ITR:
Kweli iko tabu sana! Hivi unajua historia ya Middle East wewe,! ama unaokoteza okoteza tu! Mmmebeshwa half truth za misikitini na nyinginezo ambazo ni very biased! Mara occupation! mara Israel ina commit genocide, bila kuwa na basis yoyote ile, hii brainwashed ya Waarabu aliyowajaza inasikitisha sana! Dont be lazy, do your own research !
Halafu unazungumzia Vietnam na US......Hiyo ni mada nyingine tofauti! Huifahamu context kabisa, na kama Hamas inadhani inaweza ku copy na ku paste vita vya 1955 basi itazidi kushindwa na kushindwa......Hiyo element ya Jihad ndio itakayowaangamiza Wapalestina leo na kupoteza kabisa objectivity katika kujenga hoja ya maana leo! Na ndio maana means waliobakiza Hamas katika mgogoro huo umeiona October 7
Haya hebu turudi kwenye Historia ya Palestina...Sijui unataka nianzie wapi, sijui kama you can handle the historical facts and truth. Kelele kubwa zinazopigwa na Wapelestina na washirika wake leo ni kwamba Kama Israel ikiruhusu tu Wapelestina wawe na taifa lao wenyewe, amani itapatika Mashariki ya kati. Hiki ndio tunachokisikia UN na baadhi kutoka kwa wana diplomasia wengi wa Ulaya na Uarabuni, na hata maproffesors katika baadhi ya vyuo US. Na ndio information zilozagaa kwenye media nyingi!
Kitu ambacho wengi wanashindwa kutambua Israel imetoa na kukubali kuanzishwa kwa taifa la Wapelestina zaidi ya mara tano! Nyakati tofauti tofauti! Hebu tuiangalie historia, ambayo wengi ni vipofu!
1. Baada ya kuvunjika kwa Dola ya Ottoman 1914 (Ottoman Empire) Baada kushindwa katika ya vita vya kwanza vya dunia, Uingereza ilichukua mamlaka ya kulitawala eneo hilo LOTE la Mashariki ya kati, na hiyo sehemu inayoitwa Palestine ( Kumbuka Hakukuwepo taifa hapo lilokuwa likiitwa Palestine au Israel wala utawala wowote ule)
Miaka 17 baadaye, yaani 1936 Waarabu waliasi (rebell) dhidi ya Utawala wa Waingereza (
The great Palestine Revolt ) Au Waarabu wenzako wanaita "(
al-Thawra-al Kubra) Sana ilikuwa ni kupinga Uingereza kutowasaidia wao (Waarabu walichuke eneo hilo lote na pia kupinga Wayahudi wachache waliokuwepo pia mahali hapo kuwakaribisha Wayahudi wenzao toka nchi ya Ulaya na nchi za Kiarabu.
Ili kutatua tatizo hilo la uasi wa Waarabu, Uingereza ilitengeneza Task Force ambayo iliitwa
PEEL COMMISSION Kuona jinsi ya kutatua mgogoro huo, na July 1937 ilikuja na matokeo haya,
kuwa kuna makundi mawili, Waarabu na Wayahudi wote wanataka kutawala eneo moja, wote wana historical attachment na hilo eneo, hivyo walihitimisha kwa suluhisho hili:
Kuundwe Mataifa mawili (
Two Independent States) Moja la Waarabu na taifa jingine la Wayahudi.(Two States Solution) Mgawanyiko huu ulikuwa unawapendelea Waarabu mno, Uingereza iliwapa 80% ya eneo hilo wanalogombania na Wayahudi wapate 20% Kilichotokea Waarabu walikataa KABISA hiyo asilimia 80% na Wayahudi Walikubali huo mgao waliopewa wa 20% Warabu walikataa katu katu na kuendelea kugombana na Waingereza na pia kuwashambulia Wayahudi.
HILI NI PENDEKEZO LA KWANZA KABISA WAARABU WALIKOLIKATAA.
2. Miaka 10 baadaye, 1947, Uingereza iliomba Umoja wa Mataifa itafute suluhisho jipya, maana lile la kwanza la Peel Commision lilikuwa limeshindikana, na mgogoro ulikuwa ukiendelea tu! Hivyo Umoja wa Mataifa uliona njia ya kutatua mgogoro huo ni kugawanya tena eneo hilo!
November 1947 Umoja wa Mataifa ulipiga kura ili kutengeneza Mataifa mawili (
Resolution 181)M
ataifa yaliyopiga kura kukubali yalikuwa 33, na kupinga 13, na kumi hayakupiga kura (Abstain) Mgawanyo huu uliwapa Waarabu 42% na Wayahudi 56% (Kuna sababu nyingi za mgawanyo huo siwezi kuziweka hapa. ) Kama ilivyokuwa mara ya kwanza, WAARABU WALIKATAA AZIMIO HILO WAYAHUDI WAKALIKAKUBALI na kujitangazia taifa lao sehemu waliyopewa na UN
Na sio kulikataa tu, Warabu walienda hatua ya ziada, siku ya May 14 1948 mataifa yafuatayo, Lebanon, Syria, Misri, Iraq, na Saudi Arabia waliingia Vita na Israel, na kuleta matokeo mabaya mno kwa Waarabu, walipoteza lile eneo walilopewa na UN 1947, Kwa kifupi Israel ilichukua 60% ya kile Walichopewa Waarabu na UN, na Hapo ndipo Waarabu walipopoteza pia West Bank na East Jerusalem! na kuwa "occupied territory" na Jordan!
