Gazeti la Mawio lafungiwa kwa miezi 24 kwa kosa la kuwahusisha Mkapa na Kikwete sakata la madini

Gazeti la Mawio lafungiwa kwa miezi 24 kwa kosa la kuwahusisha Mkapa na Kikwete sakata la madini

Tanzania ni takataka? wewe mwenzetu raia wa nchi gani maana hili ni tusi kwetu wazalendo, kama wewe ni mtanzania pia tafadhali tangulia dampo tutakukuta.
Wazalendo mafisi wanashabikia gazeti likifungiwa kwa kuandika habari za mafisadi?
 
Njoo nikuonyeshe nakala zingine hujazaliwa ninazo.wewe so unafungia vitumbua au kuuza kwa wauza duka?!
Lama una nakala za kabla sijazaliwa basi wewe ni mstaafu,ndiyo maana unaomuda wa kusoma magazeti,wapambanaji hawana muda huo.
 
Benja na Mrisho hawatakiwi kutajwa kwa maovu yoyote kwa sababu hata mpinga ufisadi mkuu alisema "Nitawalinda".Halafu suala la kuibwa madini haliwahusu sana hawa wazee kwa sababu wao sio walinzi wala wagambo ni wenyekiti wa CCM wakati huo.
 
Majitu yanalinda majizi, halafu yanajifanya yanapinga ufisadi. Kama KIKWETE na MKAPA walifanya makosa yaliyosababisha taifa letu liendelee kuwa maskini kwanini wanalindwa?

Leo hii MAGUFULI anafanya makosa hayo hayo waliyoyafanya watangulizi wake, kwakuwa anajuwa, hata siku akiondoka, hakuna wa kumgusa.

Bila katiba mpya hapa! Hakuna kitakachoendelea Tanzania.

Bila kuiondoa CCM hapa hakuna kitakachoendelea Tanzania.

Nisisikie lijinga linazungumzia suala la Uzalendo....!
 
Hizi Akili Za Kimakinikia Za Baadhi Ya Wakulu, Haziwezi Kukaa Sawa Bila Smelter.
 
nadhani hawa jamaa tumewapa madaraka ya kulevya wanafanya wanavyotaka,kuna umuhimu wa kuingia barabarani kudai katiba mpya
 
Wewe na mimi tunafamiana kwa ukaribu sana lakini nitakuletea ujumbe huu kutumia avatar yangu hapa JF.

Nakuomba na ninakusihi sana muwafungulie Mawio hiki kifungo mlichowapa.

Serikali ya Raisi Magufuli ambayo wewe ni mshirika inapata mvuto mkubwa sana duniani kote kwa uongozi wenu. Sifa hii inaweza kutiwa dosari kwa kitu kidogo sana kama "kuminya uhuru wa vyombo vya habari". It is not worth it Sir.

Naomba muwape Mawio onyo au karipio kali halafu waendelee tu.

Serikali has accomplished so much in a very short time. Currently, you are riding a wave of admiration duniani kote. Don't let Mawio ruin this.

We (Tanzanians) all need a smooth sailing of our President's policies. Let's not invite unnecessary distractions.
 
Bado haiondoi ukweli kua Ben na Mrisho walizingua hata hao wanaopigiwa kelele kua ni wezi watapona tu.Ccm hawasafishiki wote wezi tu.La muhimu ni kupiga kazi watoto wetu wale siasa za bongo ni kuumizana vichwa tu.Nashauri hata kina lisu kaeni kimya tu mnapigania wajinga kwa kupambana na wezi ila nani anawaona kwenye hili kundi la vipofu?
Umeonaeee....

Tunasubiri amalize muda wake tuje tena kupigishwa kelele mikataba ya Bomberdier, Chato int. Airport, standard gauge..

Saivi kuiona ni mwiko.

CCM ni ileile...mi sina muda.
 
so tuwajadili wahusika wengine tu ila hawa wawili waachwe. Hivi mawaziri watakaopandishwa kizimbani wakajitetea kwamba ulikuwa uamuzi wa pamoja wa baraza la mawaziri (ambalo Rais ndio Mwenyekiti) itakuwaje? Magufuli hadi leo akibanwa sakata la uuzaji wa nyumba za serikali anajibu "it was collective decision by cabinet".
Mkuu kwani Lowassa alisemaje baada ya kubanwa sana na media... "maagizo toka juu"..

The same will be said soon from Chenge et.al.

CCM ni ileile
 
Back
Top Bottom