TU.
Necta haivunjwi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom