Gazeti la Mwanahalisi linatafuta cha kusema pindi baraza la Mawaziri litakapotangazwa

Mkuu ukilisifia Mwanahalisi kwa kumuandika mtu liliyemuita mtekaji wa Ulimboka unazidi kulimaliza na kuonesha kuwa halifai. Si Mwanahalisi hili hili lililoandika Makala zaidi ya 70 kuelezea ufisadi wa LOWASSA? Siyo LOWASSA huyohuyo aliyepanda jukwaani pale Ubungo kumnadi KUBENEA(MMILIKI WA MWANAHALISI) wakati wa Kampeni? Kwa andiko lako , MWANAHALISI NI HOPLESS KABISA
 
"Hii serikali ya tano watanzania wana imani sana nayo na wako tayari kuiunga mkono kwa kila jambo linalolenga kuwaletea maendeleo"

Mimi hapana. Sijaamua ama "kuiunga mkono" au "kuikata mkono" kwa sbb ni mapema sana japo ameanza vizuri kiasi chake.

Lakini tusisahau serikali yoyote inayoingia madarakani kwa mara ya kwamba huanza vyema na mikwara mingi kibao.

Hata ya mkwere (J.M.Kikwete mwaka 2005 - 2015) ilianza vyema sana tu kwa kuunda ile tume oliyoongozwa na jaji Kipenka ya kumshughulikia yule polisi aliyekuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Dsm Inspekta Zombe kwa kuongoza mauaji ya wale vijana wafanyabiashara wa madini wa Ulanga (kama sijakosea) ktk msitu wa Mabwepande, Pugu kwa kuwapachika tuhuma za ujambazi kumbe shida yake ni kuwanyang'anya mamilioni ya pesa waliyokuwa nayo wale vijana.

Yaani polisi wao ndio wakawa majambazi kwa kutumia jina lao la polisi, silaha za umma na magwanda yao na kwa kupindua pindua maneno na sheria na kwa sbb tu wao ndio wenye dhamana hiyo!!

Watu wote tukaaminishwa kwamba "tumepata serikali makini" ya "chaguo la Mungu" yenye lengo la kuwaletea wananchi maendeleo. Lakini leo baada ya miaka kumi jamaa kaondoka hata wana CCM wenyewe nyie, ukiwemo wewe mnatema mate chini!!

Tuipe mwaka mmoja tu ili na bunge lianze kazi yake na afanye hata bajeti moja tu. Akiweza ku - maintain pace aliyoanza nayo, mimi nitakubaliana na wewe na hakika nitasema "hii ni serikali makini" na yenye lengo la "kuwaletea wananchi maendeleo" kweli kweli kwa maana ya "mabadiliko ya kweli ndani ya CCM".

Lakini wajuvi wa mambo wanasema, bado CCM ni ileile na falsafa yake ni mfumo uleule wa kulindana na ufisadi.

Na so long as Magufuli yuko hapo kwa tiketi ya CCM na sera za CCM, si ajabu hizi zikawa mbio za sakafuni tu ambazo mwisho wake ni kuishia ukingoni mwa ukuta yaani kudhibitiwa na chama chake!

However, tunamtakia kila la kheri na nashauri wakimzingua saana na hata kuona malengo yake ya kuwatumikia watanzania yanakwazwa na "ma - godfather" wa chama chake, basi atupe kadi ya CCM kuleee abaki kuwa Rais wa Tz.

Na ili hili aliweze, arudishe rasimu ya pili ya katiba ya tume ya jaji Warioba ambayo inamlinda kiongozi wa kuchaguliwa na wananchi kupitia chama chake kutopoteza nafasi yake hiyo i.e urais, ubunge au udiwani au uenyekiti wa kijiji au mtaa hata pale anapokuwa amepoteza sifa ya uanachama wa chake iwe kwa kuancha mwenyewe, kufukuzwa ama vyovyote!
 
mwanahalisi hata ukinipa la bure sitaki, unafki wao wa kuniaminisha Lowassa ni fisadi na tamthilia zao za akina Jason Bourne zilinifanya niamini ni gazeti makini, ila niliyoyashuhudia baadaye halinifai even kwa kulikalia kwenye vumbi.


