Gazeti la Mwanahalisi linatafuta cha kusema pindi baraza la Mawaziri litakapotangazwa

Gazeti la Mwanahalisi linatafuta cha kusema pindi baraza la Mawaziri litakapotangazwa

Kubenea tapeli yule,,hapo anacheza na akili za watu
Wewe umempa yako achezee? Kama ndiyo shauri yako. kama hapana kwa nini uamini hao watu wengine akili zao zitachezewa? Take it or leave it. Mbona udaku mnasoma kila siku na hatuwasikii mkilalamika huku? Hata riwaya ambazo zimeandikwa kuwa ni za visa vya kubuni mnazisoma, na tamthilia au filamu mnaangalia hadi wengine mnatoa machozi kwa visa na matukio ambayo mnajua kabisa dhahiri kuwa ni ya kubuni. Sasa mnahangaika nini na majina 8 ya mawaziri watarajiwa?
 
jamani mwenye kuelewa cv ya kubenea iwekwe hapa tuichambue tunaweza kumsifu kama mtu wa madia mahili kumbe hana fani hiyo
 
Hao nane binafsi naomba wasipewe kabisa wizara yoyote.... Hasa januar makamba na riz1 kikwete......
 
Mkuu TataMadiba

MWanahalisi ni gazeti pendwa kwa habari za uchunguzi.

Kumbuka ni MWanahalisi huyu huyu ambaye alinadika HABARI KUHUSU ALIYEMTEKA NA KUMTESA DR. ULIMBOKA.

je nayo ilikuwa ni uongo?????? mbona mliamua kulifungia hili gazeti kama ni gazeti la uongo???

Lisemwalo lipo na kama halipo ujue linakuja.

Usiweweseke tulia siku yake itafika tu.
swadakta
 
Last edited by a moderator:
Hilo gazeti la mwaka 205 kipindi zipo tawala za kifalme, leo tena???
 
Anajalibu kuwa mtabili na pia kawataja hao ili wasiwemo si unajua kama ilivyokuwa kwaa. PM
 
niliona kama gazeti hilo wapiga ramli kwa kusema ubashiri kama mganga wa kienyeji
 
hili ni gazeti la udaku kama yake ya shigongo ...habari zake ni kuzisoma na kupuuzia
 
Mbona wewe ndiyo unajisumbua bure?

Nani kakwambia uwahi huku.
Acha watu wasome gazeti wapate habari, mbona Uhuru lipo na unasomaga wewe na hakuna anayekuuliza?

Hivi MwanaHalisi bado linaongoza kwa mauzo kama enzi zile? maana siku hizi nikipita kwenye vibanda vya magazeti nakuta nakala za kutosha zimebaki
 
MWANAHALISI wamekosa mwelekeo siku nyingi habari zao wanazoandika mara nyingi zinakuwa hazina uhakika kabisa. Kwa mfano, mwezi uliopita wa novemba waliibuka na habari moja kwamba hotuba ya Rais Magufuli ya uzinduzi wa Bunge imevuja. Katika habari hiyo walijaribu kuelezea sehemu ya hotuba hiyo mambo ambayo rais angeyazungumza lakini hotunba rasmi iliyokuja kutolewa na Magufuli ilikuwa tofauti na ya Mwanahalisi waliyosema imevuja. Uzushi wa gazeti hili unakimbiza wateja. Tangu mwandishi JOSEPHAT ISANGO amejiunga ktk gazeti hili amekuwa akipotosha kabisa habari kwa malengo yake binafsi.
 
Mtoa mada umeandika kwa mihemko sana..mie sion tatizo na hao waliochaguliwa mbona ni watu waadilifu na wachapa kazi..wewe una lako jambo!hili baraza ni safi sana haijawai tokea!!na ndio lenyewe original si chenga..magufulselemaaa..hapakazituuu
 
Lengo la mwanahalisi hasa ni kuwaharibia hawa ili wasiteuliwe,
na wakiteuliwa achukue credit kuwa ametoa habari ya kweli,
wasipoteuliwa anakuwa katmiza lengo na pia atasema baada ya kuvuja rais akabadilisha,

hapa rais asiangalia media zinasema nini,ateue kwa utashi wake,huyu kubenea yuko kwenye misheni yake na atapenda kuharibia utawala uliopo kwa kadri anavyoweza
 
Wewe umempa yako achezee? Kama ndiyo shauri yako. kama hapana kwa nini uamini hao watu wengine akili zao zitachezewa? Take it or leave it. Mbona udaku mnasoma kila siku na hatuwasikii mkilalamika huku? Hata riwaya ambazo zimeandikwa kuwa ni za visa vya kubuni mnazisoma, na tamthilia au filamu mnaangalia hadi wengine mnatoa machozi kwa visa na matukio ambayo mnajua kabisa dhahiri kuwa ni ya kubuni. Sasa mnahangaika nini na majina 8 ya mawaziri watarajiwa?

Ha ha ha Utotole umemaliza wakishindwa kukuelewa hapa basi kutakuwa hakuna namna
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom