MTZ 255Dar
JF-Expert Member
- Sep 25, 2018
- 1,149
- 3,963
Matumaini mapya ya kusitisha vita vya GAZA yaanza kuonekana mara baada ya Wapatanishi (Misri na Katari) kueleza kuwa, kundi la wapiganaji la HAMAS limebadili Msimamo wake wa awali wa kutotoa orodha ya mateka walioko hai mpaka sasa.
Kundi la wapiganaji la HAMAS limekubali wanajeshi wa ISRAEL Kubaki ukanda wa GAZA, katika kile kinachoonekana kubadili msimamo wake wa awali ambao ulikwamisha upatikanaji wa mpango wa kusitisha vita.
Kundi la HAMAS tayari limekabidhi orodha ya mateka walioko hao mpaka sasa,wakiwemo raia wa Marekani,ambao wataachiwa huru chini ya mpango huu wa kusitisha vita. Hii ni kwa mjibu wa wapatanishi kutoka Misiri na Katar.
Ikumbukwe kuwa,kikwazo kikuu kilichokwamisha mipango ya kusitisha mapigano, ni misimamo mikali kutoka pande zote mbili za kukataa kulegeza mashariti yao. Kundi la HAMAS liliitaka ISRAEL kufanya yafuatayo kabla ya kuwaachilia mateka wote;
1. Kuondoa wanajeshi wake wote kutoka GAZA
2.Kuwaachilia maelfu ya wafungwa wa kipalestina walioko kwenye jela mbalimbali za ISRAEL.
3. Kuondoa Msingiro wa GAZA ambao umedumu tangu mwaka 2005.
Hata hivyo, baraza la vita la Israel likiongozwa na waziri mkuu BENJAMIN NETANYAHU lilikataa mashariti hayo ya HAMAS na kuapa kuendelea la Vita mpaka pale malengo yake yatakapotimia. Lakini,ISRAEL ilikubali shariti la kuwaachia wafungwa wa kipalestina kutoka kwenye jela za ISRAEL.
www.telegraph.co.uk