The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,968
- 2,957
Kama kichwa ha habari kinavyojieleza hapo juu, gazeti hili la raia mwema lilijengea umashuhuri kwa kuandika habari nzitonzito zilizofanyiwa uchunguzi wa kina, na hivyo likaaminiwa sana na umma wa watanzania.
Ila kwa sasa hali ni tofauti sana. Limekuwa likiandika habari kishabiki na kwenda tofauti na historia na misingi yake. Kwa sasa halina tofauti yoyote na gazeti la uhuru jamvi la habari mzalendo au Tanzania daima ambayo tunayajua yako pale kupigia chapuo na kuvisafisha vyama vyao.
Mimi sii mtaalamu wa vyombo vya habari lakini napenda chombo cha habari kiwe na uzania unaoridhisha kwenye habari kinayoamua kuiandika, na sio kushabikia upande unaokuvutia wewe mwandishi.
Na kwa habari za uchunguzi ndiyo kabisa unapaswa kuja na shahidi nzito zinazotuaminisha uchunguzi wako.
Hivi majuzi wamekuwa wakiandika habari ambazo wameshachagua upande.
Mfano: uchaguzi wa Kenya, wao walikuwa mwanzo mwisho wanamshadadia odinga, ndyo maana hata baada ya Ruto kushinda, wakaja na kichwa cha habari "EIBC yamtangaza Ruto". Walipatwa na mshtuko sana kuona mshindi sio odinga, ikawa aibu kwao kupiga U-turn.
Jambo lingine nilisoma kwenye hili gazeti ni eti " TFF INAIHUJUMU YANGA". Ukianza kusoma ujue hiyo TFF inaihujumu vipi yanga unakuta ni vile vile habari za kufikirika na za kishabiki.
Habari nyingine inayoniboa ni kuleta leta habari za Makonda. Jitu tulishaaza kulisahau wao wamekomaa nalo ata sijui ni kwa manufaa ya nani au wanataka wamkumbushe Mama aliteue?
Naomba nilishauri hili gazeti habari za kishabiki zinachelewesha na kukwaza maendeleo. Andikeni habari za kweli za kiuchunguzi kabla ya kuchagua upande.