Gavana wa BoT: Deni la Taifa ni Tsh Trilioni 100, linazidi kukua japo bado linahimilika

Mama alikuta deni linasoma trilioni 72, miaka minne kakopa trilioni 28. Akimaliza madaraka tunapigwa mnada maana tutakua tumeshavuka hiyo 55% wanayojigamba ndani ya miaka mitano ijayo..
 
Upande wa pili wa bahari wana asilimia ngapi katika hili deni? Maana nasikia hata wao wanakopa kwa udhamini wa huku barabarani
 
Nchi kuuzwa ni hakika
 
Mda si mrefu deni litafika Trillioni 200, hakika Kizimkazi anaupiga mwingi
 
ROSTAM AZIZI NA GSM NA BARESSA SAMIA NA ABDUL KIKWETE..MWINYI NA MASHEKH WA BAKWATA NI LAZIMA WAZIDI KUWA KABILIONEA.
 
Hela kibao zimekopwa miradi mingi imekwamwa tena miradi yenyewe ilikuwa chini ya trillion 20 lakini zimekopwa zaidi ya trillion 50 Kuna siku Forbes watatangaza mtoto wa bimkubwa au familia yake ni matajiri Africa nzima maana sio Kwa ufisadi huu wa waziwazi ndani ya miaka mitatu
 
Walioingia mikataba ya hiyo mikopo wataondoka duniani na kuviachia vizazi vijavyo matatizo matupu. Nchi Ina rasilimali Kibao ambazo zinatuwezesha kufanya kila kitu kwenye hii nchi,ila tumeishia kukopa huku tukigawa rasilimali zetu kwa mikataba ya kinyonyaji kwa manufaa ya wachache.
 
Asisahau tu kumpongeza mama kwa kufanikisha deni kukua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…