Samahani mkuu hata wale viongozi wa ukawa nao hutaki kuwasika? maana nao walituaminisha kuwa lowasa ni fisadi papa ila mwisho wa siku kilichotokea kila mtu anaye fuatilia siasa anajua.
 
Mleta nada wacha kujishaua kuwa unaelewa kitu atakochoandika matoleo yajayo
Just stick na Uhuru utasoma yanayokufurahisa,na tazama TBC uangalie Bango, no controversy
 
Huenda habari hii ina chembechembe za ukweli. Sawa na hizo habari mbili nyingine kwenye hiyo front page.
 
KUBENEA anafikiri huu bado ni utawala wa KIKWETE.
 
Nina mashaka na weledi wa waandishi wa gazeti hili! Lilijipatia umaarufu kwa serikali ya awamu ya 4 kuandika kuhusu ufisadi na kumwandika vibaya Rais wa awamu ya 4 Kikwete. Kama lisipojipanga kubadili namna yake ya uandishi, si ajabu kwa hii awamu ya 5 likajifia kimya kimya. Kulazimisha kuandika habari ambazo hazina mashiko ni hatari kwa chombo cha habari maana ni kujimaliza chenyewe.
 
We nyani kasoro mkia hivi ridhiwani kikwete anarekodi gani ya kiutendaji katika nchi hii?
Baba yake ndiye aliyefanikisha ushindi wa Magu kwa yale magari 700 ya kuwasha na vyombo vya dola pamoja na kumlazimisha yule babu wa tume kutangaza hiyo ni mojawapo ya rekodi nzuri ya familia hii katika utendaji kwahiyo subiri pini lizame kwanza
 
lIANDIKE lisiandike, ukweli ni kwamba JMP akijichanganya tu na kuweka madudu kwenye hilo baraza lake la mawaziri, atakua ameumia vibaya sana na anaweza kushusha sana heshma aliyojiwekea hadi sasa. Watu wanabashiri sana sembuse hilo gazeti!!!!!!!!!!
 

Hakuna ubaya katika vyombo vya habari, makundi au watu binafsi kujadili baraza la mawaziri liijalo. Kwa ukweli hii ni haki yao. Mijadala hiyo pia huenda ikamsaidia Raisi na washauri wake kutengeneza baraza zuri-angalau lenye uadilifu, uzalendo na azma ianayoendana na ya viongozi wetu wakuu. Halafu ni muhimu kukumbuka kuwa mawaziri individually na wanapotengeneza mtandao ndiyo chanzo kikuu cha udhaifu mkubwa serikalini-na wanaweza kudhoofisha kimbunga ambacho kinaendelea hivi sasa dhidi ya wovu(kumhujumu Raisi na Taifa). Chonde chonde Mh Raisi tusiweke mvinyo mpya katika chupa dhaifu ! Pia baadhi ya watu wanaopendekeza tayari wanatambulika kuwa political liability-kwa serikali makini ambayo inadhamiria kupambana na ufisadi. Ila mwishowe uamuzi wa nani awe waziri na katika wizara gani ni wa Raisi. Mungu awazidishie hekima Raisi na wasaidizi wake kuutanzua mtihani huu.
 
Balance story yako kwa taarifa ya gazeti la MwanaHaramu.
 

Exactly!
 
mwanahalisi hata ukinipa la bure sitaki, unafki wao wa kuniaminisha Lowassa ni fisadi na tamthilia zao za akina Jason Bourne zilinifanya niamini ni gazeti makini, ila niliyoyashuhudia baadaye halinifai even kwa kulikalia kwenye vumbi.
Kwani Lowasa Si Fisadi?
 



hebu tuwekee na gazeti letu pendwa la UHURU tuone wameandikaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…