Kuna watu wanafuraaaaahi kusikia hivi vifo. R.I.P
Inaweza ikawa ni fikra zako, kwa sababu dhamira yako imekufa.
Kila mwenye akili, furaha yake ni kusikia corona imetokomezwa. Aliyefariki hana tofauti na mimi na wewe. Pengine hakuna alichotenda tofauti na tunavyotenda sisi. Huenda alikuwa mwema na mwerevu kuliko sisi.
Tuna nini sisi hata tufurahie kifo cha mmojawetu huku sisi wenyewe hatujui kama tutavuka katikati ya janga hili la kutisha la corona na mengine mengi yatuzungukayo?
Tushirikiane na Ulimwengu nzima kupambana na corona na majanga mengine. Ni juhudi za pamoja ndizo zinazoifanya Dunia kuwa ya matumaini. Ni nani angeweza kuishi bila ya:
Chanjo ya ndui
Tiba ya kipindupindu
Tiba ya malaria
Tiba na chanjo ya kifua kikuu
Chanjo ya surua
Madawa ya magonjwa ya moyo, kisukari
Tiba za typhoid, amoebic dysentery,
Tiba za magonjwa ya zinaa
Na mengine mengi
Ni ushirikiano wa Dunia nzima ndio uliosaidia kupatikana kwa tiba hizimaana hizi dawa zote hazikugunduliwa na nchi moja au mtu mmoja. Hapo ndipo tunapooneshwa maana ya neno lile - viungo Ni vingi lakini mwili Ni mmoja. TUNAISHI KWA KUTEGEMEANA. Tumshukuru Mungu kwa ugawaji wa karama kwaajili ya ukamilifu wetu.