Matokeo ya kushindwa kwa Waarabu kulifanya wengi mno wakimbie eneo hilo na kuwa Wakimbizi! Wao wenyewe wanaita
Nakba ( Catastrophe) au janga ! Huo ndio ulikuwa mwanzo wa Waarabu (Wapelestina) kutawanyika katika nchi nyingi za kiarabu.
3. Miaka 20 baadaye, 1967, waarabu wakaanzisha vita tena! Wakiongozwa na Misri na kusaidiwa na Syria na kuishirikisha Jordan, wakataka kuliangamiza taifa la Israel! Vita hivi ambavo vinajulikana kama vita vya siku sita (
Six Day War) Viliisha kwa ushindi mkubwa mno kwa Israel, na kushindwa vibaya mno kwa Waarabu! Jerusalem na West Bank ambayo ilikuchukiwa na Jordan katika vita vya 1948 ilichukuliwa na Israel na Gaza iliyokuwa chini ya Misri.
Utawala wa Israel uligawanyika mno jinsi ya kuyamiliki maeneo mapya waliojitwalia katika ushindi wa vita hivi! Baadhi walitaka maeneo ya West Bank kuyarudisha kwa Jordan na Gaza kuirudisha tena Misri ili wawe na amani na Waarabu! Na wengine walitaka kuwapa Waarabu waliokuwa makimbizoni ambao waliaanza kujiita rasmi Wapelestina! Ambao Israel ilitegemea wataunda taifa lao wenyewe! Lakini kila option ilikuwa ngumu! Na ilikuwa na Vipingamizi vyake!
Baada ya kushindwa huku kwa Waarabu , June 1967, Mataifa ya Kiarabu chini ya umoja wao
(Arab League Summit) Walikuta Khartoum, Sudan August, 1967 na kutoa na Maazimio matatu ( The Khartoum Resolution) yanayojulikana "Three No"
- No Recognition of Israel
- No Negations with Israel
- No peace with Israel
Na Waarabu kwa pamoja wakalikata kabisa wazo la " Two State solution" Hii ikawa ni
MARA YA TATU WANAKATAA KABISA WAZO LA TWO STATE SOLUTION!
4. Mwaka 2000, Waziri Mkuu wa Israel Ehud Barak alikutana Camp David na Yasser Arafat kiongozi wa Wapelestina, ili wafikie hitimisho la "Two State Solution" Ehud Barak aliwapa offer Wapelestina sehemu yote ya Gaza na 94% ya West Bank! na East Jerusalem kama Makao Makuu, lakini Yaseer Arafat alikataa kabisa makubaliano hayo! Rais wa wakati huo wa Marekani, Bill Clinton alimwambia wazi Yasser Arafat maneno haya:
"
If the Israelis can make compromises and you can't, I should go home. You have been here 14 days and said no to everything. These things will have consequences. Failure will end the peace process. . . . Let's let hell break loose and live with the consequences."
Baada ya Yasser Arafat kukataa makubaliano hayo, alianzisha wimbi la watu kujilipua kwa mabomu na kuua kama Waisarel 1,000 , kwenye vituo vya mabasi, migahawa nk! kumbi za harusi nk!
H
ii ikawa ni mara ya NNE offer ya Israel inakataliwa.
5. Mwaka 2008 kukawa na mazungumzo mengine, kati ya Waziri Mkuu Wa Israel Ehud Olmert, yeye alienda mbali zaidi ya Ehud Barak, aliongeza maeneo ya Kuwapa Wapalestine, lakini kama alivyofanya Yasser Arafat, Mahmoud Abbas kiongozi wa Wapelestina alikataa!
Hii Katalio la Amani la mara ya Tano! Kati ya offer ya 4 na ya tano, Israel iliirudisha Gaza mikononi wa Wapelestina na kuwapa complete control na kuweza hata kufanya uchaguzi ambao uliiweka Hamas madarakani! Kinachoshangaza kitu kikubwa ambacho Hamas walifanya toka 2005, ni kugeuza Gaza uwanja wa mapambano! Na kuanza kurusha maroketi Israel!
Ikumbukwe kwamba kila Mara Israel inapokubali " Two States Solution" Wapelestine wanakataa.....Maana agenda yao ni moja tu! Kuifuta Israel chini ya jua! Kwa Wapelestina wakiongozwa na Hamas support toka Iran wao wamekataa kabisa kuwepo kwa taifa la Israel mahali hapo! Jambo wanajua wazi HALIWEZEKANI KABISA!
Jamaa yangu, Waarabu wamejaribu kutumia vita toka 1948, 1967, 1973, Wanashindwa na kupoteza maeneo! Egpty walipoona wanashindwa walifanya mapatano na Isarel hata kurudishiwa Sinai walioipoteza 1973!
Waarabu wanachokitafuta hawatakipata....! Wanapoteza Gaza kwa gharama kubwa mno! Kila approach huwa haiwafikishi mbali....Hii ya October 7 matokeo yake unayaoona! Hamas is just a death cult!
think you can handle the truth. Kelele tunazozisikia leo