Ikiwa CCM ya 2015 ilikuwa imedhoofika kiasi cha wwnanchama wao kushindwa kuvaa sare mitaani kwa kuogopa kuzomewa, chini ya Magu CCM inabebwa na ukatili, ubabe, vitisho, mauaji, watu kupotea, kulazimisha matokeo kwenye chaguzi, kukandamiza upinzani, kuminya uhuru wa kupeana habari, na utawala usiofuta sheria za nchi kwa lengo la kutekeleza kwa nguvu ilani ya CCM ili kuja kuonyesha baadae kwamba walijaribu.
Hebu ajitokeze mtu aiondelee CCM hivyo vitu vyote vinavyoibeba halafu weka uwanja sawa wa ushindani uone kama kutabaki CCM mahali..
CCM ni dhaifu na imekataliwa na Watanzania toka zamani sana. Ipo madarakani kwa sababu ya hila, na kubebwa na mfumo mzima wa dola.
Hata CCM wenyewe wanalijua hili mioyoni mwao ndio maana ukigusia kurekebisha baadhi ya sheria ili ushindani uwe wa haki, wako tayari tuanze vita kuliko kugusa kisingi inayowabakisha madarakani.
Every Tanzanian knows this FACT. And the whole world know this dirty secret.