Kwa hiyo Mzee ...mimi.niridhike na haya maelezo kuwa ni Ushahidi,!?
Hata Kama ndivyo...hoja yangu ni kuwa ,Historia iliyiandikwa humo Ina mashiko!
Kuliko unavyotaka kutuaminisha wewe!
Lombo,
Hapana usijitese bure kwa miaka mingi watu wameamini historia ya iliyoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni.
Hapana ugomvi.
Wala hakuna anaekulazimisha lazima uamini historia niloyoandika kutoka Nyaraka za Sykes inayeleza kuwa kadi no. 1 ya TANU ni ya Julius Kambarage Nyerere, kadi no. 2 ni Ally Kleist Sykes, kadi no. 3 ni Abdulwahid Kleist Sykes, kadi no. 4 Dossa Aziz, kadi no.5 Denis Phombeah, kadi 6 Dome Okochi Budohi, kadi 7 Abbas Kleist Sykes nk.
Kuwa kadi 1000 za mwanzo alinunua Ally Sykes kwa fedha zake na ndiye aliyesanifu na kuzichapa Printpak wachapaji wa gazeti la Tanganyika Standard nk.
Hakuna wa kukushurutisha uamini haya.
Wala hakuna wa kukulazimisha kuwa baba yake Abdul Sykes ndiye muasisi wa African Association.
Unaweza hata kuamini kuwa watu hawa hawakupatapo kuishi Mtaa wa Kipata (sasa Mtaa wa Sykes).
Baba zangu wawili wamekulia mtaa huu nyumba ya babu yangu ikielekezana na nyumba ya Kleist Sykes.
Hawa kwangu ni wazee wangu wameniona nazaliwa nimekuwa wananiona na nimewazika makaburi ya Kisutu mimi mtu mzima.